Jana nilifanya mazungumzo na Yesu Kristo na kumwomba ufafanuzi kuhusu amri zake kuu mbili za upendo. Na hapa nakuletea mazungumzo hayo kwa ufupi

Wakuu, kwa kuwa katika muda huu, sisi wenye mamlaka ya kusimamia na kuandaa wataalamu wa baadae (walimu) tupo likizo. Ninaitumia likizo hii kwa kwenda shambani ili kuzalisha chakula.

Wakuu, jana nilibahatika kukutana na Yesu ana kwa ana, nilikuwa natoka shambani narudi nyumbani majira ya mchana kwa ajili ya kupata la mwidebe (kula).

Ghafla, mbele yangu kwa juu nikashangaa wingu safi jeupe linashuka kwa kasi katika ueleko nilipo, punde si muda, likanifikia, lahaula kumbe ulikuwa ni usafiri uliomsafirisha Yesu kutoka mbinguni kuja kuonana na mimi.

Alinikuta njiani. Wakuu, kwa kuwa kuna mambo mengi huwa yananitatiza kila ninaposoma Biblia hasa vitabu vinavyoelezea utumishi wa Yesu Kristo akiwa hapa duniani, ilibidi niruke fasta sana na fursa adhimu kama ile kwa kuongea na kumuomba ufafanuzi kwa yale yanitatizayo.

Mazungumzo baina yangu na Yesu Kristo yalikuwa kama ifuatavyo.

Mimi: Shikamoo Bwana mkubwa Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai.
Yesu: Marhaba mdogo wangu na rafiki yangu Barnabas Mashamba.
Mimi: Hee, unalijua hadi jina langu bila kukuambia.
Yesu: Siyo jina tu, najua hadi idadi ya nywele zako kichwani. By the way, kama wewe umefahamu jina langu pasipo kukutajia, kitu gani kinafanya mimi nisilijue jina lako?
Mimi: Eniwei hivi Yesu Kristo, kwanini ulianzisha amri mpya? Si baba yako kupitia Musa alikuwa ametupatia amri kumi tena akiwa ameziandika kwa kidole chake mwenyewe kwenye mbao mbili za mawe?
Yesu: Amri gani mpya ambayo nilileta?
Mimi: Siku ulipoulizwa swali kuhusu amri ipi ni kuu katika torati na manabii, si ulileta amri mpya wewe.

Mazungumzo yangu na Yesu kristo yalitokana na yale niliyosoma katika kitabu kile cha Mathayo sura ya 22

Mathayo 22:35-40
[35]Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu;
Then one of them, which was a lawyer, asked him a question, tempting him, and saying,

[36]Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?
Master, which is the great commandment in the law?

[37]Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
Jesus said unto him, Thou shalt love the Lord thy God with all thy heart, and with all thy soul, and with all thy mind.

[38]Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
This is the first and great commandment.

[39]Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
And the second is like unto it, Thou shalt love thy neighbour as thyself.

[40]Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.
On these two commandments hang all the law and the prophets.

Yesu: Umesema swali lilihusu amri ipi kuu katika torati na manabii, right?
Mimi: exactly.
Yesu: Wakati natoa jibu, nilisema naleta amri mpya, au nilitoa jibu moja kwa moja kwa swali nililoulizwa kuhusu amri kuu katika torati na manabii?
Mimi: Sijui
Yesu: Hujui kwa kuwa hupendi kusoma.

Mimi: Sasa hapo Yesu naona unanitukana bila kujua elimu yangu, hivi kwanza wewe Yesu ulisoma ukahitimu hata darasa la kwanza?
Yesu: Hapana, sikubahatika kusoma elimu rasmi ya darasani ila nilijua kusoma na kuandika.
Mimi: Umesema kweli maana hata ulifuata msemo wa ndege wafananao huruka pamoja.
Yesu: Kwa nini unasema hivyo.
Mimi: Si ulichagua mitume ambao hawakusoma kama wewe ulivyokuwa kilaza wa elimu ya darasani yenye kumpatia mtu cheti, cheki umenukuliwa hadi kwenye mistari watu wakikuponda kuwa hukusoma, si unaona mwanao wa ukweli kabisa Yohana alitunukulia hilo kwenye Yohana 7:15, na wanafunzi wako waliokuwa wanawaza uvuvi tu wakati watoto wenzao wanakwenda shule nao wakinukuliwa kwenye Matendo 4:13, hivyo tabulalasa aliwachagua matabulalasa wenzake.

Yesu: Turudi kwenye swali lako maana naona unaanza kukwesheni elimu yangu na hapohapo unahitaji ufafanuzi wangu.
Mimi: Nisamehe master, hebu nipe nondo za kiufafanuzi sasa.

Yesu: Swali lililoulizwa lilihusu amri kuu katika torati na manabii, ndiyo au siyo?
Mimi: Ndiyo.
Yesu: Na mimi nilikuwa nimeshafundisha kuwa sikuja kutengua torati na manabii, bali kuzitimiliza, ndiyo au siyo?
Mimi: Ndiyo, tena hiyo nimeisoma kwenye Mathayo 5:17.
Yesu: Ewaaaa, uko sawa. Sasa kama nilishasema sikuja kutangua torati, kwa nini unanisakizia kuwa nilileta amri mpya?
Mimi: Kwa hiyo unamaanisha zile amri zako mbili, ya kumpenda Mungu na kuwapenda wanadamu hazikuwa mpya?
Yesu: Ewaaaa, hebu tusogee hapo kwenye mti tukae kivulini nikupe ujuzi.

Mimi na Yesu tukatembea kukiendea kivuli cha mti kilichokuwa karibu na tukaketi na mazungumzo yetu yakaendelea.

Yesu: Umenieleza umesoma, ulishawahi kusoma hisabati hata kiwango cha kujumlisha na kutoa?
Mimi: Siyo hesabu za kujumlisha na kutoa tu, hadi ma intergration, differentiation, mpaka ma-topology na abstract Algebra, ulishawahi kuzisoma?
Yesu: Nimekuuliza swali na wewe unajibu na kuniuliza swali, unanileta utanzania.

Yesu: Una Biblia hapo?
Mimi: Hapana nina jembe na panga tu.
Yesu: Ukifika nyumbani soma kitabu cha Warumi 13 : 8 , 9, lakini hapa nanukuu toka kichwani kwa ajili yako.

Warumi 13:8-9
[8]Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.
Owe no man any thing, but to love one another: for he that loveth another hath fulfilled the law.

[9]Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
For this, Thou shalt not commit adultery, Thou shalt not kill, Thou shalt not steal, Thou shalt not bear false witness, Thou shalt not covet; and if there be any other commandment, it is briefly comprehended in this saying, namely, Thou shalt love thy neighbour as thyself.

Yesu: Kwenye hiyo aya hasa ya 9, tukifuata hesabu za kujumlisha mwandishi ambaye ni mtume wangu msomi kabisa ambaye hadi aliambiwa na mfalme Agripa kuwa kusoma kwake kwingi kumemgeuza akili (Matendo 26 : 24), mtume Paulo alileta ikwesheni ya kiarithimetikisi kama ifuatavyo.

Usizini + Usiue + Usiibe + Usitami + Amri nyingine yoyote = Mpende jirani yako kama nafsi yako.

Yesu: Sasa, zamu yako kujibu maswali yangu.
Mimi: Yalete, yalete.

