Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata mimi wakati naongea na Yesu, nilitoka na summary kuwa "kushika amri/sheria huepusha mshikaji wa hiyo amri/sheria na matatizo yote yatokanayo na kutoshika sheria/amri"Aliyesoma akamaliza na kuelewa naomba nisome comment yake
Inawezekana kabisa Sir, hajakutoa chochote? 😁Mkuu, unamaanisha inawezekana Yesu alinitembelea kwa kuwa mfukoni ni peupe kwa hiyo ikawa kama anakuja kunifariji vile?
Si unaona hapo mwishoni mwa mazungumzo wakati ananiaga, aliniambia niwahi nyumbani nisije kuta chakula kimepoa?Inawezekana kabisa Sir, hajakutoa chochote? 😁
NimeipendaWakuu, kwa kuwa katika muda huu, sisi wenye mamlaka ya kusimamia na kuandaa wataalamu wa baadae (walimu) tupo likizo. Ninaitumia likizo hii kwa kwenda shambani ili kuzalisha chakula.
Wakuu, jana nilibahatika kukutana na Yesu ana kwa ana, nilikuwa natoka shambani narudi nyumbani majira ya mchana kwa ajili ya kupata la mwidebe (kula).
Ghafla, mbele yangu kwa juu nikashangaa wingu safi jeupe linashuka kwa kasi katika ueleko nilipo, punde si muda, likanifikia, lahaula kumbe ulikuwa ni usafiri uliomsafirisha Yesu kutoka mbinguni kuja kuonana na mimi.
Alinikuta njiani. Wakuu, kwa kuwa kuna mambo mengi huwa yananitatiza kila ninaposoma Biblia hasa vitabu vinavyoelezea utumishi wa Yesu Kristo akiwa hapa duniani, ilibidi niruke fasta sana na fursa adhimu kama ile kwa kuongea na kumuomba ufafanuzi kwa yale yanitatizayo.
Mazungumzo baina yangu na Yesu Kristo yalikuwa kama ifuatavyo.
Mimi: Shikamoo Bwana mkubwa Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai.
Yesu: Marhaba mdogo wangu na rafiki yangu Barnabas Mashamba.
Mimi: Hee, unalijua hadi jina langu bila kukuambia.
Yesu: Siyo jina tu, najua hadi idadi ya nywele zako kichwani. By the way, kama wewe umefahamu jina langu pasipo kukutajia, kitu gani kinafanya mimi nisilijue jina lako?
Mimi: Eniwei hivi Yesu Kristo, kwanini ulianzisha amri mpya? Si baba yako kupitia Musa alikuwa ametupatia amri kumi tena akiwa ameziandika kwa kidole chake mwenyewe kwenye mbao mbili za mawe?
Yesu: Amri gani mpya ambayo nilileta?
Mimi: Siku ulipoulizwa swali kuhusu amri ipi ni kuu katika torati na manabii, si ulileta amri mpya wewe.
Mazungumzo yangu na Yesu kristo yalitokana na yale niliyosoma katika kitabu kile cha Mathayo sura ya 22
Mathayo 22:35-40
[35]Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu;
Then one of them, which was a lawyer, asked him a question, tempting him, and saying,
[36]Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?
Master, which is the great commandment in the law?
[37]Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
Jesus said unto him, Thou shalt love the Lord thy God with all thy heart, and with all thy soul, and with all thy mind.
[38]Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
This is the first and great commandment.
[39]Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
And the second is like unto it, Thou shalt love thy neighbour as thyself.
[40]Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.
On these two commandments hang all the law and the prophets.
Yesu: Umesema swali lilihusu amri ipi kuu katika torati na manabii, right?
Mimi: exactly.
Yesu: Wakati natoa jibu, nilisema naleta amri mpya, au nilitoa jibu moja kwa moja kwa swali nililoulizwa kuhusu amri kuu katika torati na manabii?
Mimi: Sijui
Yesu: Hujui kwa kuwa hupendi kusoma.
Mimi: Sasa hapo Yesu naona unanitukana bila kujua elimu yangu, hivi kwanza wewe Yesu ulisoma ukahitimu hata darasa la kwanza?
Yesu: Hapana, sikubahatika kusoma elimu rasmi ya darasani ila nilijua kusoma na kuandika.
Mimi: Umesema kweli maana hata ulifuata msemo wa ndege wafananao huruka pamoja.
Yesu: Kwa nini unasema hivyo.
Mimi: Si ulichagua mitume ambao hawakusoma kama wewe ulivyokuwa kilaza wa elimu ya darasani yenye kumpatia mtu cheti, cheki umenukuliwa hadi kwenye mistari watu wakikuponda kuwa hukusoma, si unaona mwanao wa ukweli kabisa Yohana alitunukulia hilo kwenye Yohana 7:15, na wanafunzi wako waliokuwa wanawaza uvuvi tu wakati watoto wenzao wanakwenda shule nao wakinukuliwa kwenye Matendo 4:13, hivyo tabulalasa aliwachagua matabulalasa wenzake.
