Janet Yellen: Washington yatatokea madhara makubwa Marekani ikijitoa China

Baada ya kuona China hawezi kumwacha Mrusi, sasa Marekani kawa mpole kwa sababu timu ya BRICS ni tishio kwa Us kuliko silaha zote za nyuklia duniani.
Tishio kubwa baya ni kwa China kuikosa US ndio mana China vyovyote iwavyo anaibembeleza US hawezi fanya chochote, akiambiwa anaisaidia Urusi silaha anaruka mbingu na ardhi, US wakilianzisha Taiwan yeye anakuja chini
 
Hasara kubwa ipo China iwapo ataikosa US, ndio maana China anabembeleza, China akiambiwa anaisaidia silaha Urusi anaruka anasema yeye hajawai na hatawai anaogopa vikwazo vya US kama mdudu
 
Hasara kubwa ipo China iwapo ataikosa US, ndio maana China anabembeleza, China akiambiwa anaisaidia silaha Urusi anaruka anasema yeye hajawai na hatawai anaogopa vikwazo vya US kama mdudu
Wengi uku mnatoaa maoni yenu kishabiki sana bila kuelewa kilichoongelewa na vp uhalisia wa uchumi wa dunia ulivyo saivi kinachotokea saivi chinaa kilitokea marekani baadaa ya matajiri wengi kuamishia makampuni yao marekani.

Kwa kifupi tu hakuna kampuni yoyote ya ulaya au marekani itakayoweza kulikimbia soko LA China au kuamisha biashara zao China, purchasing power ya watu wa China inaongezeka kilaa uchwao pato LA mtu mmoja mmoja linakuwa kila siku japo bado kuna watu maskini wengi ila huwezi ifananishha China na India au Indonesia au Vietnam, bado China ndyo nchi inamatajiri wengi duniani baada ya marekani ata makampuni makubw ya ulayaa na marekani yataondoka bado China ina misuli mikubwa kwenye kubackup uchumi wake kinachogopesha zaidi makampuni makubwa ya ulaya na marekani ni kuwa siku yakiondoka China ndyo mwanzo wa kuaribu soko LA bidhaa zao sababu China anaweza toa bidhaa zilezile kwa bei nafuu na zenye ubora wa juu, misuli ya china saivi ni mikubwa sana kiuchumi ni ngumu sana kutunishiana misuli na marekani ila china alifanya ivyo kipindi cha trump marekani anajua silahaa yake iliyobaki ni chip siku china ana master hili basi ujue balaa litakuwa kubwa sana kwenye uchumi wa marekani shida uku ni wengi kumchukulia China kama kinchhi cha kawaida tu
 
Uchumi wa China uliitegemea sana Marekani na ulijengwa wakati wa Hu Jintao. Huyu jamaa yeye amekuja na zile fikra za kizamani za anti-US zinafofuatwa na Putin na ameanza kuharibu nchi yake. Usitukane wakunga wakati uzazi ungalipo.
Jiang Zemin na Hu Jintao walikuwa maraisi kipindi cha Clinton, Bush na Obama

Obama na Bush hawakuwa na sera mbovu kwa China wao walijua kuwa China na Marekani zinategemeana kibiashara

Trump na Biden ndio waliochochea kuzorotesha uhusiano mzuri uliokuwepo kati ya Marekani na China

Xi Jinping hana anti-USA policy sikuzote amekuwa akisisitiza win win cooperation kati ya mataifa hayo mawili
 
Tishio kubwa baya ni kwa China kuikosa US ndio mana China vyovyote iwavyo anaibembeleza US hawezi fanya chochote, akiambiwa anaisaidia Urusi silaha anaruka mbingu na ardhi, US wakilianzisha Taiwan yeye anakuja chini
Kwa yoyote mwenye knowledge ya biashara, atuambia China hawezi kusimama negative kwa US.

Soko la China na uwekezaji wa China ni US ndo amefanya awe hapo. US na allies wake wakimuwekea vikwazo China, athari zitakazojitokeza China ni kubwa zaidi kuliko hata hapo Russia.
 
Hasara kubwa ipo China iwapo ataikosa US, ndio maana China anabembeleza, China akiambiwa anaisaidia silaha Urusi anaruka anasema yeye hajawai na hatawai anaogopa vikwazo vya US kama mdudu
Unajua mshirika mkubwa wa kibiashara wa Marekani pale Asia ni China.

China na Marekani zinahitajiana sana kibiashara
 
Reactions: TPP
Marekani walijaribu Silaha ya mwisho kabisa ya ku control supply ya dola ili kuipandisha thamani lakini wapi…'chombo chazidi kwenda halijojo '
 
Kama unakiri economic development ya china kuongezeka (pato la mtu mmoja mmoja) maana yake ni kuwa makampuni yatalazimika uko mbeleni kutafuta mataifa ambayo pato lake bado lipo chini ili kurun biashara zao kwa gharama nafuu.
 
