Jana nilifanya mazungumzo na Yesu Kristo na kumwomba ufafanuzi kuhusu amri zake kuu mbili za upendo. Na hapa nakuletea mazungumzo hayo kwa ufupi

Wakati anaongea ilikuwa haijaondolewa bado. Lakini pia ni Lugha ambayo ilikuwa inatumika wakati huo hakukuwa na Jumatatu wala Jumatano.

Ilibidi atumie maneno kama Sabato ili aelewane na Audience wake.

Hata sasa Sabato Ipo lakini si Sabato unayoijua wewe ya kupika Ijumaa ili ule Jumamosi.


2. Kwa nini Yesu alisisitiza umuhimu wa Sabato kama sehemu ya mapenzi ya Mungu, ikiwa sheria yake ilikuja kufutwa baada ya kufa msalabani?
Hakuna Sehemu ambayo Yesu alisisitiza Sabato bali aliivunja kabisa. Baada ya Kusema yeye na bab yake wanafanya kazi muda wowote hakuna siku wanapumzika.

Yn 5:17-18 SUV
[17] Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi. [18] Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu.

3. Ikiwa Sabato ilikuwa imetimizwa kama unavyodai, kwa nini Yohana mwaka 100AD aliiona Sanduku la Agano mbinguni katika Ufunuo 11:19, maana humo Kuna Amri kumi?
Kuona Sanduku la Agano haimaanishi wewe ndio ufuate Sheria ya Dhambi na Mauti.

Hekalu la Mungu liloko Mbinguni kwa akili yako unajua kuna Jumba kule juu ya Mawingu ambalo ni hekalu, kama unawaza hivi bado sana.


4.Je, kama Sheria ya Mungu iliondolewa, Kwanini maandiko yanasisitiza kushika amri za Mungu katika siku za mwisho kama inavyoonyeshwa katika Ufunuo 14:12?
Sheria/Amri za Mungu hazipaswi kushikwa siku za Mwisho tu, zinatakiwa kwishikwa Leo Tena mara moja tu.

Amri hizo zinazozungumzwa hapo siyo Amri 10. Amri anazozungumza ufunuo 14:12 hazishikwi kwa mwili, na wala kwa kutumia mwili wako huwezi kushika Amri/Sheria kamwe.

Kwahiyo Siyo hizo Amri unazozijua wewe.
 
Una Escape kitoto sana. Hapo umetumia KJV.

Hebu tuone AMP
Colossians 2:16 AMP
[16] Therefore let no one judge you in regard to food and drink or in regard to [the observance of] a festival or a new moon or a Sabbath day.

Haya sasa hao wamesema Sabbath Day. Kiswahili wamesema "au Sabato" wakimaanisha vyote bila kubagua.

Wewe umejimegea Sabato na Vyakula vinywaji umekwepa
Wala sijakwepa nimeandika hivo ili kusave muda. Hakuna mtu kuhukumiwa kwa chochote Kinywaji e.g Coca, Serengeti Lite.
Vyakula e.g Bata, Kambale, Kitimoto
Siku e.g Jumamosi, Jumapili.

Usijekusahau kuwa kupata uzima kwetu si kwa kushika Sheria kama ulivyokuwa unasema huko juu kuwa kushika sheria haichangii wokovu Wokovu.
 
Eti Yesu alikuwa hajui anazungunzia Sabato gani ,lini mtaacha kuzusha uongo?

Kutaja kwamba Sabato ilikuwa inatumika wakati ambapo "hakukuwa na Jumatatu wala Jumatano" ni kupuuza muktadha wa kihistoria. Katika wakati wa Biblia, siku za wiki zilikuwa zinatambulika kwa njia tofauti na si kwa mfumo wa kalenda wa kisasa kama tunavyoujua sasa.

Yesu alikubali kuwa Sabato ni muhimu, lakini alionyesha kuwa kazi ya Mungu inaendelea siku zote. Alisema kuwa yeye na Baba yake wanatenda kazi hata wakati wa Sabato, lakini hakuwa akikiuka sheria ya Sabato kwa maana ya kuzuia mapumziko, bali alifundisha umuhimu wa huruma na ufanisi wa sheria hizo.

Sanduku la Agano halimaanishi kufuata sheria zote za Kiebrania za zamani. Linawakilisha agano la Mungu na wa Israeli, lakini si ishara ya kuendelea kufuata sheria ambazo zimebadilika katika mafundisho ya Yesu.

Sheria za Mungu hazikusudiwi kuwa za kufuatwa tu katika siku za mwisho. Yesu alifundisha kuwa sheria za Mungu zinapaswa kufuatwa kwa moyo wa upendo, siyo kwa utekelezaji wa kifasihi tu.
 
Umeenda kuokoteza huko,lkn Bado upo pale pale

Konyagi ni kinywaji

Swali ,hautahukumiwa kwa kunywa konyagi?
 