Yesu: Turudi kwenye swali lako maana naona unaanza kukwesheni elimu yangu na hapohapo unahitaji ufafanuzi wangu.
Mimi: Nisamehe master, hebu nipe nondo za kiufafanuzi sasa.
Yesu: Swali lililoulizwa lilihusu amri kuu katika torati na manabii, ndiyo au siyo?
Mimi: Ndiyo.
Yesu: Na mimi nilikuwa nimeshafundisha kuwa sikuja kutengua torati na manabii, bali kuzitimiliza, ndiyo au siyo?
Mimi: Ndiyo, tena hiyo nimeisoma kwenye Mathayo 5:17.
Yesu: Ewaaaa, uko sawa. Sasa kama nilishasema sikuja kutangua torati, kwa nini unanisakizia kuwa nilileta amri mpya?
Mimi: Kwa hiyo unamaanisha zile amri zako mbili, ya kumpenda Mungu na kuwapenda wanadamu hazikuwa mpya?
Yesu: Ewaaaa, hebu tusogee hapo kwenye mti tukae kivulini nikupe ujuzi.
Mimi na Yesu tukatembea kukiendea kivuli cha mti kilichokuwa karibu na tukaketi na mazungumzo yetu yakaendelea.
Yesu: Umenieleza umesoma, ulishawahi kusoma hisabati hata kiwango cha kujumlisha na kutoa?
Mimi: Siyo hesabu za kujumlisha na kutoa tu, hadi ma intergration, differentiation, mpaka ma-topology na abstract Algebra, ulishawahi kuzisoma?
Yesu: Nimekuuliza swali na wewe unajibu na kuniuliza swali, unanileta utanzania.
Yesu: Una Biblia hapo?
Mimi: Hapana nina jembe na panga tu.
Yesu: Ukifika nyumbani soma kitabu cha Warumi 13 : 8 , 9, lakini hapa nanukuu toka kichwani kwa ajili yako.
Warumi 13:8-9
[8]Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.
Owe no man any thing, but to love one another: for he that loveth another hath fulfilled the law.
[9]Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
For this, Thou shalt not commit adultery, Thou shalt not kill, Thou shalt not steal, Thou shalt not bear false witness, Thou shalt not covet; and if there be any other commandment, it is briefly comprehended in this saying, namely, Thou shalt love thy neighbour as thyself.
Yesu: Kwenye hiyo aya hasa ya 9, tukifuata hesabu za kujumlisha mwandishi ambaye ni mtume wangu msomi kabisa ambaye hadi aliambiwa na mfalme Agripa kuwa kusoma kwake kwingi kumemgeuza akili (Matendo 26 : 24), mtume Paulo alileta ikwesheni ya kiarithimetikisi kama ifuatavyo.
Usizini + Usiue + Usiibe + Usitami + Amri nyingine yoyote = Mpende jirani yako kama nafsi yako.
Yesu: Sasa, zamu yako kujibu maswali yangu.
Mimi: Yalete, yalete.
Swali la 1
Yesu: Ukizini na mke au mme wa mtu, atakayeumia kihisia na kiakili ni Mungu au mke au mme wa aliyezini.
Mimi: Mke au mme ndiye ataumia kiimoshono, kihisia na huenda hata kiakili. Wengine hufikia hatua ya kuua waliozini na baada ya hapo hujimaliza pia.
Swali la 2
Yesu: Unakubaliana nami kuwa kwenye amri kumi, kuanzia amri ya tano mpaka ya kumi, amri hizo zote zinahusu mapendano ya binadamu na binadamu?
Mimi: Kwani amri hizo ya tano hadi ya kumi zinasemaje?
Yesu: Ndiyo hizo alizonukuu mtume Paulo, sema yeye hakuanza na amri ya tano, kwa faida yako amri zenyewe tuzijumlishe kwenye ikwesheni ya kiarithimetikisi kama ifuatavyo.
Amri ya tano + Amri ya sita + Amri ya saba + Amri ya nane + Amri ya tisa + Amri ya kumi = Mpende jirani yako kama nafsi yako.
Ambazo ini samare.
Waheshimu baba na mama yako + Usiue + Usizini + Usiibe + Usishuhudie uongo + Usitamani mali ya jirani yako = Mpende jirani yako kama nafsi yako.
Yesu: Ukimweshimu mzazi wako, umempenda jirani yako, binadamu mwenzako mwenye cheo cha uzazi.
Yesu: Usipozini, utakuwa umempenda binadamu mwenzako anayemiliki mme au mke ambaye ungezini naye. Kwa kutozini unakuwa umeepusha mambo ya misongo na matatizo ya kiakili yawakumbayo walioziniwa.
Yesu: Usipoiba, umempenda mwenye mali ambayo ungeiiba. Fikiria mtu ameteseka miaka ya kutosha akitafuta mali, wewe kwa siku moja tu unataka uimiliki mali yake.