Swali la 1
Yesu: Ukizini na mke au mme wa mtu, atakayeumia kihisia na kiakili ni Mungu au mke au mme wa aliyezini.
Mimi: Mke au mme ndiye ataumia kiimoshono, kihisia na huenda hata kiakili. Wengine hufikia hatua ya kuua waliozini na baada ya hapo hujimaliza pia.

Swali la 2
Yesu: Unakubaliana nami kuwa kwenye amri kumi, kuanzia amri ya tano mpaka ya kumi, amri hizo zote zinahusu mapendano ya binadamu na binadamu?
Mimi: Kwani amri hizo ya tano hadi ya kumi zinasemaje?
Yesu: Ndiyo hizo alizonukuu mtume Paulo, sema yeye hakuanza na amri ya tano, kwa faida yako amri zenyewe tuzijumlishe kwenye ikwesheni ya kiarithimetikisi kama ifuatavyo.

Amri ya tano + Amri ya sita + Amri ya saba + Amri ya nane + Amri ya tisa + Amri ya kumi = Mpende jirani yako kama nafsi yako.

Ambazo ini samare.

Waheshimu baba na mama yako + Usiue + Usizini + Usiibe + Usishuhudie uongo + Usitamani mali ya jirani yako = Mpende jirani yako kama nafsi yako.

Yesu: Ukimweshimu mzazi wako, umempenda jirani yako, binadamu mwenzako mwenye cheo cha uzazi.

Yesu: Usipozini, utakuwa umempenda binadamu mwenzako anayemiliki mme au mke ambaye ungezini naye. Kwa kutozini unakuwa umeepusha mambo ya misongo na matatizo ya kiakili yawakumbayo walioziniwa.

Yesu: Usipoiba, umempenda mwenye mali ambayo ungeiiba. Fikiria mtu ameteseka miaka ya kutosha akitafuta mali, wewe kwa siku moja tu unataka uimiliki mali yake.

Yesu: Ni hivyo hivyo kwa zile amri nne za mwanzo, zenyewe zinahusu kumpenda Mungu kama nafsi yako.

Yesu: Kwenye hesabu zetu, tuki-recall from above

Amri ya kwanza + Amri ya pili + Amri ya tatu + Amri ya nne = Mpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako wote, kwa roho yako na kwa akili zako zote.

Yesu: Amri ya kwanza inakataza kuwa na miungu mingine. Kitendo cha kutafuta mungu mwingine na kumuacha Mungu muumbaji, umemwacha Mungu, umependa miungu.

Yesu: Amri ya pili inakataza kuchonga sanamu na kuliweka mahali pa Mungu.

Yesu: Amri ya tatu inakataza kutaja jina la Mungu pasipo sababu za msingi.

Yesu: Ya nne inakumbusha utunzaji wa sabato ambayo Mungu anasema ni mali yake na mimi Yesu Kristo niliwafundisha hata wanafunzi wangu kuwa mimi ndiye Bwana wa Sabato.

Hivyo kwa ikwesheni ya kiarithimetikisi

Usiwe na miungu mingine + Usijifanyie sanamu ya kuchonga + Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako + Ikumbuke siku ya sabato uitakase = Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako na kwa akili zako zote.

Mimi: Nisipozishika, kuna madhara yoyote nitapata.

Yesu: Chukulia mfano huu. Si unayafahamu yale maspika yaitwayo poromondo.
Mimi: Nayafahamu, si yale mara nyingi wanayatumia machinga kutangazia bidhaa zao mfano "Nanunua mabetri mabovu, ya gari, ya sola pamoja na ya pikipikiiiiiiiiii".
Yesu: Ewaaaa, hayohayo. Ukilichukua ukapita mfano karibu na kituo cha Polisi huku unamtukana Mungu kwa sauti inayosaidiwa na kusikika sehemu kubwa na hilo poromondo, Polisi watakukamata?
Mimi: Nadhani watanichukulia kama mwehu flani aliyetoroka matibabu.
Yesu: Vipi kwenye hicho hicho kituo ukapita unamtukana Rais wa nchi?
Mimi: Mhhh, nadhani Tanzania bara jeki, makofi, virungu, na kufunguliwa kesi ya kumtukana Rais vitanihusu.
Yesu: Ewaaa, ila hapo umechemka sehemu moja, ni Tanganyika jeki na siyo ulivyosema wewe.
Mimi: Ni kwa vile tu mfupa hauna ulimi.

Yesu: Kwa nini aliyetukana Mungu aachwe na aliyetukana Rais aadabishwe?
Mimi: Mungu anahitaji kupruviwa uwepo wake, sasa kwa mfano polisi anikamate namtukana Mungu, akifika mahakamani akaulizwa huyo Mungu niliyemtukana anakaa wapi, si atabaki anatoa macho kama kenge anayejifungua.
Yesu: Ewaaa, lakini kwa kuwa Rais ni binadamu anayeonekana, ndiyo maana utashughulikiwa papendikulale.

Yesu: Hapo nchini kwenu, mtu akiiba atafanywaje?
Mimi: Akiwa mwenye bahati, atakingiwa kifua na wakubwa, akiwa na bahati ya wastani atashitakiwa mahakamani, akiwa hana bahati akakutana na wenye hasira kali, atapigwa mawe, atavishwa tairi, mafuta yataletwa na kumwagwa kwenye tairi, moto utawashwa, na habari yake itaishia hapo.

Yesu: Mtu akizini.
Mimi: Mwenye bahati (asiyekamatwa au hata kuhisiwa au akiwa na mme au mke zumbukuku) atapeta tu, mwenye bahati ya wastani ataendewa kwa mafundi na kupewa mimba hata kama ni mwanamme, asiye na bahati (hasa mwanamme) atageuzwa malindalesi, dushe kukatwa na kubanikwa kama mshikaki na watu kulila mbele yake.

Yesu: Hivyo, ukimtukana Mungu, au hata ukitoa kufuru lolote kwa kusema mambo kama vile Mungu hayupo, chonga sanamu liabudu, na vitu vyote kinyume cha zile amri kumi, no wani wili kea, hakuna kesi utafunguliwa mahakamani kwamba umemtukana Mungu, du yu no whai.
Mimi: Sijui
Yesu: Ni kwa sababu, hizo amri zinamhusu Mungu mwenyewe, hivyo hakuna binadamu mwenye mamlaka ya kumuwajibisha mwenzake kisa amemtukana Mungu, hashiki sabato, kajifanyia sanamu n.k, hizo mtoa adhabu ni Mungu. Hivyo amri nne zenye summary ya "mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote... " mtoa adhabu ni Mungu mwenyewe.

Yesu: Lakini ni tofauti na amri zile za upendano wa kibinadamu, zinawahusu binadamu ambao wanaonana, hakuna haja ya kutafuta prufu ya kuthibitisha kama mme au mke wa mtu anaegizisti, hivyo ukimkosea binadamu mwenzako lazima utawajibishwa, utawajibishwa kwa kupelekwa mahakamani au hata kuuliwa papo kwa papo.

Yesu: Kwa ufupi, amri nne za kumhusu Mungu, adhabu za kuzikiuka zitatolewa na Mungu mwenyewe, amri sita zinazohusu mapendano ya wanadamu adhabu ya kwanza mnamalizana ama kibabe au mahakamani hapa hapa duniani na baadaye Mungu pia atatoa adhabu yake.

