Jana nilifanya mazungumzo na Yesu Kristo na kumwomba ufafanuzi kuhusu amri zake kuu mbili za upendo. Na hapa nakuletea mazungumzo hayo kwa ufupi

KAZI NZURI YA FASIHI ANDISHI...HONGERA NA UBARIKIWE.UKO MULE MULE NDANI YA ANDIKO.NINGEKUPINGA KM UNGEKUWA NJE YA ANDIKO
 
Aliyesoma akamaliza na kuelewa naomba nisome comment yake
Hata mimi wakati naongea na Yesu, nilitoka na summary kuwa "kushika amri/sheria huepusha mshikaji wa hiyo amri/sheria na matatizo yote yatokanayo na kutoshika sheria/amri"

Hivyo kwa ufupi.
Shika amri usipate jambo baya.
 
Nimeipenda
 
Nimerudi ,

Mbona unajichanganya sana aisee

Yesu aliposema katika Mathayo 5:17-18 kwamba hakuja kutangua sheria bali kuitimiliza, hakuashiria kuwa sheria ingeondolewa baada ya kutimia kwake. Maneno yake yalionyesha kuwa sheria ilibeba maana pana zaidi ya mfumo wa kafara na taratibu za kimwonekano. Kuitimiliza maana yake ni kuonyesha ukamilifu na dhamira ya sheria, si kuiondoa. Yesu mwenyewe alisema, "Kwa maana, amin, nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapopita, yodi moja wala nukta moja ya sheria haitaondoka, hata yote yatimie." Hii inamaanisha kuwa sheria itaendelea kuwa hai na yenye nguvu, maadamu mbingu na nchi bado zipo.

Yale yaliyotakiwa kutimia ni pamoja na unabii wote kuhusu Kristo, mfumo wa dhabihu ambao ulikuwa kivuli cha dhabihu yake msalabani, na kuonyesha maana halisi ya sheria ya Mungu kwa wanadamu. Hata hivyo, kutimia kwa mambo haya hakumaanishi sheria imeondolewa, bali nafasi yake imebadilika. Warumi 3:31 inathibitisha kwamba imani haibatilishi sheria, bali inaithibitisha. Kwa hivyo, waamini wanaoongozwa na Kristo bado wanaenenda kwa maadili na kanuni za sheria ya Mungu kwa neema, si kwa juhudi za kisheria.

Sheria bado ni mwongozo wa maisha ya haki kwa waamini, lakini haiwezi kuwa chanzo cha wokovu. Warumi 8:3-4 inasema kuwa Kristo alitimiza haki ya torati ndani yetu tunaoongozwa na Roho. Kwa hivyo, ingawa sehemu za sheria kama taratibu za kikuhani zilihitimishwa, amri za maadili za Mungu, ikiwa ni pamoja na Sabato, bado zina nafasi muhimu. Kuitimiliza hakumaanishi kuachana na sheria, bali ni kuishi kwa neema ya Mungu huku tukiendelea kuenenda kwa mapenzi yake yaliyoelezwa katika sheria.

Halafu uwe unajibu maswali yangu

1. Kwa nini Yesu alisema yodi moja wala nukta moja ya sheria haitaondoka mpaka mbingu na nchi zitakapopita, ikiwa sheria imeondolewa?


2. Warumi 3:31 inasema imani inaithibitisha sheria. Je, hii haionyeshi kuwa sheria bado ina nguvu kwa waamini?


3. Ikiwa Kristo alitimiza sheria kwa njia ya upendo, je, hii inamaanisha kuwa upendo unabatilisha sheria ya Mungu?


4. Amri Kumi, zikiwemo agizo la Sabato, ziliandikwa kwa kidole cha Mungu. Je, kuna maandiko yanayosema kuwa Mungu alibatilisha Amri hizi?


5. Katika Ufunuo 14:12, waaminifu wa Kristo wanatajwa kushika "amri za Mungu na imani ya Yesu." Je, unakubaliana kuwa amri hizi zinajumuisha zile kumi?
 