Nilikua napita tuu huu uzi...nikiona kichwa cha habari naona uzi wa kilokole...
Ila nime enjoy sana..
"Karibu sana Yesu Kristo nyumbani kwangu"
 
Nakushauri kasome hiyo Wakolosai 2:16 pia katika tafsiri ya KJV, kigiriki utagundua jinsi unavyopotosha maandiko
Sawa mkuu, Upande nimeeleza Mengi ya Maana ukipumzika nakuomba pitia post moja moja huwenda kuna kitu utaongeza.

Nimejibu maswali yako yote, Kwaheri, Umebarikiwa mtakatifu wa Mungu.
 
Umekwepa vzr Hadi nimecheka ,

Hapo pametajwa vinywaji , Nakuuliza Tena Pombe, Kama Konyagi, mbege ,wanzuki ni vinywaji ,Je hautahukumiwa kwa Unywaji pombe?

Kama Konyagi sio kinywaji uje hapa Useme

Na kwa Andiko hilo hilo unavyolitumia ,Na Mlevi atalitumia hivo hivo je atakuwa sahihi?

Sasa twende nikufundishe hiyo Wakolosai 2:16 maana walokole mnakurupukiaga maandiko Hadi mnajikuta mmefungua makanisa na kujiita manabii



Wakolosai 1:16 “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;”

Wahubiri wengi hulitikisa fungu hili lionekane kama linathibitisha kuwa Sabato ilipita, lakini Paulo katika fungu hilo hakumaanisha “Sabato ya wiki”, bali alimaanisha “sabato za mwaka”.

Katika Strong’s Exhaussive Concordance ya Biblia, neno Sabato la kiebrania linamaanisha vitu vifuatavyo…

‘Shabbath’ linalotamkwa, (‘shab-bawth’).

Linalomaanisha…
1) Sabato
1a) sabato
1b) siku ya upatanisho
1c) sabato ya mwaka
1d) sabato ya wiki
.
Angalia Strongs #07676

Neno ‘Sabato’ la kigiriki lililotumika katika Wakolosai 2:16 ni ‘sabbaton’ (sab’-bat-on) linalomaanisha wingi; yaan, “sabato zaidi ya moja” au ‘siku za sabato’. Biblia ya kiingereza KJV imetaja kama “sabbath [days]”

Sabato zilizotajwa katika Wakolosai 2:16 siyo sabato ya wiki ambayo iko katika sheria 10 za Mungu. Ukisoma Walawi 23:23-38 utaona kuwa sabato zilizotajwa katika Wakolosai 2:16 ni “sabato za mwaka” ambazo zinajulikana kama “siku za sikukuu” zilizoadhimishwa kama kivuli kinachoonyesha kuwa katika siku za mbele Masihi angekuja kuwaokoa watu wake. Hii ndiyo maana Paulo anazitaja kama kivuli cha mambo yajayo.

Katika sabato hizo za mwaka ambazo ziliishia msalabani, desturi ilikuwa kama hivi: Siku ya 14 ya mwezi wa kwanza ilikuwa ni pasaka(Law 23:5), kisha siku ya 15 iliyofuata baada ya pasaka ilikuwa ni sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu ambayo ilifanyika kwa muda wa siku 7(Law 23:6). Katika siku ya 1 ya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, ilikuwa ni sabato ambayo haikuruhusiwa kufanya kazi yoyote isipokuwa ile ya kusongenza sadaka, pia katika siku ya 7 ya sikukuu hiyo haikuruhusiwa kufanya kazi yoyote(Law 23:8).

Baada ya sikuku ya mikate isiyotiwa chachu kupita, siku ya pili baada ya Sabato walihesabu Sabato 7, tena zilipita siku 2 baada ya zile Sabato 7 kupita, walihesabu siku 50 mbele ambazo walitoa sadaka za vyakula na vinywaji na ilikuwa ni pumziko takatifu haikuruhusiwa kufanya kazi yoyote(Law 23:9-21)

Harafu katika siku ya 1 ya mwezi wa 7 haikuruhusiwa kufanya kazi yoyote, ilikuwa ni kusanyiko takatifu(Law 23:24-25), na katika siku ya 10 ya mwezi huo wa 7 ilikuwa ni siku ya upatanisho, haikuruhusiwa kufanya kazi yoyote, ilikuwa ni sabato.
_
Walawi 23:27-32 “Lakini siku ya kumi ya mwezi huo wa saba ni siku ya upatanisho;…Nanyi msifanye kazi yo yote siku hiyo; kwa kuwa ni siku ya upatanisho…Itakuwa kwenu sabato ya kustarehe kabisa, nanyi mtazitesa nafsi zenu; siku ya kenda ya mwezi wakati wa jioni, tangu jioni hata jioni, mtaishika hiyo Sabato yenu.”

Halafu tena katika siku ya 15 ya mwezi huo wa 7 ilikuwa ni sikukuu ya vibanda iliyochukua muda wa siku 7, ambapo siku ya 1 haikuruhusiwa kufanya kazi yoyote, na siku ya 8 baada ya sikukuu ya vibanda kuisha haikuruhusiwa kufanya kazi yoyote, ilikuwa ni sabato(Law 23:34-36). Hapa kitu cha muhimu kuzingatia ni kwamba, baada ya Mungu kutaja sikukuu zote hizo, katika Walawi 23:38 zile “siku za sikukuu” ambazo hakuruhusu kufanya kazi yoyote ndani yake, akaziita kuwa ni “Sabato za BWANA.” Hivyo, Sabato hizo ndizo zilizotajwa katika Wakolosai 2:16 na hazimaanishi sabato ya siku ya 7 ya kila wiki, kwa sababu ziliadhimishwa kwa kufuata tarehe maluumu na mwandamo wa mwezi kila mwaka. Kwa kifupi zinaitwa “sabato za mwaka.”