Mimi: Kwa sentensi yenye maneno yasiyozidi matano, unanishaurije, yaani nipe code ya kuziishi hizo amri maana nimeona kuna pande mbili, kumkosea Mungu au binadamu, bora kwa Mungu kwenyewe hakuna adhabu ya papo kwa papo mpaka wakati ulioamriwa, ila binadamu nimeona wanatoa adhabu za papo kwa papo tena zingine za kikatili sana mpaka najiuliza hao ni binadamu?

Yesu: Shika amri hutaona neno baya.

Mimi: Kama kawaida yako kunukuu toka kwenye maandiko, maana hapo naona umenukuu toka kitabu cha Muhubiri 8:5.

Yesu: Ulikuwa wakati mzuri baina yetu kwa siku ya leo, nitakutembelea tena wiki ijayo, siku, muda na mahali hapa hapa kama ilivyokuwa leo, wahi nyumbani usije kuta chakula kimepoa.
Mimi: Karibu sana Yesu Kristo nyumbani kwangu.
Yesu: Asante sana.

Baada ya mazungumzo hayo, Yesu alipanda chombo chake cha usafiri (wingu), na kwa spidi ya mwanga akatoweka machoni pangu.

Wakuu, kwa kuwa Bwana Yesu Kristo ameniahidi kunitembelea tena wiki ijayo, nitawaletea kitakachojiri kwenye mazungumzo kati yetu hapa hapa JamiiForums saa mbili kamili asubuhi siku ya jumamosi.​
Hakikisha umetoa fungu la 10 mkuu.
 
Sikupingi, nitakupiga Iwapo maneno yako yatakuwa kinyume na maandiko

Na mpaka sasa sijaona popote ambapo upo kinyume na maandiko

Hadi hapo nimejiridhisha kweli aliyekutokea ni Yesu au huenda ni MALAIKA

Watu watakupinga ila Hadi Leo Mungu anafanya kazi kama zamani ,ni wewe tu uweke mahusihano yako karibu na Mungu

Biblia inasema hata Leo tunao watu kama kina Nabii Eliya ,ambaye alifanya maajabu makubwa achana na Hawa matapeli wenu wanaojiita mitume na manabii wanauzia watu mafuta .
Huyo alikuwa anawasilisha somo kwa njia ya uigizaji na wengi mmevutiwa kusoma kutokana na mbinu aliyoitumia kwenye uwasilishaji wake na yuko kanisani sasa hivi.
 
Umesoma wapi ? Mnadanganywa sana na kina mwamposa
2 Kor 3:13-16 SUV
[13] nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba Waisraeli wasitazame sana mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika; [14] ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo; [15] ila hata leo, torati ya Musa isomwapo, utaji huikalia mioyo yao. [16] Lakini wakati wo wote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa.

Nisitoe maelezo yoyote bali nikuwekee tafsiri ya kiswahili rahisi huwenda luna kitu utaelewa...

2 Wakorintho 3:13-17 TKU
[13] Hatuko kama Musa, ambaye alifunika uso wake ili watu wa Israeli wasiendelee kuona kuwa utaratibu wa zamani wa kumtumikia Mungu ulikuwa unaelekea mwisho. [14] Lakini mioyo yao ilikuwa imefungwa. Na hata leo, watu wale wanapolisoma agano la kale, fahamu zao zinakuwa zimefunikwa. Ni kwa kupitia Yesu Kristo tu agano la kale linaondolewa. [15] Ndiyo, hata leo, wanaposoma sheria ya Musa, fahamu zao zimefunikwa. [16] Lakini, kama maandiko yanavyosema juu ya Musa, “Kila anapomgeukia Bwana, ufahamu wake unafunuliwa.” [17] Katika maandiko hayo Bwana ni Roho, na palipo na Roho wa Bwana, pana uhuru.
 
Tatizo lenu nyie jamaa ,mnatumia vibaya sana Maandiko ya Paulo ,ndio maana Leo matapeli wanaojiita mitume na manabii wamekuwa wengi sana

Katika 2 Petro 3:15-16, Petro anaonya wazi kuhusu upotoshaji wa nyaraka za Paulo, akisema kuwa kuna mambo magumu kueleweka ambayo watu wasio na elimu hupotosha kwa uvunjifu wao wenyewe.

Hii inadhihirisha kuwa nyaraka za Paulo hazipaswi kufasiriwa kirahisi bila muktadha wa maandiko yote ya Biblia. Kwa msingi huu, hoja ya kwamba sheria au amri za Mungu hazina kazi si sahihi na inatokana na upotoshaji wa maandiko.

Katika 2 Wakorintho 3:13-16, Paulo hakukataa sheria za Musa, bali alieleza jinsi torati ya Agano la Kale ilivyokuwa mwongozo wa muda kuelekea wokovu kupitia Kristo. Aya ya 13 inasema kuwa Musa alifunika uso wake ili Waisraeli wasione mwisho wa utukufu wa sheria, lakini hii haimaanishi kwamba sheria haikuwa na maana. Badala yake, sheria ilikusudiwa kuwa daraja la kuelekea neema ya Kristo, kama inavyothibitishwa katika Wagalatia 3:24, ambayo inasema kwamba torati ilikuwa mwalimu wetu wa kutuleta kwa Kristo ili tupate haki kwa imani.

Aya ya 14 inazungumzia fikira za Waisraeli zilizotiwa uzito, zikimaanisha kwamba walishindwa kuelewa maana ya kweli ya sheria kwa sababu walikuwa na mioyo migumu. Hata leo, watu wengi wanaposoma sheria, wanashindwa kuona uzuri wake kwa sababu hawajamgeukia Kristo. Lakini, aya ya 16 inasema kuwa wakati wowote wanapomgeukia Bwana, pazia linaondolewa. Hii inaonyesha kuwa Kristo hakufuta sheria bali alitimiza sheria na kuzifanya kuwa na maana kamilifu kwa wale waliomwamini. Hivyo, kudai kwamba sheria za Mungu hazina kazi ni kupinga wazi mafundisho ya Biblia, hasa maneno ya Yesu katika Mathayo 5:17, aliposema, "Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza."

Kwa msingi huu, hoja inayodai kwamba sheria za Mungu hazina kazi inapuuza ukweli wa Biblia kuwa sheria ni takatifu, ya haki, na ya uzima (Warumi 7:12).

Sheria si njia ya wokovu, lakini inatufundisha juu ya dhambi na hitaji letu la neema kupitia Kristo. Kupinga sheria ni sawa na kupinga mpango wa Mungu wa wokovu na maisha matakatifu.

Naomba unijibu maswali yafuatayo

1. Ikiwa sheria ya Mungu haina kazi, kwa nini Yesu alisema kuwa hakufuta torati bali alikuja kuitimiliza (Mathayo 5:17)?

2. Kama sheria ilikuwa batili, kwa nini Paulo alisema kuwa torati ni takatifu na amri zake ni za haki na za uzima (Warumi 7:12)?

3. Je, ni kwa njia gani tunapaswa kufahamu dhambi kama si kupitia sheria, kama Paulo alivyosema katika Warumi 3:20, kwamba kwa sheria hutoka ujuzi wa dhambi?