Yesu: Ni hivyo hivyo kwa zile amri nne za mwanzo, zenyewe zinahusu kumpenda Mungu kama nafsi yako.
Yesu: Kwenye hesabu zetu, tuki-recall from above
Amri ya kwanza + Amri ya pili + Amri ya tatu + Amri ya nne = Mpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako wote, kwa roho yako na kwa akili zako zote.
Yesu: Amri ya kwanza inakataza kuwa na miungu mingine. Kitendo cha kutafuta mungu mwingine na kumuacha Mungu muumbaji, umemwacha Mungu, umependa miungu.
Yesu: Amri ya pili inakataza kuchonga sanamu na kuliweka mahali pa Mungu.
Yesu: Amri ya tatu inakataza kutaja jina la Mungu pasipo sababu za msingi.
Yesu: Ya nne inakumbusha utunzaji wa sabato ambayo Mungu anasema ni mali yake na mimi Yesu Kristo niliwafundisha hata wanafunzi wangu kuwa mimi ndiye Bwana wa Sabato.
Hivyo kwa ikwesheni ya kiarithimetikisi
Usiwe na miungu mingine + Usijifanyie sanamu ya kuchonga + Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako + Ikumbuke siku ya sabato uitakase = Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako na kwa akili zako zote.
Mimi: Nisipozishika, kuna madhara yoyote nitapata.
Yesu: Chukulia mfano huu. Si unayafahamu yale maspika yaitwayo poromondo.
Mimi: Nayafahamu, si yale mara nyingi wanayatumia machinga kutangazia bidhaa zao mfano "Nanunua mabetri mabovu, ya gari, ya sola pamoja na ya pikipikiiiiiiiiii".
Yesu: Ewaaaa, hayohayo. Ukilichukua ukapita mfano karibu na kituo cha Polisi huku unamtukana Mungu kwa sauti inayosaidiwa na kusikika sehemu kubwa na hilo poromondo, Polisi watakukamata?
Mimi: Nadhani watanichukulia kama mwehu flani aliyetoroka matibabu.
Yesu: Vipi kwenye hicho hicho kituo ukapita unamtukana Rais wa nchi?
Mimi: Mhhh, nadhani Tanzania bara jeki, makofi, virungu, na kufunguliwa kesi ya kumtukana Rais vitanihusu.
Yesu: Ewaaa, ila hapo umechemka sehemu moja, ni Tanganyika jeki na siyo ulivyosema wewe.
Mimi: Ni kwa vile tu mfupa hauna ulimi.
Yesu: Kwa nini aliyetukana Mungu aachwe na aliyetukana Rais aadabishwe?
Mimi: Mungu anahitaji kupruviwa uwepo wake, sasa kwa mfano polisi anikamate namtukana Mungu, akifika mahakamani akaulizwa huyo Mungu niliyemtukana anakaa wapi, si atabaki anatoa macho kama kenge anayejifungua.
Yesu: Ewaaa, lakini kwa kuwa Rais ni binadamu anayeonekana, ndiyo maana utashughulikiwa papendikulale.
Yesu: Hapo nchini kwenu, mtu akiiba atafanywaje?
Mimi: Akiwa mwenye bahati, atakingiwa kifua na wakubwa, akiwa na bahati ya wastani atashitakiwa mahakamani, akiwa hana bahati akakutana na wenye hasira kali, atapigwa mawe, atavishwa tairi, mafuta yataletwa na kumwagwa kwenye tairi, moto utawashwa, na habari yake itaishia hapo.
Yesu: Mtu akizini.
Mimi: Mwenye bahati (asiyekamatwa au hata kuhisiwa au akiwa na mme au mke zumbukuku) atapeta tu, mwenye bahati ya wastani ataendewa kwa mafundi na kupewa mimba hata kama ni mwanamme, asiye na bahati (hasa mwanamme) atageuzwa malindalesi, dushe kukatwa na kubanikwa kama mshikaki na watu kulila mbele yake.
Yesu: Hivyo, ukimtukana Mungu, au hata ukitoa kufuru lolote kwa kusema mambo kama vile Mungu hayupo, chonga sanamu liabudu, na vitu vyote kinyume cha zile amri kumi, no wani wili kea, hakuna kesi utafunguliwa mahakamani kwamba umemtukana Mungu, du yu no whai.
Mimi: Sijui
Yesu: Ni kwa sababu, hizo amri zinamhusu Mungu mwenyewe, hivyo hakuna binadamu mwenye mamlaka ya kumuwajibisha mwenzake kisa amemtukana Mungu, hashiki sabato, kajifanyia sanamu n.k, hizo mtoa adhabu ni Mungu. Hivyo amri nne zenye summary ya "mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote... " mtoa adhabu ni Mungu mwenyewe.
Yesu: Lakini ni tofauti na amri zile za upendano wa kibinadamu, zinawahusu binadamu ambao wanaonana, hakuna haja ya kutafuta prufu ya kuthibitisha kama mme au mke wa mtu anaegizisti, hivyo ukimkosea binadamu mwenzako lazima utawajibishwa, utawajibishwa kwa kupelekwa mahakamani au hata kuuliwa papo kwa papo.
