Jana ndo nimegundua tatizo lililompata jamaa yangu. Ndo tunampoteza hivi hivi. Inasikitisha sana kwa kweli

Jana ndo nimegundua tatizo lililompata jamaa yangu. Ndo tunampoteza hivi hivi. Inasikitisha sana kwa kweli

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Huyu jamaa zamani alikuwa serious mtu kazi. Mnapeana kazi kila mtu anamaliza kwa wakati mnafanya majumuisho mnasonga mbele.

Hapa katikati amebadilika sana.mnaweza peana majukumu nyie mkamaliza yeye mkakuta anasua sua na kuwakwamisha sometimes. Ukimpigia anasema yupo busy sana mara sijui nini.

Sasa mara kadhaa huwa nalazimika kumfuata kwake sababu mi sijaoa ye kaoa. So ananiambia niende tukasaidiane amalize kazi. Ni jamaa yupo vizuri tu kwenye IT.

Jana nikaenda, tumefanya kazi imefika jioni. Anasema tusitishe kwanza. Nikamuuliza why ?tufanye kazi tumalize mi niwahi home. Akanisihi sana. Mwishowe ndo akaniambia anataka kuangalia tamthiliya hizi zinaoneshwa zimetafsiriwa kwa kiswahili.

Nlishtuka sana. Nlidhani anatania. Nikakuta kweli anataka tusogee sebuleni tukae tuangalie.maana muda huo wote tulikaa meza ya dinning.

Kwa kweli ilibidi nimuage mi huwa siwezi kukaa kuangalia mambo ya kijinga. Jamaa amechange kumbe ni tamthiliya hizi za kibwege. Na ukiangalia jamaa hata uongeaji wake umebadilika sana. Amekuwa kama bwabwa.

Anaangalia sana hizo tamthiliya kwenye decoder ya kampuni flani pendwa nchini. Hovyo sana. Amekuwa jinga jinga tu hivi. Amekaa na mkewe na house girl wanafurahi na kukumbushana last week ilikuaje.

Nimeumia sana ndo maan jamaa hata kazi siku hizi hazifanyi kwa wakati. Amekuwa bwege kabisa. Kama haitoshi anazungumza kuwa anatafuta tena CDs za sijui Mkonjani....? Nikamuuliza ni nani anasema "we hujawahi mwona? Ukipanda mabasi ya mikoani wanaweka sana filamu zake"

Nlikumbuka basi moja nlipanda la Tanga nikawaambia wabadilishe hiyo film ya kitoto na mle ndani tumepanda watu wazima. Dereva alipata shida kunielewa.

Kizazi hiki hata ushoga unazidi kwa sababu ya mambo ya kijinga kama haya. Watu wanakuwa mafala sana. Jamaa amekuwa fala na bwege kweli kweli. Jinga kabisa. Analaza na kazi sababu akili yake isha rojoka mpaka mwisho.
 
Mshauri tu aweze kufanya kazi kwa wakati ajue anajigawa vipi ila mambo ya kuangalia tamthilia nadhani ni suala lake binafsi.
 
Mshauri tu aweze kufanya kazi kwa wakati ajue anajigawa vipi ila mambo ya kuangalia tamthilia nadhani ni suala lake binafsi.
Niamini mimi. Kuna vitu ukianza angalia hata akili uwezo wake nao unabadilika. Jamaa amekuwa bwege sana aisee....hakuwa hivi. Hata ukiongea naye analeta leta masikhara ya kwenye hizo tamthiliya. Imagine unaongea naye issue ya maana anakwambia ila we jamaa unafanana na mtu flani wa kwenye Utuglo.

Na anasisitiza kabisa kuwa uanze kufanya moja mbili tatu kama huyo mhusika. Amekuwa bwege sana.
 
Kwahiyo ukaona utaje ushoga?? Km lengo lilikua kusemea ushoga ungesema bila kuhusisha tamthilia hizo.

Maana ni vitu tófauti kabisaaa.

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
Hili mbona limekuumiza sana? Hiyo tabia mimi naichukia hili nikwambie tu kwa kweli. So kma umekwazika ndo hivyo sina namna.
 
Staili ya uandishi wako kumhusu jamaa inachekesha sn.

Nilipoona kichwa cha habari nilidhani yupo taabani hatua za mwisho kwa ugonjwa usio na matibabu,Kumbe amekuwa mpenda series.

Jamaako kaamua kutokuwa serious na maisha plus too na sasa tumeletewa TRAT na TRAB, mwache tu ayafurahie maisha.
 
Kwahiyo ukaona utaje ushoga?? Km lengo lilikua kusemea ushoga ungesema bila kuhusisha tamthilia hizo.

Maana ni vitu tófauti kabisaaa.

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
Unapenda sn Vita wewe mtoto..

Hivi coca kwa nn hupendi kusikia neno ushoga limetajwa na unamrarua mtu yeyote akileta hizo stori?
 
Nina bro mmoja tulikuwa tunakae nae ni mkubwa kwangu ana miaka 39 au 40 sasa huyu jamaa kipindi cha nyuma ana miaka ile ya kujipambania alikuwa ni mtu wa tamthilia sana 😥😥😥zile sijui la relevancha ,sijui maria Clara na the long wait zote anafuatilia na pale enzi zile sisi ikiisha mielekeza jumamosi hao tunaingia zetu kulala.

Naona huo umri ana watoto wakubwa wawili wako darasa la nne mwingine la kwanza ila jamaa anakaa kwao mpaka kesho yaani kapumbaaa yeye kuwa mbele mbele kweny shughuli kama harusi, sijui sendoff na kazi kachagua zile za urojo urojo kujifanya mtu wa mapambo ila anakaa kwao sema mzee ana pesa kidogo halafu ye ndo wa kwanza mdgo wake around 35 ana nyumba mbili ana mke na watoto Tena mkoani ila huyo kapumbaaa tangu kijana.

Kuna kipind wenzie walizamia akaambiwa akadai "je nilienda kufa' yaani muoga ila anapendwa na mother yake ni mzee yupo hai mpaka leo.
 
Back
Top Bottom