UKINIJIBU HAYO MASWALI NITASHUKURU SANA ,UKIYAKIMBIA SAWA
 
Naangalia juu naomwona yesu namwambia nipe tano nie gwara we ndo mchizi wangu. Hapo naona ulipiga kitu cha arusha kwanza ndo ukapiga story na bwana jesus
 
Katika 2 Wakorintho 3:13-16, Paulo hakukataa sheria za Musa, bali alieleza jinsi torati ya Agano la Kale ilivyokuwa mwongozo wa muda kuelekea wokovu kupitia Kristo.
Katu yangu na wewe nani anashindwa kwa kutafsiri vizuri... Unasoma bible nusunusu kwa kulenga yale unayoona yanakufaa.

Wewe ni moja ya watu uliyesikia na kujua ukweli lakini hutaki kuamini kwa sababu kila ukitaka kuamini pazia linakalia moyo wako.
Umesema Torati ya Musa ilikuwa mwongozo wa Muda kuelekea wokovu, sasa tumepata wokovu tunahaja gani tena ya kukumbatia kile kilichokuwa cha muda?

Hebu soma hapa kwa kiswahili rahisi kabisa...

Wagalatia 3:23-25 TKU
[23] Kabla ya aliye mwaminifu kuja, sheria ilituweka sisi kama wafungwa. Hatukuwa huru hadi imani hii inayokuja ilipofunuliwa kwetu. [24] Nina maana kuwa sheria ilikuwa ni mlezi aliyetusimamia tu hadi Kristo alipokuja. Baada ya kuja kwake, tungefanyika kuwa wenye haki mbele za Mungu kwa njia ya imani. [25] Sasa kwa sababu imani hii imekuja, hatuhitaji tena kusimamiwa na kulelewa na sheria.

Soma hapa aya ya 25 kwa kiswahili ulichozoea...

Gal 3:25 SUV
[25] Lakini, iwapo imani imekuja, hatupo tena chini ya kiongozi.

Kwa kuwa Kristo amekuja, hatuhitaji Tena Torati kama msimamizi wetu bali hata sasa tupo kwa Kristo hatuhitaji kiongozi mwingine isipokuwa Kristo.

Na ukiendelea kushikiria sheria unabaki Mfungwa mpaka pale itakapofuniliwa Torati huondoka palipo na kristo.

Narejea kujibu maswali yako
 
Amri mbili;
1. Ya kwanza,mpende Mungu kwa uwezo wako wote,,
Halafu kwa upendo huo unaompenda Mungu,na wewe jipende hivyo hivyo.
Yaani usitoe hela zako zote sadaka Kanisani halafu useme Mungu amekutuma.
2. Halafu mpende ndugu yako kama unavyojipenda wewe.
Again,usisahau maslahi yako eti kwa ajili unataka kuonyesha upendo kwa ndugu au jirani.
Love your neighbhour as yourself.

YOU CONTINUE TO PRACTICE ALL THE WAYS TO BREAK THE LAWS OF GOD AND CREATION FOR YOU HAVE FORGOTTEN WHAT THEY ARE. I SHALL REMIND YOU OF A FEW OF THEM HERE:

COMMANDMENTS OF GOD YOU SHALL HAVE NO OTHER GODS THAN THE GOD CREATOR AND ABIDE WITHIN THE LAWS OF THE CREATION WHICH ENCOMPASSES ALL.

YOU SHALL NOT MAKE FOR YOURSELVES IDOLS AND FALSE IMAGES TO WORSHIP AS GODS FOR THEREIN YOU GIVE POWER INTO THE HANDS OF EVIL, FOR WITHIN YOUR HEARTPLACE MUST DWELL A DOUBT OF THE FULNESS OF CREATOR IF YOU EMPOWER OTHER THAN GOD AND THE GOD FRAGMENT WITHIN SELF.

The repercussions of breaking this law are usually most heinous indeed and once Pproduced; i.e., the lands depleted, the addictions of the mother to the babe, the disease unto the children, etc., you can see that the “sin” or error, of the parent is visited most surely upon the child and the grandchildren and so on.

YOU SHALL LOVE THY LORD GOD WITH ALL THY HEART, SOUL AND BEING. (YOU SHALL LOVE GOD AS THINESELF!)

Most of you hate and despise yourselves beyond comprehension. If you live according to the Laws there is balance and these things of negative destruction do not come into beingness.

YOU SHALL NOT USE THE NAME OF GOD IRREVERENTLY, NOR USE OF IT TO SWEAR TO A FALSEHOOD.

If you do this thing, then you have proven that your own word is without merit and further, you are calling into play great power which also gives unto evil the gift of your strength.

REMEMBER THE SABBATH TO KEEP IT HOLY.

This is possibly the most truly misunderstood of all directives and has been most incorrectly applied according to man. YE SHALL ALLOW OF TIME TO COMMUNE IN TRUTH WITH GOD IN HIS TEMPLE WHICH IS WITHIN SELF . YOU SHALL REFRESH OF YOUR MINDS THE TRUTH OF THE DIRECTIVES AND ABIDE IN TRUTH AND HONOR. IT REPRESENTS YOUR TIME OF DEVOTION AND COMMUNION TO GOD AND THE CREATION THAT YOU NOT STRAY INTO THE TRAP OF EVIL. IT MOST CERTAINLY DOES NOT MEAN THAT YOU GO FORTH INTO A MAN-MADE TEMPLE TO HEAR ANOTHER MAN'S INTERPRETATION OF GOD. YOU GO FORTH INTO THE VERY PLACES WHERE EVIL HAS SET UP THE IDOLS FOR YOU TO WORSHIP. OH LITTLE ONES OF THE LIE, MERCY BE UNTO YOU FOR YOU HAVE SLEPT TOO LONG.

HONOR YOUR FATHER AND YOUR MOTHER THAT YOUR LIFE SHALL BE LONG IN THE LAND GIVEN UNTO YOUR CARE.

So be it. Give appreciation, honor, care and respect unto those earth humans who gave you passageway into human format--BUT HONOR THY FATHER, CREATOR, AND MOTHER, THE CREATION, OF WHOM YOU ARE SOLELY COMPRISED. THROUGH YOUR DISHONOR THEREOF YOU HAVE SLAIN YOURSELVES.

YOU SHALL NOT MURDER THY FELLOW HU-MAN.

There is naught to misunderstand in this edict. Murder is the willful taking of another's life through intent, assisted suicide or suicide, or any such act, with knowledge and intent. That, brothers, includes WAR!

YOU MUST NOT COMMIT ADULTERY

. Now here is one you have written and rewritten to suit of yourselves. You have given of your own definitions to words to suit the lust and desires of the human physical form. “ADULTERY” is any sexual copulation of any form, outside the state of contractual marriage and that act within a marriage EXCEPT between A HUSBAND AND WIFE to procreate offspring to form family segments. WHAT HAVE YE ONES DONE WITH THIS COMMANDMENT?

Oh, I see, you don't like that? So you have brought overpopulation, disease, murder through abortion, child abuse and all manner of gross evil against yourselves and your peoples. You, as a planet, cannot survive the burden of that which you have brought forth through the re-writing of that Law to please your human physical lust. So be it. Whether or not you like of it, it is a most reasonable Law indeed .

YOU MUST NOT STEAL.

That, too, is most simple to understand--you take nothing that is another's, whether it be tangible or idea; especially his ideas, for they are most privately his possession. You must always give honor and appreciation for the use of another's ideas even if he has departed your dimension. Dear ones, even the heinous ideas--for thy evil brother should be given his due credit if his ideas have precipitated evil. Ye shall cease in the practice of giving credit to the Lord thy God for the corruption and heinous acts of evil.