Yesu: Kwa ufupi, amri nne za kumhusu Mungu, adhabu za kuzikiuka zitatolewa na Mungu mwenyewe, amri sita zinazohusu mapendano ya wanadamu adhabu ya kwanza mnamalizana ama kibabe au mahakamani hapa hapa duniani na baadaye Mungu pia atatoa adhabu yake.
Mimi: Kwa sentensi yenye maneno yasiyozidi matano, unanishaurije, yaani nipe code ya kuziishi hizo amri maana nimeona kuna pande mbili, kumkosea Mungu au binadamu, bora kwa Mungu kwenyewe hakuna adhabu ya papo kwa papo mpaka wakati ulioamriwa, ila binadamu nimeona wanatoa adhabu za papo kwa papo tena zingine za kikatili sana mpaka najiuliza hao ni binadamu?
Yesu: Shika amri hutaona neno baya.
Mimi: Kama kawaida yako kunukuu toka kwenye maandiko, maana hapo naona umenukuu toka kitabu cha Muhubiri 8:5.
Yesu: Ulikuwa wakati mzuri baina yetu kwa siku ya leo, nitakutembelea tena wiki ijayo, siku, muda na mahali hapa hapa kama ilivyokuwa leo, wahi nyumbani usije kuta chakula kimepoa.
Mimi: Karibu sana Yesu Kristo nyumbani kwangu.
Yesu: Asante sana.
Baada ya mazungumzo hayo, Yesu alipanda chombo chake cha usafiri (wingu), na kwa spidi ya mwanga akatoweka machoni pangu.
Wakuu, kwa kuwa Bwana Yesu Kristo ameniahidi kunitembelea tena wiki ijayo, nitawaletea kitakachojiri kwenye mazungumzo kati yetu hapa hapa JamiiForums saa mbili kamili asubuhi siku ya jumamosi.
Nimerudi ,Mpaka yote Yatimie. Yapi? Mpaka yote yatimie maana yake alimaanisha yakishatimia inaondolewa.
Ukiyajua hayo yaliyotakiwa kutimia, kama yalitimia maana yake Torati iliondoka kwa sababu ilikuwepo tu mpaka yote yatimie.
Tunarudi palepale... Yale yaliyotakiwa kutumia ni sisi kufika kwa Imani/Kristo kama tumefika basi yametimia torati inaondoka kwa kuwa yametimia.
Watu wakishafika kwa Kristo wanafanyaje? Yaani wameshika Sabato/sheria wameona kumbe haiwezi kuwaokoa badala yake wanazidi kuivunja inabidi waende kwa Kristo wakishafika kwa Kristo wanafanyaje?
Kwamba Kristo atawaambia nendeni mkajikaze muendelee kushika🤣 Unachekesha.
1. Kwa nini Yesu alisema, "Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu" (Yohana 14:15), ikiwa Sheria ya Mungu haikuwa na umuhimu kwa waamini?Kama sikosei Mapenzi ya Mungu ni wote tuwe na Uzima.
Je kwa kushika sheria umetimiza mapenzi ya Mungu? Kwamba kwa kishika sheria umepata Uzima?
Nataka nikupe homework kamuulize Mchungaji wako haya maswali akijibu basi sawa leta majibu hapaKama sikosei Mapenzi ya Mungu ni wote tuwe na Uzima.
Je kwa kushika sheria umetimiza mapenzi ya Mungu? Kwamba kwa kishika sheria umepata Uzima?
.
Kol 2:16 SUV
[16] Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
Umeanza vizuri ila kwenye mitume na manabii umetuchanganya, kwakua unasema wapo alafu unajipinga tena kwa kuwakashifuSikupingi, nitakupiga Iwapo maneno yako yatakuwa kinyume na maandiko
Na mpaka sasa sijaona popote ambapo upo kinyume na maandiko
Hadi hapo nimejiridhisha kweli aliyekutokea ni Yesu au huenda ni MALAIKA
Watu watakupinga ila Hadi Leo Mungu anafanya kazi kama zamani ,ni wewe tu uweke mahusihano yako karibu na Mungu
Biblia inasema hata Leo tunao watu kama kina Nabii Eliya ,ambaye alifanya maajabu makubwa achana na Hawa matapeli wenu wanaojiita mitume na manabii wanauzia watu mafuta .
Nilikwambia toka awali nikakuwekea na andiko la mtume Petro alionya jinsi mnavyopotosha nyaraka za Paulo ,ukapuuziaKama mtu asituhukumu kwa vyakula, ama sabato. Inamaana hata Mungu mwenyewe hatuhukumu kwa mambo hayo sababu kuna kitu alifuta hapo juu...