Hata hivyo huu sio ushahidi pekee, tukisoma katika Wakolosai 2:16 tunaona Paulo amezitaja “sabato” hizo kwa kuzijumlisha na “sikukuu”, “mwandamo wa mwezi”, na sadaka za “vyakula”, na “vinywaji” vile vile kama Walawi 23 inavyoweka wazi kuwa “sabato” hizo zilikuwa ndani ya “sikuku za Bwana,” na ziliadhimishwa kwa kufuata tarehe maalumu na “mwandamo wa mwezi,” na wakati wa sikukuu hizo wana wa Israeli walitoa sadaka za “vyakula” na “vinywaji.”

Wana wa Israeli waliadhimisha sikukuu hizo wakiaashiria kuwa Bwana aliwatoa katika nyumba ya utumwa Misri(Kut 12:17, 13:3), hivyo hii ilikuwa ni kivuli au mfano wa kwamba siku moja angekuja Masihi kuwaokoa watu wake kutoka kwenye utumwa wa dhambi. Na kwa kuwa Masihi mwenyewe alishakuja, hivyo haitakiwi kuziazimisha “sikukuu” hizo pamoja na “sabato” zake, na “mwandamo” wake, na “sadaka” zake za vyakula na vinywaji; kwa sababu Masihi ambaye sikukuu hizo zilionyesha kivuli chake alikuwa tayari ameshakuja Yeye Mwenyewe. Hiki ndicho alichomaanisha Paulo katika Wakolosai 2:16 pale aliposema kuwa “…mtu asiwahukumu ninyi(Wakristo) katika (sadaka za)vyakula au vinyinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo…” Lakini Paulo hakumaanisha sabato ya wiki, bali alimaanisha sabato za mwaka zilizofanyika kwa kufuata mwandamo wa mwezi katika zile sikukuu za wana wa Israeli.
 
Sawa mkuu, Upande nimeeleza Mengi ya Maana ukipumzika nakuomba pitia post moja moja huwenda kuna kitu utaongeza.

Nimejibu maswali yako yote, Kwaheri, Umebarikiwa mtakatifu wa Mungu.
Nimepitia zote
 
Sheria za Mungu hazikusudiwi kuwa za kufuatwa tu katika siku za mwisho. Yesu alifundisha kuwa sheria za Mungu zinapaswa kufuatwa kwa moyo wa upendo, siyo kwa utekelezaji wa kifasihi tu.
Manabii walitabiri Agano jipya(Sheria mpya) ambalo halitafanana na hilo la kwanza. (Sheria za Kwanza/Torati)


Yer 31:31-32 SUV
[31] Angalia, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. [32] Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema BWANA.
 
Kwahiyo inaruhusiwa kunywa Pombe ?

Pombe ni kinywaji
Ndio, Konyagi unakunywa kulingana na mwili wako kama unaruhusu na kama unaipenda Kunywa Kabisa chupa za Kutosha.

Ndiyo Pombe ni Kinywaji.

Wenye haunywi Konyagi ili Upate uzima wa Milele? Au ndio wale mnajizuia kula nyama mkiyaita matengenezo ili Mungu awakubali.

Kama upo kwenye hilo Group, bado uelewa wako kuhusu Mungu ni mdogo.

Wewe haunywi konyagi ili upate uzima wa milele?
 
Mbona unaongeza maneno yako hapo,

Agano jipya siyo kuondoa agano la kwanza:, Andiko hilo lipo wazi kabisa linasema kuwa agano jipya litatofautiana na agano la zamani (Torati) kwa sababu watu walilivunja agano la zamani, ingawa Mungu alifanya ahadi na wao. Hii haimaanishi kuwa agano la zamani limetenguliwa, bali agano jipya litakuwa na mabadiliko katika uhusiano wa Mungu na watu wake, ambapo Mungu ataandika sheria zake katika mioyo ya watu badala ya kuwaandikia kwenye mawe, na kuleta uhusiano wa ndani zaidi.
 
Mtoa mada usipende kufanya utani kwenye mambo ya Kimungu usitumie jina la Mungu wako vibaya.Leo ungekuwa mbele ya kiti cha enzi ungeongea kama ulivyoandika?
 
Ok kwahiyo unakunywa Pombe pia kwa mujibu wa Wakolosai 2:16

Unalielewaje hili andiko?

Waefeso 5:18
"Wala msilewe kwa divai, ambayo inazalisha uasherati, bali mjazeni kwa Roho."
Aya hii inakataza kulewa kwa divai, ikionyesha kuwa divai inazalisha uasherati na inahimiza watu kujazwa na Roho Mtakatifu badala ya pombe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…