Una Escape kitoto sana. Hapo umetumia KJV.
Hebu tuone AMP
Colossians 2:16 AMP
[16] Therefore let no one judge you in regard to food and drink or in regard to [the observance of] a festival or a new moon or a Sabbath day.
Haya sasa hao wamesema Sabbath Day. Kiswahili wamesema "au Sabato" wakimaanisha vyote bila kubagua.
Wala sijakwepa nimeandika hivo ili kusave muda. Hakuna mtu kuhukumiwa kwa chochote Kinywaji e.g Coca, Serengeti Lite.
Vyakula e.g Bata, Kambale, Kitimoto
Siku e.g Jumamosi, Jumapili.
Usijekusahau kuwa kupata uzima kwetu si kwa kushika Sheria kama ulivyokuwa unasema huko juu kuwa kushika sheria haichangii wokovu Wokovu.
Umekwepa vzr Hadi nimecheka ,
Hapo pametajwa vinywaji , Nakuuliza Tena Pombe, Kama Konyagi, mbege ,wanzuki ni vinywaji ,Je hautahukumiwa kwa Unywaji pombe?
Kama Konyagi sio kinywaji uje hapa Useme
Na kwa Andiko hilo hilo unavyolitumia ,Na Mlevi atalitumia hivo hivo je atakuwa sahihi?
Sasa twende nikufundishe hiyo Wakolosai 2:16 maana walokole mnakurupukiaga maandiko Hadi mnajikuta mmefungua makanisa na kujiita manabii
Wakolosai 1:16 “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;”
Wahubiri wengi hulitikisa fungu hili lionekane kama linathibitisha kuwa Sabato ilipita, lakini Paulo katika fungu hilo hakumaanisha “Sabato ya wiki”, bali alimaanisha “sabato za mwaka”.
Katika Strong’s Exhaussive Concordance ya Biblia, neno Sabato la kiebrania linamaanisha vitu vifuatavyo…
‘Shabbath’ linalotamkwa, (‘shab-bawth’).
Linalomaanisha…
1) Sabato
1a) sabato
1b) siku ya upatanisho
1c) sabato ya mwaka
1d) sabato ya wiki
.
Angalia Strongs #07676
Neno ‘Sabato’ la kigiriki lililotumika katika Wakolosai 2:16 ni ‘sabbaton’ (sab’-bat-on) linalomaanisha wingi; yaan, “sabato zaidi ya moja” au ‘siku za sabato’. Biblia ya kiingereza KJV imetaja kama “sabbath [days]”
Sabato zilizotajwa katika Wakolosai 2:16 siyo sabato ya wiki ambayo iko katika sheria 10 za Mungu. Ukisoma Walawi 23:23-38 utaona kuwa sabato zilizotajwa katika Wakolosai 2:16 ni “sabato za mwaka” ambazo zinajulikana kama “siku za sikukuu” zilizoadhimishwa kama kivuli kinachoonyesha kuwa katika siku za mbele Masihi angekuja kuwaokoa watu wake. Hii ndiyo maana Paulo anazitaja kama kivuli cha mambo yajayo.
Katika sabato hizo za mwaka ambazo ziliishia msalabani, desturi ilikuwa kama hivi: Siku ya 14 ya mwezi wa kwanza ilikuwa ni pasaka(Law 23:5), kisha siku ya 15 iliyofuata baada ya pasaka ilikuwa ni sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu ambayo ilifanyika kwa muda wa siku 7(Law 23:6). Katika siku ya 1 ya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, ilikuwa ni sabato ambayo haikuruhusiwa kufanya kazi yoyote isipokuwa ile ya kusongenza sadaka, pia katika siku ya 7 ya sikukuu hiyo haikuruhusiwa kufanya kazi yoyote(Law 23:8).