Wapo ila sio Hawa matapeli wanaouzia watu maji na mafuta ,Hawa ambao ni machawa wa serikaliUmeanza vizuri ila kwenye mitume na manabii umetuchanganya, kwakua unasema wapo alafu unajipinga tena kwa kuwakashifu
Hili swali mbona nimeshajibu... Na bado jibu lake umeliandika hapahapa.Kwa nini Yesu alisema yodi moja wala nukta moja ya sheria haitaondoka mpaka mbingu na nchi zitakapopita, ikiwa sheria imeondolewa?
Sheria ina Nguvu gani unayoizungumzia? Mwanadamu kitu muhimu kwake ni kimoja tu Uzima wa milele.Warumi 3:31 inasema imani inaithibitisha sheria. Je, hii haionyeshi kuwa sheria bado ina nguvu kwa waamini?
Upendo unaenda kinyume na Torati. Torati inasema mtu akizini apigwe mawe kitu ambacho ni kinyume na Upendo.3. Ikiwa Kristo alitimiza sheria kwa njia ya upendo, je, hii inamaanisha kuwa upendo unabatilisha sheria ya Mungu?
Ndio yapo. Haya ni baadhi ya Maandiko yanayozungumzia kuondolewa kwa Agano kati ya Israel na Mungu na kisha kusimamishwa agano jipya.4. Amri Kumi, zikiwemo agizo la Sabato, ziliandikwa kwa kidole cha Mungu. Je, kuna maandiko yanayosema kuwa Mungu alibatilisha Amri hizi?
Amri hizi hazijumlishi zile 10 wala hazijumlishi amri yoyote iliyopo kwenye Torati. Umesema Amri za Vyakula ni za Mungu pia lakini Mbinguni hatunywi wala kula kwahiyo kwenye vyakula Mungu alikuwa anajitekenya na kujicheka.5. Katika Ufunuo 14:12, waaminifu wa Kristo wanatajwa kushika "amri za Mungu na imani ya Yesu." Je, unakubaliana kuwa amri hizi zinajumuisha zile kumi?
Sawa mbuzi.... endelea kuwa sawa, hii ni namna ya kuwasilisha ujumbe kwa hadhiraKweli aliewaita makondoo hakukosea
Mkuu, hapa ulimpotezea Yesu muda tu kwani uliacha kumuuliza maswali ya maana badala yake ukawa unamzuga tu. Ungemuuliza kinagaubaga, hivi ni lini na wapi imeandikwa kuwa Muddy ni mwakilishi wa Mungu hapa duniani na kama ni mwakilishi wa Mungu kwanini alikuwa anabaka wake za watu na kuua watu waliompinga yeye kuwa si mtume wa Mungu? Mungu anaruhusuje hivi vituko ya Muddy? Na je baada ya Muddy kuuliwa yuko motoni au karudi kwa mshikaji wake shetani? Naomba Yesu akija tena kukutembelea muulize haya maswali ya maana ufungue akili nduguzo waliopotea na kujiabudia majini.Wakuu, kwa kuwa katika muda huu, sisi wenye mamlaka ya kusimamia na kuandaa wataalamu wa baadae (walimu) tupo likizo. Ninaitumia likizo hii kwa kwenda shambani ili kuzalisha chakula.
Wakuu, jana nilibahatika kukutana na Yesu ana kwa ana, nilikuwa natoka shambani narudi nyumbani majira ya mchana kwa ajili ya kupata la mwidebe (kula).
Ghafla, mbele yangu kwa juu nikashangaa wingu safi jeupe linashuka kwa kasi katika ueleko nilipo, punde si muda, likanifikia, lahaula kumbe ulikuwa ni usafiri uliomsafirisha Yesu kutoka mbinguni kuja kuonana na mimi.
Alinikuta njiani. Wakuu, kwa kuwa kuna mambo mengi huwa yananitatiza kila ninaposoma Biblia hasa vitabu vinavyoelezea utumishi wa Yesu Kristo akiwa hapa duniani, ilibidi niruke fasta sana na fursa adhimu kama ile kwa kuongea na kumuomba ufafanuzi kwa yale yanitatizayo.
Mazungumzo baina yangu na Yesu Kristo yalikuwa kama ifuatavyo.
Mimi: Shikamoo Bwana mkubwa Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai.
Yesu: Marhaba mdogo wangu na rafiki yangu Barnabas Mashamba.
Mimi: Hee, unalijua hadi jina langu bila kukuambia.
Yesu: Siyo jina tu, najua hadi idadi ya nywele zako kichwani. By the way, kama wewe umefahamu jina langu pasipo kukutajia, kitu gani kinafanya mimi nisilijue jina lako?
Mimi: Eniwei hivi Yesu Kristo, kwanini ulianzisha amri mpya? Si baba yako kupitia Musa alikuwa ametupatia amri kumi tena akiwa ameziandika kwa kidole chake mwenyewe kwenye mbao mbili za mawe?
Yesu: Amri gani mpya ambayo nilileta?
Mimi: Siku ulipoulizwa swali kuhusu amri ipi ni kuu katika torati na manabii, si ulileta amri mpya wewe.