Unajua mshirika mkubwa wa kibiashara wa Marekani ni China.

China na Marekani zinahitajiana sana kibiashara
Hapana mkuu, kasome Balance of Trade baina ya hizo nchi mbili. Kwa US kuna negative kubwa, anachoimport kutoka china ni kama nusu na zaidi ya kile yeye anachoexport kwenda China.
 
Marekani walijaribu Silaha ya mwisho kabisa ya ku control supply ya dola ili kuipandisha thamani lakini wapi…'chombo chazidi kwenda halijojo '
Masuala y dola achana nayo mkuu maana yatafanya tuonekane Jf ni wendawazimu. Ishu ya kuishusha dola leo au kesho au ata wajukuu zao hawataweza kuona hilo.
 
Masuala y dola achana nayo mkuu maana yatafanya tuonekane Jf ni wendawazimu. Ishu ya kuishusha dola leo au kesho au ata wajukuu zao hawataweza kuona hilo.
umenielewa kwanza?

nimezungumzia uamuzi wa Treasury ya US ku control supply ya Dola kulinda thamani yake wewe unazungumiza kuishusha dola ? una elimu kidogo ya haya masuala au ndio kila jambo tunalijua kwa kuwa kuna google ?

kama huna elimu ya Devaluation na depreciation of currency huwezi kunielewa
 
China walikuwa na long plans za ukuzaji wa uchumi wao tangu zamani enzi za chairman Mao.

Aliyekuja kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kuufanya modern ni Deng Xiaoping

Nchi za West zimekuja baadaye kuwekeza China baada ya sera nzuri za China. Misingi ilishawekwa na China yenyewe na tayari walikuwa na viwanda na makampuni yao

China ilipojiunga WTO (World Trade Organisaztion) mwaka 2001 ndio makampuni ya West yalianza kuwekeza China. Na hii ni kwa sababu China ilipojiunga na WTO ilitakiwa kufanya mabadiliko katika sera za kibiashara sera hizo zikayavutia mataifa ya West kuwekeza China

Kwa nini China?
●Usalama
●Sera nzuri za uwekezaji kwenye rates na tax
●Labor force
●Soko la uhakika
●Miundombinu bora; barabara, umeme, usafiri, maji, bandari, reli n.k
●Skilled labor
●Uwepo wa teknolojia kwa R&D n.k

Hivyo vyote ni Wachina wenyewe walikuwa wameboresha

Kusema bila mataifa ya West, China ya leo isingekuwepo hapo ilipo ni uongo hizo ni propaganda tu.

Mataifa ya West wamekuta tayari gurudumu la maendeleo la China lipo mbioni tena kwa kasi ya juu
 
Hasara kubwa ipo China iwapo ataikosa US, ndio maana China anabembeleza, China akiambiwa anaisaidia silaha Urusi anaruka anasema yeye hajawai na hatawai anaogopa vikwazo vya US kama mdudu
Unapingana na US secretary of the treasury ?
 
Hapana mkuu, kasome Balance of Trade baina ya hizo nchi mbili. Kwa US kuna negative kubwa, anachoimport kutoka china ni kama nusu na zaidi ya kile yeye anachoexport kwenda China.
Mwaka jana Marekani aliingiza $150.4 billion kwa kuexport bidhaa China.

Na China ikawa taifa la tatu ambalo Marekani aliexport zaidi baada ya Canada na Mexico

Hata hao washirika wa karibu wa USA kama Ulaya na Japan hawajamfikishia hilo pato.

Ndio maana wawekezaji wengi wa Marekani hawajawahi kufurahishwa na sera za Marekani kwa China.
 
Reactions: TPP
Wawekezaji wa mwanzo China baada ya mabadiliko ya sera za kiuchumi na ufunguzi walitoka Hongkong, Macau, Taiwan
 
Uchumi wa China uliitegemea sana Marekani na ulijengwa wakati wa Hu Jintao. Huyu jamaa yeye amekuja na zile fikra za kizamani za anti-US zinafofuatwa na Putin na ameanza kuharibu nchi yake. Usitukane wakunga wakati uzazi ungalipo.
Ujenzi wa uchumi wa China umeanza toka wakati wa Chairman Mao mpaka sasa wakati wa General secretary Xi sio wakati wa General secretary Hu pekee.

Kuielewa safari ya uchumi na maendeleo ya China mpya yapaswa kujifunza harakati za mwanzo za ukombozi za CPC ,kuzaliwa kwa Jamhuri ya watu wa China, kipindi cha mwenyekiti Mao, Deng, Jiang, Hu na sasa katibu mkuu Xi Jinping
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…