Baada ya sikuku ya mikate isiyotiwa chachu kupita, siku ya pili baada ya Sabato walihesabu Sabato 7, tena zilipita siku 2 baada ya zile Sabato 7 kupita, walihesabu siku 50 mbele ambazo walitoa sadaka za vyakula na vinywaji na ilikuwa ni pumziko takatifu haikuruhusiwa kufanya kazi yoyote(Law 23:9-21)
Harafu katika siku ya 1 ya mwezi wa 7 haikuruhusiwa kufanya kazi yoyote, ilikuwa ni kusanyiko takatifu(Law 23:24-25), na katika siku ya 10 ya mwezi huo wa 7 ilikuwa ni siku ya upatanisho, haikuruhusiwa kufanya kazi yoyote, ilikuwa ni sabato.
_
Walawi 23:27-32 “Lakini siku ya kumi ya mwezi huo wa saba ni siku ya upatanisho;…Nanyi msifanye kazi yo yote siku hiyo; kwa kuwa ni siku ya upatanisho…Itakuwa kwenu sabato ya kustarehe kabisa, nanyi mtazitesa nafsi zenu; siku ya kenda ya mwezi wakati wa jioni, tangu jioni hata jioni, mtaishika hiyo Sabato yenu.”
Halafu tena katika siku ya 15 ya mwezi huo wa 7 ilikuwa ni sikukuu ya vibanda iliyochukua muda wa siku 7, ambapo siku ya 1 haikuruhusiwa kufanya kazi yoyote, na siku ya 8 baada ya sikukuu ya vibanda kuisha haikuruhusiwa kufanya kazi yoyote, ilikuwa ni sabato(Law 23:34-36). Hapa kitu cha muhimu kuzingatia ni kwamba, baada ya Mungu kutaja sikukuu zote hizo, katika Walawi 23:38 zile “siku za sikukuu” ambazo hakuruhusu kufanya kazi yoyote ndani yake, akaziita kuwa ni “Sabato za BWANA.” Hivyo, Sabato hizo ndizo zilizotajwa katika Wakolosai 2:16 na hazimaanishi sabato ya siku ya 7 ya kila wiki, kwa sababu ziliadhimishwa kwa kufuata tarehe maluumu na mwandamo wa mwezi kila mwaka. Kwa kifupi zinaitwa “sabato za mwaka.”
Hata hivyo huu sio ushahidi pekee, tukisoma katika Wakolosai 2:16 tunaona Paulo amezitaja “sabato” hizo kwa kuzijumlisha na “sikukuu”, “mwandamo wa mwezi”, na sadaka za “vyakula”, na “vinywaji” vile vile kama Walawi 23 inavyoweka wazi kuwa “sabato” hizo zilikuwa ndani ya “sikuku za Bwana,” na ziliadhimishwa kwa kufuata tarehe maalumu na “mwandamo wa mwezi,” na wakati wa sikukuu hizo wana wa Israeli walitoa sadaka za “vyakula” na “vinywaji.”
Wana wa Israeli waliadhimisha sikukuu hizo wakiaashiria kuwa Bwana aliwatoa katika nyumba ya utumwa Misri(Kut 12:17, 13:3), hivyo hii ilikuwa ni kivuli au mfano wa kwamba siku moja angekuja Masihi kuwaokoa watu wake kutoka kwenye utumwa wa dhambi. Na kwa kuwa Masihi mwenyewe alishakuja, hivyo haitakiwi kuziazimisha “sikukuu” hizo pamoja na “sabato” zake, na “mwandamo” wake, na “sadaka” zake za vyakula na vinywaji; kwa sababu Masihi ambaye sikukuu hizo zilionyesha kivuli chake alikuwa tayari ameshakuja Yeye Mwenyewe. Hiki ndicho alichomaanisha Paulo katika Wakolosai 2:16 pale aliposema kuwa “…mtu asiwahukumu ninyi(Wakristo) katika (sadaka za)vyakula au vinyinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo…” Lakini Paulo hakumaanisha sabato ya wiki, bali alimaanisha sabato za mwaka zilizofanyika kwa kufuata mwandamo wa mwezi katika zile sikukuu za wana wa Israeli.