Mazungumzo yangu na Yesu kristo yalitokana na yale niliyosoma katika kitabu kile cha Mathayo sura ya 22
Mathayo 22:35-40
[35]Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu;
Then one of them, which was a lawyer, asked him a question, tempting him, and saying,
[36]Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?
Master, which is the great commandment in the law?
[37]Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
Jesus said unto him, Thou shalt love the Lord thy God with all thy heart, and with all thy soul, and with all thy mind.
[38]Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
This is the first and great commandment.
[39]Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
And the second is like unto it, Thou shalt love thy neighbour as thyself.
[40]Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.
On these two commandments hang all the law and the prophets.
Yesu: Umesema swali lilihusu amri ipi kuu katika torati na manabii, right?
Mimi: exactly.
Yesu: Wakati natoa jibu, nilisema naleta amri mpya, au nilitoa jibu moja kwa moja kwa swali nililoulizwa kuhusu amri kuu katika torati na manabii?
Mimi: Sijui
Yesu: Hujui kwa kuwa hupendi kusoma.
Mimi: Sasa hapo Yesu naona unanitukana bila kujua elimu yangu, hivi kwanza wewe Yesu ulisoma ukahitimu hata darasa la kwanza?
Yesu: Hapana, sikubahatika kusoma elimu rasmi ya darasani ila nilijua kusoma na kuandika.
Mimi: Umesema kweli maana hata ulifuata msemo wa ndege wafananao huruka pamoja.
Yesu: Kwa nini unasema hivyo.
Mimi: Si ulichagua mitume ambao hawakusoma kama wewe ulivyokuwa kilaza wa elimu ya darasani yenye kumpatia mtu cheti, cheki umenukuliwa hadi kwenye mistari watu wakikuponda kuwa hukusoma, si unaona mwanao wa ukweli kabisa Yohana alitunukulia hilo kwenye Yohana 7:15, na wanafunzi wako waliokuwa wanawaza uvuvi tu wakati watoto wenzao wanakwenda shule nao wakinukuliwa kwenye Matendo 4:13, hivyo tabulalasa aliwachagua matabulalasa wenzake.
Yesu: Turudi kwenye swali lako maana naona unaanza kukwesheni elimu yangu na hapohapo unahitaji ufafanuzi wangu.
Mimi: Nisamehe master, hebu nipe nondo za kiufafanuzi sasa.
Yesu: Swali lililoulizwa lilihusu amri kuu katika torati na manabii, ndiyo au siyo?
Mimi: Ndiyo.
Yesu: Na mimi nilikuwa nimeshafundisha kuwa sikuja kutengua torati na manabii, bali kuzitimiliza, ndiyo au siyo?
Mimi: Ndiyo, tena hiyo nimeisoma kwenye Mathayo 5:17.
Yesu: Ewaaaa, uko sawa. Sasa kama nilishasema sikuja kutangua torati, kwa nini unanisakizia kuwa nilileta amri mpya?
Mimi: Kwa hiyo unamaanisha zile amri zako mbili, ya kumpenda Mungu na kuwapenda wanadamu hazikuwa mpya?
Yesu: Ewaaaa, hebu tusogee hapo kwenye mti tukae kivulini nikupe ujuzi.
Mimi na Yesu tukatembea kukiendea kivuli cha mti kilichokuwa karibu na tukaketi na mazungumzo yetu yakaendelea.
Yesu: Umenieleza umesoma, ulishawahi kusoma hisabati hata kiwango cha kujumlisha na kutoa?
Mimi: Siyo hesabu za kujumlisha na kutoa tu, hadi ma intergration, differentiation, mpaka ma-topology na abstract Algebra, ulishawahi kuzisoma?
Yesu: Nimekuuliza swali na wewe unajibu na kuniuliza swali, unanileta utanzania.
Yesu: Una Biblia hapo?
Mimi: Hapana nina jembe na panga tu.
Yesu: Ukifika nyumbani soma kitabu cha Warumi 13 : 8 , 9, lakini hapa nanukuu toka kichwani kwa ajili yako.
Warumi 13:8-9
[8]Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.
Owe no man any thing, but to love one another: for he that loveth another hath fulfilled the law.
[9]Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
For this, Thou shalt not commit adultery, Thou shalt not kill, Thou shalt not steal, Thou shalt not bear false witness, Thou shalt not covet; and if there be any other commandment, it is briefly comprehended in this saying, namely, Thou shalt love thy neighbour as thyself.
Yesu: Kwenye hiyo aya hasa ya 9, tukifuata hesabu za kujumlisha mwandishi ambaye ni mtume wangu msomi kabisa ambaye hadi aliambiwa na mfalme Agripa kuwa kusoma kwake kwingi kumemgeuza akili (Matendo 26 : 24), mtume Paulo alileta ikwesheni ya kiarithimetikisi kama ifuatavyo.
Usizini + Usiue + Usiibe + Usitami + Amri nyingine yoyote = Mpende jirani yako kama nafsi yako.
Yesu: Sasa, zamu yako kujibu maswali yangu.