YOU MUST NOT LIE.

Well, this too has been written and re-written and totally misunderstood. A “lie” is not some smattering of words from the lips. The LIE is the practice and projection of evil in any form. You, for instance, have become people of the lie and subjects of the Prince of Lies. This one would require all the rest of this document to fully discuss.

YOU MUST NOT COVET OR ENVY THAT WHICH BELONGS TO THY NEIGHBOR.

You must be pleased over that which is another's if it be worthy and ye shall try to earn in honor and integrity that which may be equal. You shall not take that which is your friend's or your neighbor's nor shall you desire to take his property for your own and leave him without that which is his.

COMMANDMENTS OF SATANIC PRACTICE

SATANIC COMMANDMENTS AND RULES ONLY AMOUNT TO “DEGREE” OF ONE LAW--BREAK ALL LAWS OF GOD CREATOR AND THE CREATION--

IN SUBSTANCE, ACT, AND COMPLETELY IN LITERAL COMPLETION!

LET THAT SEEP INTO YOUR CONSCIOUSNESS FOR A MOMENT

IT DOES NOT ULTIMATELY MEAN TO MURDER AN INSECT OR AN ANIMAL--IT MEANS EXACTLY WHAT IT SAYS--MURDER A HUMAN BEING. KILL IT AND DEFILE IT IN ANY MANNER POSSIBLE BEFORE OR AFTER DEATH OF THE VICTIM BODY, FOR THE INTENT IS TO DEFILE THE SOUL WHICH IS THE FRAGMENT OF ETERNAL LIFE.

IT FURTHER MEANS THAT IT IS NOT ENOUGH IF “SEVERAL” KILL A HUMAN ENTITY--IT MEANS THAT EACH SATAN FOLLOWER MUST KILL TO FULFILL HIS INDIVIDUAL COMMANDMENT REQUIREMENTS.

SINCE ADULTS ARE NOT SO EASILY TRAPPED AND UTILIZED, THE CHILDREN--YOUR CHILDREN--ARE TAKEN FOR THESE DEATH RITUALS. MOTIVES, THE POLICE WILL SEEK--THEY WILL MOST OFTEN FIND NONE. FURTHER, IN YOUR CURRENT TIME, THE VERY ACT OF MURDER WILL BE HIDDEN BEHIND THE FACADE OF THEFT, DRUGS, AND ALL MANNER OF FALSE DISGUISES. THE MORE ATROCIOUS THE METHOD AND CIRCUMSTANCE, THE HIGHER THE RANK OF THE LEADER OF THE INDIVIDUAL COVENS.

WHEN THE GOING GETS ROUGH AND THE BOOM COMES DOWN, THE DEVIL WILL DESERT HIS OWN ONCE THEY CAN NO LONGER BE USEFUL AS TOOLS. HE WILL PROMISE YOU POWER, GREATNESS, WEALTH AND ON AND ON WILL HE PROMISE YOU “THINGS”. THEN, AS ABRUPTLY, WHEN YOUR USEFULNESS IS SERVED, YOU WILL BE THROWN TO THE WINDS TO REAP OF THE PAIN ALONE AND BE DESTROYED.

THE ONSET WILL BE SUBTLE, JUST A LITTLE LIE, JUST A LITTLE GREED, JUST A LITTLE TAKING, JUST A BIT OF ADULTERY, JUST ONE HIT OF A DRUG TO TEST IT (note that drugs are now addicting from first trial! That is no accident!), JUST A LITTLE BIT OF VIOLENCE AND LAWBREAKING TO GET A “HIGH”, JUST A LITTLE BIT OF A RIPOFF OF YOUR COMPANY OR NEIGHBOR IN SECRET. THEN, A LITTLE MORE AND A LITTLE MORE AND FINALLY YOU ARE SWALLOWED ALIVE

GOD MAY BE MOST MYSTERIOUS IN HIS WONDERS TO PERFORM. BUT, DEAR ONES, EVIL IS NOT EVEN CONCERNED ENOUGH TO BE MYSTERIOUS! PLAY UNTO MAN'‟S FEARS AND BLINDNESS AND YOU CAN CONTROL HIM UNTO HUMAN DEATH.
 
Katu yangu na wewe nani anashindwa kwa kutafsiri vizuri... Unasoma bible nusunusu kwa kulenga yale unayoona yanakufaa.

Wewe ni moja ya watu uliyesikia na kujua ukweli lakini hutaki kuamini kwa sababu kila ukitaka kuamini pazia linakalia moyo wako.
Umesema Torati ya Musa ilikuwa mwongozo wa Muda kuelekea wokovu, sasa tumepata wokovu tunahaja gani tena ya kukumbatia kile kilichokuwa cha muda?

Hebu soma hapa kwa kiswahili rahisi kabisa...

Wagalatia 3:23-25 TKU
[23] Kabla ya aliye mwaminifu kuja, sheria ilituweka sisi kama wafungwa. Hatukuwa huru hadi imani hii inayokuja ilipofunuliwa kwetu. [24] Nina maana kuwa sheria ilikuwa ni mlezi aliyetusimamia tu hadi Kristo alipokuja. Baada ya kuja kwake, tungefanyika kuwa wenye haki mbele za Mungu kwa njia ya imani. [25] Sasa kwa sababu imani hii imekuja, hatuhitaji tena kusimamiwa na kulelewa na sheria.

Soma hapa aya ya 25 kwa kiswahili ulichozoea...

Gal 3:25 SUV
[25] Lakini, iwapo imani imekuja, hatupo tena chini ya kiongozi.

Kwa kuwa Kristo amekuja, hatuhitaji Tena Torati kama msimamizi wetu bali hata sasa tupo kwa Kristo hatuhitaji kiongozi mwingine isipokuwa Kristo.

Na ukiendelea kushikiria sheria unabaki Mfungwa mpaka pale itakapofuniliwa Torati huondoka palipo na kristo.

Narejea kujibu maswali yako
Acha maneno mengi,Rudi ujibu maswali ,halafu ulichoeleza hapa ,ni wazi wewe ni wale Petro aliowasemanayapotosha maandiko ya Paulo

Torati ya Musa haikuwa mwongozo wa muda kuelekea wokovu bali ni sehemu ya mpango wa Mungu wa milele kwa mwanadamu. Katika Mathayo 5:17, Yesu alisema wazi kuwa hakukuja kuitangua Torati bali kuitimiliza. Hii ina maana kwamba Torati bado ina umuhimu wake katika kuelewa haki ya Mungu na njia zake. Kristo hakuondoa sheria, bali alitimiza maana yake kamili kwa kutufunulia jinsi inavyotumika ndani ya neema na imani. Ikiwa Torati ni ya muda tu, kwa nini Mungu aliihusisha na maagizo ya milele kama Sabato na amri za maadili? Je, Kristo kuja kunafuta hizo sheria za msingi?

Kudai kwamba hatuhitaji tena Torati kwa sababu Kristo amekuja ni kupotosha maandiko. Torati si adui wa wokovu, bali ni kielelezo cha tabia ya Mungu na viwango vyake vya haki. Warumi 3:31 inasema, "Je! Basi, tunaibatilisha sheria kwa imani? Hasha! Kinyume chake tunaithibitisha sheria." Hii inaonyesha kwamba imani kwa Kristo haiondoi umuhimu wa sheria, bali inaimarisha nafasi yake katika maisha ya waumini. Katika Wagalatia 3:24-25, Paulo anasema sheria ilitulea kama mlezi, lakini je, kulelewa hakumaanishi kuwa tunapaswa kuheshimu msingi wa kile tulichofundishwa? Kwa nini uamini kuwa mlezi huyo hakufundisha thamani ya kudumu?