Kama sikosei Mapenzi ya Mungu ni wote tuwe na Uzima.

Je kwa kushika sheria umetimiza mapenzi ya Mungu? Kwamba kwa kishika sheria umepata Uzima?
1. Kwa nini Yesu alisema, "Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu" (Yohana 14:15), ikiwa Sheria ya Mungu haikuwa na umuhimu kwa waamini?


2. Warumi 7:12 inasema, "Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema." Je, ikiwa sheria ni ya haki na njema, kwa nini waamini waiachilie kabisa?


3. Katika Ufunuo 14:12, waaminifu wa Mungu wanaelezewa kama wale "wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu." Je, amri hizi zinajumuisha Sheria ya Mungu, na kama siyo, ni amri zipi zinaelekezwa hapa?


4. Ikiwa sheria ya Mungu haina umuhimu, kwa nini Yesu alisema kwamba hakuna yodi wala nukta moja ya sheria itakayopita mpaka mbingu na nchi zitakapopita (Mathayo 5:18)? Je, mbingu na nchi tayari zimepita?


5. Biblia inasema katika Warumi 3:31, "Je! Basi tunaibatilisha torati kwa imani? Hasha! Bali twaithibitisha torati." Je, waamini wanathibitisha vipi Sheria ya Mungu ikiwa haina umuhimu kwa maisha yao?
 
Kama sikosei Mapenzi ya Mungu ni wote tuwe na Uzima.

Je kwa kushika sheria umetimiza mapenzi ya Mungu? Kwamba kwa kishika sheria umepata Uzima?
Nataka nikupe homework kamuulize Mchungaji wako haya maswali akijibu basi sawa leta majibu hapa

Mathayo 24:20 inasema hivi

"Ombeni kukimbia kwenu isiwe wakati wa baridi au Sabato."


Sasa Mimi nataka ukamuulize haya maswali maana najua wewe huwezi kuyajibu

1. Ikiwa sheria ya Mungu iliondolewa, kwa nini Yesu alisema kwamba waombe "kukimbia kwao mwaka 70AD na Katika nyakati za mwisho isiwe siku ya sabato" (Mathayo 24:20) nikusaidie tu uharibifu wa Yerusalemu ulitokea mwaka wa 70 AD na Bado tunasubiri pia katika siku za mwisho, Je Yesu hakujua kama Sabato imefutwa?


2. Kwa nini Yesu alisisitiza umuhimu wa Sabato kama sehemu ya mapenzi ya Mungu, ikiwa sheria yake ilikuja kufutwa baada ya kufa msalabani?


3. Ikiwa Sabato ilikuwa imetimizwa kama unavyodai, kwa nini Yohana mwaka 100AD aliiona Sanduku la Agano mbinguni katika Ufunuo 11:19, maana humo Kuna Amri kumi?


4.Je, kama Sheria ya Mungu iliondolewa, Kwanini maandiko yanasisitiza kushika amri za Mungu katika siku za mwisho kama inavyoonyeshwa katika Ufunuo 14:12?
 
.

Kol 2:16 SUV
[16] Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;

Tunaposema jamani biblia isisomwe kama gazeti ,hamuelewi ,hiyo Aya umeikurupukia

Tuisome wote Wakolosai 2:16-17 (King James Version):
"Let no man therefore judge you in meat, or in drink, or in respect of an holyday, or of the new moon, or of the sabbath days: Which are a shadow of things to come; but the body is of Christ."

Hapo Zimetajwa Sabbath days hizi zimeelezwa kwenye mambo ya walawi 23 sura nzima ,ni tofauti kabisa na Sabbath day yaani Sabato ya siku ya 7

Halafu umedokoa kamstari kamoja ,kwa Aya hiyo hiyo ,imetaja Vyakula ,vinywaji ,

Nakuswalika

Pombe ni kinywaji ,je kwa kutumia hiyo Wakolosai 2:16 je inaruhusiwa kunywa pombe ?