Mimi: Yalete, yalete.
Swali la 1
Yesu: Ukizini na mke au mme wa mtu, atakayeumia kihisia na kiakili ni Mungu au mke au mme wa aliyezini.
Mimi: Mke au mme ndiye ataumia kiimoshono, kihisia na huenda hata kiakili. Wengine hufikia hatua ya kuua waliozini na baada ya hapo hujimaliza pia.
Swali la 2
Yesu: Unakubaliana nami kuwa kwenye amri kumi, kuanzia amri ya tano mpaka ya kumi, amri hizo zote zinahusu mapendano ya binadamu na binadamu?
Mimi: Kwani amri hizo ya tano hadi ya kumi zinasemaje?
Yesu: Ndiyo hizo alizonukuu mtume Paulo, sema yeye hakuanza na amri ya tano, kwa faida yako amri zenyewe tuzijumlishe kwenye ikwesheni ya kiarithimetikisi kama ifuatavyo.
Amri ya tano + Amri ya sita + Amri ya saba + Amri ya nane + Amri ya tisa + Amri ya kumi = Mpende jirani yako kama nafsi yako.
Ambazo ini samare.
Waheshimu baba na mama yako + Usiue + Usizini + Usiibe + Usishuhudie uongo + Usitamani mali ya jirani yako = Mpende jirani yako kama nafsi yako.
Yesu: Ukimweshimu mzazi wako, umempenda jirani yako, binadamu mwenzako mwenye cheo cha uzazi.
Yesu: Usipozini, utakuwa umempenda binadamu mwenzako anayemiliki mme au mke ambaye ungezini naye. Kwa kutozini unakuwa umeepusha mambo ya misongo na matatizo ya kiakili yawakumbayo walioziniwa.
Yesu: Usipoiba, umempenda mwenye mali ambayo ungeiiba. Fikiria mtu ameteseka miaka ya kutosha akitafuta mali, wewe kwa siku moja tu unataka uimiliki mali yake.
Yesu: Ni hivyo hivyo kwa zile amri nne za mwanzo, zenyewe zinahusu kumpenda Mungu kama nafsi yako.
Yesu: Kwenye hesabu zetu, tuki-recall from above
Amri ya kwanza + Amri ya pili + Amri ya tatu + Amri ya nne = Mpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako wote, kwa roho yako na kwa akili zako zote.
Yesu: Amri ya kwanza inakataza kuwa na miungu mingine. Kitendo cha kutafuta mungu mwingine na kumuacha Mungu muumbaji, umemwacha Mungu, umependa miungu.
Yesu: Amri ya pili inakataza kuchonga sanamu na kuliweka mahali pa Mungu.
Yesu: Amri ya tatu inakataza kutaja jina la Mungu pasipo sababu za msingi.
Yesu: Ya nne inakumbusha utunzaji wa sabato ambayo Mungu anasema ni mali yake na mimi Yesu Kristo niliwafundisha hata wanafunzi wangu kuwa mimi ndiye Bwana wa Sabato.
Hivyo kwa ikwesheni ya kiarithimetikisi
Usiwe na miungu mingine + Usijifanyie sanamu ya kuchonga + Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako + Ikumbuke siku ya sabato uitakase = Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako na kwa akili zako zote.
Mimi: Nisipozishika, kuna madhara yoyote nitapata.
Yesu: Chukulia mfano huu. Si unayafahamu yale maspika yaitwayo poromondo.
Mimi: Nayafahamu, si yale mara nyingi wanayatumia machinga kutangazia bidhaa zao mfano "Nanunua mabetri mabovu, ya gari, ya sola pamoja na ya pikipikiiiiiiiiii".
Yesu: Ewaaaa, hayohayo. Ukilichukua ukapita mfano karibu na kituo cha Polisi huku unamtukana Mungu kwa sauti inayosaidiwa na kusikika sehemu kubwa na hilo poromondo, Polisi watakukamata?
Mimi: Nadhani watanichukulia kama mwehu flani aliyetoroka matibabu.
Yesu: Vipi kwenye hicho hicho kituo ukapita unamtukana Rais wa nchi?
Mimi: Mhhh, nadhani Tanzania bara jeki, makofi, virungu, na kufunguliwa kesi ya kumtukana Rais vitanihusu.
Yesu: Ewaaa, ila hapo umechemka sehemu moja, ni Tanganyika jeki na siyo ulivyosema wewe.
Mimi: Ni kwa vile tu mfupa hauna ulimi.
Yesu: Kwa nini aliyetukana Mungu aachwe na aliyetukana Rais aadabishwe?
Mimi: Mungu anahitaji kupruviwa uwepo wake, sasa kwa mfano polisi anikamate namtukana Mungu, akifika mahakamani akaulizwa huyo Mungu niliyemtukana anakaa wapi, si atabaki anatoa macho kama kenge anayejifungua.
Yesu: Ewaaa, lakini kwa kuwa Rais ni binadamu anayeonekana, ndiyo maana utashughulikiwa papendikulale.