Pia, kushikilia kwamba kushika Torati ni kubaki mfungwa kiroho ni kufasiri vibaya maandiko. Sheria ilitolewa kwa upendo ili kutufundisha kuhusu dhambi na kutupeleka kwa Kristo (Wagalatia 3:24). Kristo hakutufanya huru kutoka kwa wajibu wa kumtii Mungu bali kutoka katika adhabu ya dhambi. Wakati tunapokea neema, tunaitimiza Torati kupitia maisha yaliyoongozwa na Roho Mtakatifu (Warumi 8:4). Kama kuendelea kushikilia Torati ni kubaki "mfungwa kiroho," unafafanua vipi Warumi 7:12 inayosema "Kwa hiyo sheria ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema"? Je, hili si pingamizi kwa tafsiri yako?

Kwa hivyo, hoja kwamba Torati imeondolewa kabisa si sahihi. Wokovu unapatikana kwa imani kwa Kristo, lakini Torati bado inatuonyesha mapenzi ya Mungu na kutusaidia kuishi maisha matakatifu. Kuitupilia mbali ni kupoteza kipengele muhimu cha Neno la Mungu.
 
Huyo alikuwa anawasilisha somo kwa njia ya uigizaji na wengi mmevutiwa kusoma kutokana na mbinu aliyoitumia kwenye uwasilishaji wake na yuko kanisani sasa hivi.
Mbinu ya uwasilishaji somo ilikuwa excellent.
Lengo la somo limefanikiwa 100%
Ila mbwembwe kidogo zilitaka kuzidi. Next time apunguze mbwembwe ili kuokoa muda na kutokuwachosha wasomaji.
 
1. Ikiwa sheria ya Mungu haina kazi, kwa nini Yesu alisema kuwa hakufuta torati bali alikuja kuitimiliza (Mathayo 5:17)?
Wewe unahisi Sheria ina kazi gani?

Yesu anawataja waliomtangulia kuwa ni WEZI, mwizi huja ila kuiba na kuua.
Waliomtangulia hasa unafikri ni akina nani? MUSA/TORATI ndio aliyemtangulia KRISTO na wote lengo lao ni moja ni kumwokoa mwanadamu.

Lakini Yesu anasema waliotangulia ni WEZI bali yeye pekee ndio Mwokozi.

Yn 10:7-10 SUV
[7] Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo. [8] Wote walionitangulia ni wevi na wanyang’anyi; lakini kondoo hawakuwasikia. [9] Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho. [10] Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.

Hivyo ukiniuliza kazi kubwa ya Sheria mimi nakujibu kazi yake ni KUUA/KUCHINJA/KUANGAMIZA.

Paulo ni moja ya wale waliolewa neno hili anakiri hapa namna Amri ilivyomuua hapo kabla ya kujua ukweli...

Rum 7:9-10 SUV
[9] Nami nalikuwa hai hapo kwanza bila sheria; ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, nami nikafa. [10] Nikaona ile amri iletayo uzima ya kuwa kwangu mimi ilileta mauti.

Mtu yeyote anayetoa huduma ya Amri Kumi mtu huyo anatoa huduma ya mauti.
2 Kor 3:7 SUV
[7] Basi, ikiwa huduma ya mauti, iliyoandikwa na kuchorwa katika mawe...(Nafikri unajua ni kitu gani kiliandikwa kwenye mawe)

Kwanini Yesu alisema hakuja kutangua bali kutimiliza sheria
Kutimiliza ni sawa na kukamilisha.

Lengo la Torati ilikuwa ni kuwapa watu uzima na kubarikiwa(mith 3:1-6, Kumb 28:1-14, 30:19).

Lakini sheria haikuweza kuwapa watu uzima bali kila Kifo ndio kilizidi kuongezeka, kuvunja sheria moja tu adhabu yake ilikuwa ni kuuawa ama kutengwa.

Baada ya Torati kufeli Kristo ndiye aliyeamua kukamilisha Lengo la Sheria la kuleta Uzima. Kwahiyo alivyosema hakuja Kuifuta bali alikuja kukamilisha Lengo la Sheria. Na baada ya hapo hatuna haja tena ya Kushika Torati ili tupate Uzima bali ni kazi Yetu ni kuamini aliyekamilisha kazi ya Sheria.

Naendelea swali la pili.
 
Katika 2 Wakorintho 3:13-16, Paulo hakukataa sheria za Musa, bali alieleza jinsi torati ya Agano la Kale ilivyokuwa mwongozo wa muda kuelekea wokovu kupitia Kristo.

Torati ya Musa haikuwa mwongozo wa muda kuelekea wokovu bali ni sehemu ya mpango wa Mungu wa milele kwa mwanadamu.
Inaonekana hakuna unachoamini kwa sabubu hueleweki unatetea kipi. Jipange ueleweke kwanza ndio Tuzungumze.
 
Ikiwa Torati ni ya muda tu, kwa nini Mungu aliihusisha na maagizo ya milele kama Sabato na amri za maadili? Je, Kristo kuja kunafuta hizo sheria za msingi?
Kwa uelewa wako inaonesha huijui Sabato ni nini?

Pia hata sheria huijui vizuri.

  1. Sheria inakataza usiwashe moto siku ya sabato
  2. Sheria inakataza kulima mazao mawili kwenye shamba moja.
  3. Sheria inakutaka utoe asilimia kumi ya mapato yako.
  4. Sheria inazuia kuvaa nguo zenye material tofauti(yaani usivae suruali ya Pamba na shati la nylon)
  5. Sheria inakuhitaji usiache mchawi aishi, sheria inakutaka umuue yule atakayevunja sabato.
Je Kwenye hayo nimekosea? Kama sijakosea unahisi inawezekana hayo yote kuyashika? Hebu angalia watu kama Iran, Afghanistan wanaojaribu angalau nukta kushika sheria uone ulivyotofauti nao.
 
Wakuu, kwa kuwa katika muda huu, sisi wenye mamlaka ya kusimamia na kuandaa wataalamu wa baadae (walimu) tupo likizo. Ninaitumia likizo hii kwa kwenda shambani ili kuzalisha chakula.

Wakuu, jana nilibahatika kukutana na Yesu ana kwa ana, nilikuwa natoka shambani narudi nyumbani majira ya mchana kwa ajili ya kupata la mwidebe (kula).

Ghafla, mbele yangu kwa juu nikashangaa wingu safi jeupe linashuka kwa kasi katika ueleko nilipo, punde si muda, likanifikia, lahaula kumbe ulikuwa ni usafiri uliomsafirisha Yesu kutoka mbinguni kuja kuonana na mimi.

Alinikuta njiani. Wakuu, kwa kuwa kuna mambo mengi huwa yananitatiza kila ninaposoma Biblia hasa vitabu vinavyoelezea utumishi wa Yesu Kristo akiwa hapa duniani, ilibidi niruke fasta sana na fursa adhimu kama ile kwa kuongea na kumuomba ufafanuzi kwa yale yanitatizayo.

Mazungumzo baina yangu na Yesu Kristo yalikuwa kama ifuatavyo.

