Jana ulikuwa ni mkutano wa CCM uliovalishwa vazi la CHADEMA

Jana ulikuwa ni mkutano wa CCM uliovalishwa vazi la CHADEMA

Haya ni maoni yako. Tunayaheshimu..

Huu ni mtazamo wako Kwa muono wako. We respect that..

Lakini ulichoona na kukielewa, it's not necessarily iwe hivyo Kwa wengine..

Mimi nasema, umeyatazama kwa muono mdogo na mfupi sana...!

Kwani huo ndiyo ulikuwa mkutano wa kwanza na wa mwisho..?

Umefuatilia mkutano wa Musoma Leo J'pili trh 22/1/2023...?

What's the difference...?

To cut it short, ni kuwa, ktk hotuba bora na yenye akili ya Mh. Freeman Mbowe, basi ni ya Jana Kwa sababu aliweza Kwa umakini mkubwa kuepuka kuingia ktk mtego wa CCM na serikali..

Credit to him..

However, I respect your views and opinions..

🙏🏾🙏🏾🙏🏾
 
Nilishasemaga wewe ni mpumbavu. Long narrative halafu pumba tupu. Why should you always load JF valued server kwa upuuzi now and then?! Ni ukosefu wa maarifa na busara? Hunaga washauri au huna hata self conscious?

Unataka nikuajiri wewe ili uwe mshauri wangu?
 
Mtoa hoja jipiganie mwenyewe kwa hayo unayoyaamini uliyoyaandika humu, usijifanye shujaa kwa kujificha kwa ID fake hizi,Mh.Mbowe amekaa jela zaidi ya 150days bila ya kuwa na wapendwa wake, wewe ulifanya nini?maana muda wote ulikuwa na familia yako, Mh.Mbowe he done his bit sasa ni wakati wa ninyi middle class kujitokeza na kufanya mabadiliko ya kuisukuma nchi yetu mbele, it's craze mtu unatumia muda mwingi kumlaumu mtu mwingine eti akupiganie haki zako, uoga na uzuzu wa middle class ni cancer ndani ya nchi hii
Asante mkuu kwa kumuelewesha
 
Na, Robert Heriel

Jana agenda kuu ya mkutano ilikuwa kumshukuru na kumpongeza Rais, na ukimpongeza Rais tafsiri yake umeipongeza CCM. Ninaweza kusema Ulikuwa Mkutano wa CCM katika Vazi la CHADEMA. Na Hii ndio inaweza kutoa picha ni aina gani ya Siasa katika nchi hii tulizonazo.

Hakukuwa na sababu hata moja ya kumtaja Rais achilia mbali kumsifia kama kweli ule ungekuwa Mkutano wa CHADEMA.

Mwenyekiti Mbowe na viongozi wengine waliomsifia mwenyekiti wa CCM, Rais, Dr Samia Suluhu, wamefanya kosa kubwa kisiasa, kiushawishi.

Kimantiki, Kilichokuwa kinafanyika Jana ni kuushawishi umma wa watanzania waikubali CCM na kumuamini Rais Samia katika kuongoza Dola.

Sio ajabu Mbowe alizomewa, na walikuwa na haki ya kumzomea wafuasi wa Chadema. Jambo ambalo kama ingekuwa ni Mkutano wa CHADEMA lisingetokea.

Kama ungekuwa Mkutano wa Chadema, basi wazungumzaji wote waliopewa nafasi ya kusimama kuzungumza wangewashawishi watu kwa hoja namna CCM na Mwenyeketi wake walivyokosa sifa na vigezo vya kuongoza taifa hili.

Mkutano wa Jana Mwanza wa CCM, umejaribu kuonyesha watu wa nchi hii picha halisi ya wapinzani tulionao.

Hakuna anayetaka siasa za matusi, Mbowe kusema kuwa ati hatamtukana Mwenyekiti wa CCM, inashangaza, hakuna aliyemuambia amtukane. Wanachokataa ni Mbowe kuwa upande wa Samia, kuwa CCM. Tafsiri yake ni kuwa Wanachadema hawataki kuongozwa na MTU aliyeupande wa CCM.