Yesu: Hapo nchini kwenu, mtu akiiba atafanywaje?
Mimi: Akiwa mwenye bahati, atakingiwa kifua na wakubwa, akiwa na bahati ya wastani atashitakiwa mahakamani, akiwa hana bahati akakutana na wenye hasira kali, atapigwa mawe, atavishwa tairi, mafuta yataletwa na kumwagwa kwenye tairi, moto utawashwa, na habari yake itaishia hapo.
Yesu: Mtu akizini.
Mimi: Mwenye bahati (asiyekamatwa au hata kuhisiwa au akiwa na mme au mke zumbukuku) atapeta tu, mwenye bahati ya wastani ataendewa kwa mafundi na kupewa mimba hata kama ni mwanamme, asiye na bahati (hasa mwanamme) atageuzwa malindalesi, dushe kukatwa na kubanikwa kama mshikaki na watu kulila mbele yake.
Yesu: Hivyo, ukimtukana Mungu, au hata ukitoa kufuru lolote kwa kusema mambo kama vile Mungu hayupo, chonga sanamu liabudu, na vitu vyote kinyume cha zile amri kumi, no wani wili kea, hakuna kesi utafunguliwa mahakamani kwamba umemtukana Mungu, du yu no whai.
Mimi: Sijui
Yesu: Ni kwa sababu, hizo amri zinamhusu Mungu mwenyewe, hivyo hakuna binadamu mwenye mamlaka ya kumuwajibisha mwenzake kisa amemtukana Mungu, hashiki sabato, kajifanyia sanamu n.k, hizo mtoa adhabu ni Mungu. Hivyo amri nne zenye summary ya "mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote... " mtoa adhabu ni Mungu mwenyewe.
Yesu: Lakini ni tofauti na amri zile za upendano wa kibinadamu, zinawahusu binadamu ambao wanaonana, hakuna haja ya kutafuta prufu ya kuthibitisha kama mme au mke wa mtu anaegizisti, hivyo ukimkosea binadamu mwenzako lazima utawajibishwa, utawajibishwa kwa kupelekwa mahakamani au hata kuuliwa papo kwa papo.
Yesu: Kwa ufupi, amri nne za kumhusu Mungu, adhabu za kuzikiuka zitatolewa na Mungu mwenyewe, amri sita zinazohusu mapendano ya wanadamu adhabu ya kwanza mnamalizana ama kibabe au mahakamani hapa hapa duniani na baadaye Mungu pia atatoa adhabu yake.
Mimi: Kwa sentensi yenye maneno yasiyozidi matano, unanishaurije, yaani nipe code ya kuziishi hizo amri maana nimeona kuna pande mbili, kumkosea Mungu au binadamu, bora kwa Mungu kwenyewe hakuna adhabu ya papo kwa papo mpaka wakati ulioamriwa, ila binadamu nimeona wanatoa adhabu za papo kwa papo tena zingine za kikatili sana mpaka najiuliza hao ni binadamu?
Yesu: Shika amri hutaona neno baya.
Mimi: Kama kawaida yako kunukuu toka kwenye maandiko, maana hapo naona umenukuu toka kitabu cha Muhubiri 8:5.
Yesu: Ulikuwa wakati mzuri baina yetu kwa siku ya leo, nitakutembelea tena wiki ijayo, siku, muda na mahali hapa hapa kama ilivyokuwa leo, wahi nyumbani usije kuta chakula kimepoa.
Mimi: Karibu sana Yesu Kristo nyumbani kwangu.
Yesu: Asante sana.
Baada ya mazungumzo hayo, Yesu alipanda chombo chake cha usafiri (wingu), na kwa spidi ya mwanga akatoweka machoni pangu.
Wakuu, kwa kuwa Bwana Yesu Kristo ameniahidi kunitembelea tena wiki ijayo, nitawaletea kitakachojiri kwenye mazungumzo kati yetu hapa hapa JamiiForums saa mbili kamili asubuhi siku ya jumamosi.
Kama mnanipenda mtazishika Sheria/Amri zangu. Je ni zipi? Ni hizihizi zilizopo Kumbukumbu la Torati ama kuna zingine?1. Kwa nini Yesu alisema, "Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu" (Yohana 14:15), ikiwa Sheria ya Mungu haikuwa na umuhimu kwa waamini?
Kwa macho ya Mungu mambo yote ni Mema na mazuri kabisa ndio maana kuna vilema na wala siyo vibaya.2. Warumi 7:12 inasema, "Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema." Je, ikiwa sheria ni ya haki na njema, kwa nini waamini waiachilie kabisa?
Kwa akili yako unataka uzishike ili ufanye nini wakati tumeelewana Hazileti Uzima wala Wokovu.4.Je, kama Sheria ya Mungu iliondolewa, Kwanini maandiko yanasisitiza kushika amri za Mungu katika siku za mwisho kama inavyoonyeshwa katika Ufunuo 14:12?