Mimi: Shikamoo Bwana mkubwa Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai.
Yesu: Marhaba mdogo wangu na rafiki yangu Barnabas Mashamba.
Mimi: Hee, unalijua hadi jina langu bila kukuambia.
Yesu: Siyo jina tu, najua hadi idadi ya nywele zako kichwani. By the way, kama wewe umefahamu jina langu pasipo kukutajia, kitu gani kinafanya mimi nisilijue jina lako?
Mimi: Eniwei hivi Yesu Kristo, kwanini ulianzisha amri mpya? Si baba yako kupitia Musa alikuwa ametupatia amri kumi tena akiwa ameziandika kwa kidole chake mwenyewe kwenye mbao mbili za mawe?
Yesu: Amri gani mpya ambayo nilileta?
Mimi: Siku ulipoulizwa swali kuhusu amri ipi ni kuu katika torati na manabii, si ulileta amri mpya wewe.

Mazungumzo yangu na Yesu kristo yalitokana na yale niliyosoma katika kitabu kile cha Mathayo sura ya 22

Mathayo 22:35-40
[35]Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu;
Then one of them, which was a lawyer, asked him a question, tempting him, and saying,

[36]Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?
Master, which is the great commandment in the law?

[37]Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
Jesus said unto him, Thou shalt love the Lord thy God with all thy heart, and with all thy soul, and with all thy mind.

[38]Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
This is the first and great commandment.

[39]Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
And the second is like unto it, Thou shalt love thy neighbour as thyself.

[40]Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.
On these two commandments hang all the law and the prophets.

Yesu: Umesema swali lilihusu amri ipi kuu katika torati na manabii, right?
Mimi: exactly.
Yesu: Wakati natoa jibu, nilisema naleta amri mpya, au nilitoa jibu moja kwa moja kwa swali nililoulizwa kuhusu amri kuu katika torati na manabii?
Mimi: Sijui
Yesu: Hujui kwa kuwa hupendi kusoma.

Mimi: Sasa hapo Yesu naona unanitukana bila kujua elimu yangu, hivi kwanza wewe Yesu ulisoma ukahitimu hata darasa la kwanza?
Yesu: Hapana, sikubahatika kusoma elimu rasmi ya darasani ila nilijua kusoma na kuandika.
Mimi: Umesema kweli maana hata ulifuata msemo wa ndege wafananao huruka pamoja.
Yesu: Kwa nini unasema hivyo.
Mimi: Si ulichagua mitume ambao hawakusoma kama wewe ulivyokuwa kilaza wa elimu ya darasani yenye kumpatia mtu cheti, cheki umenukuliwa hadi kwenye mistari watu wakikuponda kuwa hukusoma, si unaona mwanao wa ukweli kabisa Yohana alitunukulia hilo kwenye Yohana 7:15, na wanafunzi wako waliokuwa wanawaza uvuvi tu wakati watoto wenzao wanakwenda shule nao wakinukuliwa kwenye Matendo 4:13, hivyo tabulalasa aliwachagua matabulalasa wenzake.

Yesu: Turudi kwenye swali lako maana naona unaanza kukwesheni elimu yangu na hapohapo unahitaji ufafanuzi wangu.
Mimi: Nisamehe master, hebu nipe nondo za kiufafanuzi sasa.

Yesu: Swali lililoulizwa lilihusu amri kuu katika torati na manabii, ndiyo au siyo?
Mimi: Ndiyo.
Yesu: Na mimi nilikuwa nimeshafundisha kuwa sikuja kutengua torati na manabii, bali kuzitimiliza, ndiyo au siyo?
Mimi: Ndiyo, tena hiyo nimeisoma kwenye Mathayo 5:17.
Yesu: Ewaaaa, uko sawa. Sasa kama nilishasema sikuja kutangua torati, kwa nini unanisakizia kuwa nilileta amri mpya?
Mimi: Kwa hiyo unamaanisha zile amri zako mbili, ya kumpenda Mungu na kuwapenda wanadamu hazikuwa mpya?
Yesu: Ewaaaa, hebu tusogee hapo kwenye mti tukae kivulini nikupe ujuzi.

Mimi na Yesu tukatembea kukiendea kivuli cha mti kilichokuwa karibu na tukaketi na mazungumzo yetu yakaendelea.

Yesu: Umenieleza umesoma, ulishawahi kusoma hisabati hata kiwango cha kujumlisha na kutoa?
Mimi: Siyo hesabu za kujumlisha na kutoa tu, hadi ma intergration, differentiation, mpaka ma-topology na abstract Algebra, ulishawahi kuzisoma?
Yesu: Nimekuuliza swali na wewe unajibu na kuniuliza swali, unanileta utanzania.

Yesu: Una Biblia hapo?
Mimi: Hapana nina jembe na panga tu.
Yesu: Ukifika nyumbani soma kitabu cha Warumi 13 : 8 , 9, lakini hapa nanukuu toka kichwani kwa ajili yako.

Warumi 13:8-9
[8]Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.
Owe no man any thing, but to love one another: for he that loveth another hath fulfilled the law.

[9]Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
For this, Thou shalt not commit adultery, Thou shalt not kill, Thou shalt not steal, Thou shalt not bear false witness, Thou shalt not covet; and if there be any other commandment, it is briefly comprehended in this saying, namely, Thou shalt love thy neighbour as thyself.

Yesu: Kwenye hiyo aya hasa ya 9, tukifuata hesabu za kujumlisha mwandishi ambaye ni mtume wangu msomi kabisa ambaye hadi aliambiwa na mfalme Agripa kuwa kusoma kwake kwingi kumemgeuza akili (Matendo 26 : 24), mtume Paulo alileta ikwesheni ya kiarithimetikisi kama ifuatavyo.

Usizini + Usiue + Usiibe + Usitami + Amri nyingine yoyote = Mpende jirani yako kama nafsi yako.

Yesu: Sasa, zamu yako kujibu maswali yangu.
Mimi: Yalete, yalete.

Swali la 1
Yesu: Ukizini na mke au mme wa mtu, atakayeumia kihisia na kiakili ni Mungu au mke au mme wa aliyezini.
Mimi: Mke au mme ndiye ataumia kiimoshono, kihisia na huenda hata kiakili. Wengine hufikia hatua ya kuua waliozini na baada ya hapo hujimaliza pia.

Swali la 2
Yesu: Unakubaliana nami kuwa kwenye amri kumi, kuanzia amri ya tano mpaka ya kumi, amri hizo zote zinahusu mapendano ya binadamu na binadamu?
Mimi: Kwani amri hizo ya tano hadi ya kumi zinasemaje?
Yesu: Ndiyo hizo alizonukuu mtume Paulo, sema yeye hakuanza na amri ya tano, kwa faida yako amri zenyewe tuzijumlishe kwenye ikwesheni ya kiarithimetikisi kama ifuatavyo.

Amri ya tano + Amri ya sita + Amri ya saba + Amri ya nane + Amri ya tisa + Amri ya kumi = Mpende jirani yako kama nafsi yako.

Ambazo ini samare.

Waheshimu baba na mama yako + Usiue + Usizini + Usiibe + Usishuhudie uongo + Usitamani mali ya jirani yako = Mpende jirani yako kama nafsi yako.

Yesu: Ukimweshimu mzazi wako, umempenda jirani yako, binadamu mwenzako mwenye cheo cha uzazi.