Wanachadema wanaposema Mbowe analamba Asali, bila Shaka wanarejelea maana ya kuwa Mbowe yupo upande wa watawala wa CCM. Indirect way wanajaribu kusema Mbowe ni CCM. Na kama Mbowe yupo upande wa CCM automatically Mkutano wa Jana ulikuwa wa CCM.

Kulikuwa na hoja nyingi za msingi za kuzizungumzia,

1. Mbowe alipaswa aanzie alipoishia, kuwekwa ndani na baadaye kesi yake kufutwa. Ingawaje ni Jambo gumu 😀 lakini angeanzia hapo. Mfano Lissu yeye huanziaga pale alipopigwa Risasi. Wanasema ukitaka kumuua nyoka anzia miguuni.

2. Hoja ya Katiba Mpya, hii wameijadili lakini katika kiwango cha Chini.

3. Hoja ya Hali ngumu ya Maisha. Mkutano wa Jana ungepaswa utoe muhtasari wa jinsi serikali iliyopo madarakani ilivyoshindwa kuwapa unafuu Wananchi. Bei za bidhaa zipo juu. Wananchi wanataabika. Badala yake wanasifia CCM. Mpaka unajiuliza ulikuwa Mkutano wa chama cha upinzani kweli au Laa.

4. Hoja za Haki na Uhuru wa kujieleza.
Katika uwasilishaji wangejaribu kuwashawishi watu namna gani walivyofanikiwa kupigania hilo eneo. Hoja zao zijikite kuwa kila mafanikio na Maendeleo ya haki na Uhuru ndani ya nchi hii yamechangiwa Kwa kiasi kikubwa na Chadema.

Wangetakiwa wasema hata kuruhusiwa kwa mikutano ya kisiasa ni Kutokana na juhudi zao. Na watahakikisha kuwa Haki na Uhuru watavipigania Kwa gharama yoyote.

Hivi MTU akisema hivyo ametukana popote, amevunja sheria yoyote, jibu ni Hapana. Sasa unapomsifia hasimu wako kuwa bila yeye mikutano isingeruhusiwa unajaribu kuwaambia nini Wananchi?

Yaani ni sawasawa unaenda mtongoza Demu, alafu badala ujisifie wewe ATI unamsifia Mshindani wako. Unategemea Demu atakuonaje, si atakuona hamnazo!

5. Hoja ya UMOJA na USHIRIKIANO.
Katika Mkutano, Chadema ingeeleza kwa namna gani CCM ilivyoshindwa kuleta UMOJA na USHIRIKIANO ndani ya nchi. Kwa Hoja ZENYE mashiko na mifano dhahiri Wananchi wangeelewa.

Kisha iseme, Chadema Ipo kwaajili ya kuijenga nchi hii katika UMOJA na USHIRIKIANO. Sio kama CCM walivyofanya(unataja mifano).

Binafsi nimesikitishwa na chama ambacho ni kikubwa chenye miaka 30 Kwa Makusudi kabisa kikashindwa kuifanya siku ya Jana kuwa siku kweli ya uzinduzi. Badala yake wamezindua UCCM.

Kama tutaweka unafiki pembeni, nataka kusema, viongozi wa Chadema wamewaangusha wanachadema,
CCM inawazidije ujanja, Sasa si Bora hata msingefanya Mkutano kuliko kupoteza Muda na Pesa.

CCM wenzenu watapitia humohumo kwenye mapungufu yenu.

CCM ninavyowajua watakuja na kuwapaka Mavi mnuke,

Mimi ngoja nipumzike.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es
In fact mim naona ana haki ya kumshukuru na kumpongeza Samia kwasababu
1- Samia kapunguza vikwazo vya kidemokrasia hasa kuruhusu mikutano ya kisiasa
2- Samia yupo kinyume na CCM approximately 75% maana, karuhusu marekebisho ya katiba
 
Back
Top Bottom