Kwanza kabisa mie nimecheka sana kwa mleta post kumsifia huyo Graduate kwa kuchoma mahindi, baada ya kusoma nikaona eti kasoma IT, hapo ndio nikazidi kushangaa, bora angekuwa amesoma mambo ya kilimo na biashara anagalau tungesema anafanya research ili aje na bonge la project
Mie nashangaa kwa nini kama unasema lengo ni kuanzia chini, basi asianze hata na kakibanda ka kurekebisha software katika simu, kuistall apps mbali mbali, kutengeneza laptops, Computer nk, yaani kuna watu ni darasa la saba wanapiga hela kwa kujifany amafundi simu na simu zetu zinapona tukiwapelekea, sasa huyo IT wa degree hili limemshinda, si angeenda kwa fundi simu akajifanya mjinga akafundishwa utundu wa kutengeneza halafu akaongeza na elimu yake baada ya mwaka huenda atakuwa mbali.
Mie ninachokiona hapo ni kuwa degree zetu ni za vyeti lakini kichwani hamna kitu, mtu aliyesoma IT lazima atakuwa anamiliki laptop, lazim anajuana na watoto wa mjini wanaouza laptop used, fursa zote hizo hajaziona akaenda kuchoma mahindi, this is a shame for real
Wasomi wengi wa kibongo wakimaliza hutaka kuajiriwa kwa kuwa hawana skills, hivyo wanakimbilia kuajiriwa ili wakafundishwe kazi huko maofisini na watu wenye uzoefu lakini wao huja kwenye ajira vichwa tupu, we fuatilia tu, tafuta Mhasibu aliyegraduate mwambie akufungie mahesabu hawezi, tafuta engineer wa umeme aliyegraduate mwambie akakague mradi wa umeme wa TANESCO utaona madudu tu, hao ndio wasomi wa bongo
Sasa badala ya kusifiana ujinga tuambiane ukweli kuna haja gani ya kumaliza zaidi ya Tsh 10 MIL kwa miaka mitatu aliyotumia kusoma IT halafu anakuja kuchoma mahindi, hiyo 10 mIL si angeanza biashara ya kuuza mahindi jumla na reja reja mapema tu akaachana na huko alikoenda kusoma halafu hawezi hata kutengeneza simu.
THIS IS A SHAME FOR OUR COUNTRY