Yesu: Usipozini, utakuwa umempenda binadamu mwenzako anayemiliki mme au mke ambaye ungezini naye. Kwa kutozini unakuwa umeepusha mambo ya misongo na matatizo ya kiakili yawakumbayo walioziniwa.

Yesu: Usipoiba, umempenda mwenye mali ambayo ungeiiba. Fikiria mtu ameteseka miaka ya kutosha akitafuta mali, wewe kwa siku moja tu unataka uimiliki mali yake.

Yesu: Ni hivyo hivyo kwa zile amri nne za mwanzo, zenyewe zinahusu kumpenda Mungu kama nafsi yako.

Yesu: Kwenye hesabu zetu, tuki-recall from above

Amri ya kwanza + Amri ya pili + Amri ya tatu + Amri ya nne = Mpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako wote, kwa roho yako na kwa akili zako zote.

Yesu: Amri ya kwanza inakataza kuwa na miungu mingine. Kitendo cha kutafuta mungu mwingine na kumuacha Mungu muumbaji, umemwacha Mungu, umependa miungu.

Yesu: Amri ya pili inakataza kuchonga sanamu na kuliweka mahali pa Mungu.

Yesu: Amri ya tatu inakataza kutaja jina la Mungu pasipo sababu za msingi.

Yesu: Ya nne inakumbusha utunzaji wa sabato ambayo Mungu anasema ni mali yake na mimi Yesu Kristo niliwafundisha hata wanafunzi wangu kuwa mimi ndiye Bwana wa Sabato.

Hivyo kwa ikwesheni ya kiarithimetikisi

Usiwe na miungu mingine + Usijifanyie sanamu ya kuchonga + Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako + Ikumbuke siku ya sabato uitakase = Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako na kwa akili zako zote.

Mimi: Nisipozishika, kuna madhara yoyote nitapata.

Yesu: Chukulia mfano huu. Si unayafahamu yale maspika yaitwayo poromondo.
Mimi: Nayafahamu, si yale mara nyingi wanayatumia machinga kutangazia bidhaa zao mfano "Nanunua mabetri mabovu, ya gari, ya sola pamoja na ya pikipikiiiiiiiiii".
Yesu: Ewaaaa, hayohayo. Ukilichukua ukapita mfano karibu na kituo cha Polisi huku unamtukana Mungu kwa sauti inayosaidiwa na kusikika sehemu kubwa na hilo poromondo, Polisi watakukamata?
Mimi: Nadhani watanichukulia kama mwehu flani aliyetoroka matibabu.
Yesu: Vipi kwenye hicho hicho kituo ukapita unamtukana Rais wa nchi?
Mimi: Mhhh, nadhani Tanzania bara jeki, makofi, virungu, na kufunguliwa kesi ya kumtukana Rais vitanihusu.
Yesu: Ewaaa, ila hapo umechemka sehemu moja, ni Tanganyika jeki na siyo ulivyosema wewe.
Mimi: Ni kwa vile tu mfupa hauna ulimi.

Yesu: Kwa nini aliyetukana Mungu aachwe na aliyetukana Rais aadabishwe?
Mimi: Mungu anahitaji kupruviwa uwepo wake, sasa kwa mfano polisi anikamate namtukana Mungu, akifika mahakamani akaulizwa huyo Mungu niliyemtukana anakaa wapi, si atabaki anatoa macho kama kenge anayejifungua.
Yesu: Ewaaa, lakini kwa kuwa Rais ni binadamu anayeonekana, ndiyo maana utashughulikiwa papendikulale.

Yesu: Hapo nchini kwenu, mtu akiiba atafanywaje?
Mimi: Akiwa mwenye bahati, atakingiwa kifua na wakubwa, akiwa na bahati ya wastani atashitakiwa mahakamani, akiwa hana bahati akakutana na wenye hasira kali, atapigwa mawe, atavishwa tairi, mafuta yataletwa na kumwagwa kwenye tairi, moto utawashwa, na habari yake itaishia hapo.

Yesu: Mtu akizini.
Mimi: Mwenye bahati (asiyekamatwa au hata kuhisiwa au akiwa na mme au mke zumbukuku) atapeta tu, mwenye bahati ya wastani ataendewa kwa mafundi na kupewa mimba hata kama ni mwanamme, asiye na bahati (hasa mwanamme) atageuzwa malindalesi, dushe kukatwa na kubanikwa kama mshikaki na watu kulila mbele yake.

Yesu: Hivyo, ukimtukana Mungu, au hata ukitoa kufuru lolote kwa kusema mambo kama vile Mungu hayupo, chonga sanamu liabudu, na vitu vyote kinyume cha zile amri kumi, no wani wili kea, hakuna kesi utafunguliwa mahakamani kwamba umemtukana Mungu, du yu no whai.
Mimi: Sijui
Yesu: Ni kwa sababu, hizo amri zinamhusu Mungu mwenyewe, hivyo hakuna binadamu mwenye mamlaka ya kumuwajibisha mwenzake kisa amemtukana Mungu, hashiki sabato, kajifanyia sanamu n.k, hizo mtoa adhabu ni Mungu. Hivyo amri nne zenye summary ya "mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote... " mtoa adhabu ni Mungu mwenyewe.

Yesu: Lakini ni tofauti na amri zile za upendano wa kibinadamu, zinawahusu binadamu ambao wanaonana, hakuna haja ya kutafuta prufu ya kuthibitisha kama mme au mke wa mtu anaegizisti, hivyo ukimkosea binadamu mwenzako lazima utawajibishwa, utawajibishwa kwa kupelekwa mahakamani au hata kuuliwa papo kwa papo.

Yesu: Kwa ufupi, amri nne za kumhusu Mungu, adhabu za kuzikiuka zitatolewa na Mungu mwenyewe, amri sita zinazohusu mapendano ya wanadamu adhabu ya kwanza mnamalizana ama kibabe au mahakamani hapa hapa duniani na baadaye Mungu pia atatoa adhabu yake.

Mimi: Kwa sentensi yenye maneno yasiyozidi matano, unanishaurije, yaani nipe code ya kuziishi hizo amri maana nimeona kuna pande mbili, kumkosea Mungu au binadamu, bora kwa Mungu kwenyewe hakuna adhabu ya papo kwa papo mpaka wakati ulioamriwa, ila binadamu nimeona wanatoa adhabu za papo kwa papo tena zingine za kikatili sana mpaka najiuliza hao ni binadamu?

Yesu: Shika amri hutaona neno baya.

Mimi: Kama kawaida yako kunukuu toka kwenye maandiko, maana hapo naona umenukuu toka kitabu cha Muhubiri 8:5.

Yesu: Ulikuwa wakati mzuri baina yetu kwa siku ya leo, nitakutembelea tena wiki ijayo, siku, muda na mahali hapa hapa kama ilivyokuwa leo, wahi nyumbani usije kuta chakula kimepoa.
Mimi: Karibu sana Yesu Kristo nyumbani kwangu.
Yesu: Asante sana.

Baada ya mazungumzo hayo, Yesu alipanda chombo chake cha usafiri (wingu), na kwa spidi ya mwanga akatoweka machoni pangu.

Wakuu, kwa kuwa Bwana Yesu Kristo ameniahidi kunitembelea tena wiki ijayo, nitawaletea kitakachojiri kwenye mazungumzo kati yetu hapa hapa JamiiForums saa mbili kamili asubuhi siku ya jumamosi.​
Mwambie afungue account ya Jf akikutembelea tena.
 
Back
Top Bottom