Hapo ndio utajua Biblia Ina utaratibu wake wa kuisoma
 
Umeanza vizuri ila kwenye mitume na manabii umetuchanganya, kwakua unasema wapo alafu unajipinga tena kwa kuwakashifu
 
Kama mtu asituhukumu kwa vyakula, ama sabato. Inamaana hata Mungu mwenyewe hatuhukumu kwa mambo hayo sababu kuna kitu alifuta hapo juu...
Nilikwambia toka awali nikakuwekea na andiko la mtume Petro alionya jinsi mnavyopotosha nyaraka za Paulo ,ukapuuzia

Haya hapa umetumia Wakolosai 2:16 ili tu Uvunje Sabato na ule nguruwe na kenge

Hiyo Wakolosai 2:16 imetaja vitu vitatu ,

Sabbath days ambazo zimeelezwa sura nzima katika mambo ya walawi 23,humo utakuta na sadaka za vinywaji

Pia pametajwa Vyakula na Vinywaji ambazo zimeelezwa sura nzima mambo ya walawi 23

Wewe umejimegea Sabato na Vyakula vinywaji umekwepa

Mimi nakuuliza Vinywaji vimetajwa, Je na Pombe unakunywa ? Je Mlevi akitumia hiyo Aya utamkataza ikiwa wewe unaitumia kwa malengo yako?


Nakushauri kasome hiyo Wakolosai 2:16 pia katika tafsiri ya KJV, kigiriki utagundua jinsi unavyopotosha maandiko
 
Kwa nini Yesu alisema yodi moja wala nukta moja ya sheria haitaondoka mpaka mbingu na nchi zitakapopita, ikiwa sheria imeondolewa?
Hili swali mbona nimeshajibu... Na bado jibu lake umeliandika hapahapa.

Sheria haitaondoka mpaka mbingu na nchi zitakapopota, sheria haitaondoka mpaka yote yatimie.

Je yote yametimia? Je mbingu na nchi zimepita? Hivi kama vimefanyika basi sheria imeondoka lakini kama bado havijafanyika basi sheria ndio kiongozi wetu.

Yote yametimia? Mbingu na nchi zimepita? (Hii ni mada nyingine) Lakini kiufupi Yote yameshatimia, na Mbingu na nchi zimepita leo tupo nchi mpya na Mbingu mpya.


Warumi 3:31 inasema imani inaithibitisha sheria. Je, hii haionyeshi kuwa sheria bado ina nguvu kwa waamini?
Sheria ina Nguvu gani unayoizungumzia? Mwanadamu kitu muhimu kwake ni kimoja tu Uzima wa milele.
Sheria haina mchango katika uzima hivyo sheria haina nguvu yoyote kuelekea uzima. (Yn 1:17)

Ila Sheria ndio iliyoshikilia nguvu za Mauti. Mauti Nguvu yake ipo kwenye Sheria, sheria ikifa umeua mauti.

3. Ikiwa Kristo alitimiza sheria kwa njia ya upendo, je, hii inamaanisha kuwa upendo unabatilisha sheria ya Mungu?
Upendo unaenda kinyume na Torati. Torati inasema mtu akizini apigwe mawe kitu ambacho ni kinyume na Upendo.

Sheria inasema Toa asilimia 10% ya mapato yako kitu ambacho ni kinyume na Upendo... Upendo unatoa bila kuhesabu.

4. Amri Kumi, zikiwemo agizo la Sabato, ziliandikwa kwa kidole cha Mungu. Je, kuna maandiko yanayosema kuwa Mungu alibatilisha Amri hizi?
Ndio yapo. Haya ni baadhi ya Maandiko yanayozungumzia kuondolewa kwa Agano kati ya Israel na Mungu na kisha kusimamishwa agano jipya.

Ni sawa na kusema kuondolewa kwa Sheria za Agano la huko mlima sinai na kisha kusimamishwa kwa Sheria mpya.

Ebr 10:9 SUV
[9] ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili.


Ebr 8:13 SUV
[13] Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka.

5. Katika Ufunuo 14:12, waaminifu wa Kristo wanatajwa kushika "amri za Mungu na imani ya Yesu." Je, unakubaliana kuwa amri hizi zinajumuisha zile kumi?
Amri hizi hazijumlishi zile 10 wala hazijumlishi amri yoyote iliyopo kwenye Torati. Umesema Amri za Vyakula ni za Mungu pia lakini Mbinguni hatunywi wala kula kwahiyo kwenye vyakula Mungu alikuwa anajitekenya na kujicheka.

Amri/Sheria za Mungu zipo aina mbili zilizokuja kwa nyakati Tofauti.
1. Sheria/Amri ya Dhambi na Mauti (Hii ndio tunaizungumzia toka mwanzo)
2. Sheria ya Roho wa Uzima (Hii ni sheria ambayo hatujaizungumzia kabisa)
(Rejea Rumi 8 : 1-3)

Kwahiyo waaminifu wanatakwa kushika Sheria ya Mungu ya Roho wa Uzima na siyo sheria ya dhambi na mauti kwahiyo hapo ufunuo haizungumzii Amri 10.
 
Mkuu, hapa ulimpotezea Yesu muda tu kwani uliacha kumuuliza maswali ya maana badala yake ukawa unamzuga tu. Ungemuuliza kinagaubaga, hivi ni lini na wapi imeandikwa kuwa Muddy ni mwakilishi wa Mungu hapa duniani na kama ni mwakilishi wa Mungu kwanini alikuwa anabaka wake za watu na kuua watu waliompinga yeye kuwa si mtume wa Mungu? Mungu anaruhusuje hivi vituko ya Muddy? Na je baada ya Muddy kuuliwa yuko motoni au karudi kwa mshikaji wake shetani? Naomba Yesu akija tena kukutembelea muulize haya maswali ya maana ufungue akili nduguzo waliopotea na kujiabudia majini.
 
1. Kwa nini Yesu alisema, "Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu" (Yohana 14:15), ikiwa Sheria ya Mungu haikuwa na umuhimu kwa waamini?
Kama mnanipenda mtazishika Sheria/Amri zangu. Je ni zipi? Ni hizihizi zilizopo Kumbukumbu la Torati ama kuna zingine?

Rum 8:1-2
Sheria zipo katika makundi mawili Sheria ya Dhambi na Mauti na Sheria ya Roho wa Uzima

Katika makundi hayo mawili kundi moja huwezi kulishika ukatimiza hata kama ungekuwa unakesha kanisani.
Sheria alizozungumzia Yesu hazihusiani kabisa na Mwili hata kidogo, yani hazihusiani na kuacha kulima jumamosi, wala kushika panga na kuua mtu haziko hivo, yaani hazihusiahi mwili. Kwahiyo Siyo AMRI KUMI.

2. Warumi 7:12 inasema, "Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema." Je, ikiwa sheria ni ya haki na njema, kwa nini waamini waiachilie kabisa?
Kwa macho ya Mungu mambo yote ni Mema na mazuri kabisa ndio maana kuna vilema na wala siyo vibaya.

Waumini waiachilie kabisa kwa Sababu mwisho wake ni Mauti. Ndiyo maana inaitwa Sheria ya Dhambi na Mauti (Rum 8:2). Kushikiria hii Sheria ni Kukumbatia Mauti na kuuacha Uzima.


4.Je, kama Sheria ya Mungu iliondolewa, Kwanini maandiko yanasisitiza kushika amri za Mungu katika siku za mwisho kama inavyoonyeshwa katika Ufunuo 14:12?
Kwa akili yako unataka uzishike ili ufanye nini wakati tumeelewana Hazileti Uzima wala Wokovu.
Anyway Bado huelewi kuhusu maagano Muhimu mawili ya Mungu.

Mungu Vs Israel.
Mungu Vs Watu Wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…