Janet Yellen: Washington yatatokea madhara makubwa Marekani ikijitoa China

Janet Yellen: Washington yatatokea madhara makubwa Marekani ikijitoa China

Sikiliza hii kutokea ndani ya China. Walisema ustukane wakunga wakati uzazi ungalipo.

wazungu wakiondoka, wachina wanao uwezo kujenga viwanda vyao na market wanayo. wazungu watutishe sisi waafrica tu ila wachina hawawezi kuwatisha.
 
Kati ya Xi na akina Trump na Biden nani wamevuruga uhusiano mzuri uliokuwepo kati ya China na Marekani

Kumbuka sikuzote chini ya utawala wa Trump na Biden Marekani ndio wamekuwa wa kwanza kuyafungia au kuyawekea vikwazo makampuni ya China

Na hayo makampuni yalikuwepo kipindi cha akina Clinton, Bush na Obama hatukuona yakifungiwa.
 
wazungu wakiondoka, wachina wanao uwezo kujenga viwanda vyao na market wanayo. wazungu watutishe sisi waafrica tu ila wachina hawawezi kuwatisha.
Tayari walishajenga, wameshajenga na watajenga. West wamefika China tayari wana China based manufacturing industries nyingi tu.

Hata ukitembelea website za makampuni mengi ya China (China based companies& mfg industries) utakuta yalianzishwa zamani mengine tangu miaka ya 1950's hadi 1990's kabla hata West hawajaenda kuwekeza China

Ni vile tu China alikuwa amekomaa na soko la ndani wengi tulifahamu bidhaa chache za China walizokuwa wakiexport

Ndio maana wengine wanabeza kuwa uchumi wa China ni wa kutengeneza cherehani na baiskeli phoenix.

Wanaosema hivyo siwezi kuwabishia kwa sababu zilikuwa ni miongoni mwa bidhaa chache zilizovuka border ya China kutufikia wakati huo kabla hawajaanza exportation kwa kiasi kikubwa kama sasa
 
Clinton alikuwa na cheo gani pale WTO mkuu?
Baada ya WTO kuanzishwa kama replacement ya GATT, mwanzoni nchi zote zilitakiwa kukubaliwa na Congress ya Marekani kwanba zinafanya biashara ya haki. Clinton wakati anamalizia kipindi chake cha urais ndiye aliyesukuma Congress kuikubali China kuwa infanya biashara ya hakoi kwa kupytisha sheria U.S.–China Relations Act of 2000. Bila sheria hiyo, China isingeingia kwenye WTO wakati huo. Katika ya mambo ambayo Trump amekuwa anamlaumu sana Clinton ni hilo la kuikubali China kwenye WTO.
 
Kati ya Xi na akina Trump na Biden nani wamevuruga uhusiano mzuri uliokuwepo kati ya China na Marekani

Kumbuka sikuzote chini ya utawala wa Trump na Biden Marekani ndio wamekuwa wa kwanza kuyafungia au kuyawekea vikwazo makampuni ya China

Na hayo makampuni yalikuwepo kipindi cha akina Clinton, Bush na Obama hatukuona yakifungiwa.
Mbona anahangaika kuwaomba ma-CEO na viongozi wengine wa makampuni ya Marekani wasiondoke? Huyu mama siyo mmarekani wala hajawahi kuishi Marekani, na hiyo TV siyo ya marekani, nadhani iko India au Nepal. Kwa hiyo usiseme ni propaganda za Marekani.

Baada ya WTO kuanzishwa kama replacement ya GATT, mwanzoni nchi zote zilitakiwa kukubaliwa na Congress ya Marekani kwanba zinafanya biashara ya haki. Clinton wakati anamalizia kipindi chake cha urais ndiye aliyesukuma Congress kuikubali China kuwa infanya biashara ya hakoi kwa kupytisha sheria U.S.–China Relations Act of 2000. Bila sheria hiyo, China isingeingia kwenye WTO wakati huo. Katika ya mambo ambayo Trump amekuwa anamlaumu sana Clinton ni hilo la kuikubali China kwenye WTO.
Kuingia kwa China kwenye WTO kumeleta mapinduzi katika suala zima la global supply chains. USA na China zimefaidika na hilo ijapokuwa viongozi wa Marekani kama Trump na Biden wameanza kuharibu
 
Hata kabla ya Hu Jintao uchumi wa China ulikuwa unakua.

Iko hivi China mwaka 2001 kipindi raisi akiwa Jiang Zemin ilijiunga na WTO

Moja ya manufaa makubwa China alipata baada ya kujiunga na shirika hilo la biashara duniani WTO ni kuanza kuexport kwa kiasi kikubwa bidhaa zake duniani.

Na kuanzia hapo uchumi wa China ulianza kukua kwa kasi hadi kufikia 10% na point kadhaa

Mwaka 2007 ikaizidi Ujerumani ikawa ya 3 kiuchumi duniani mwaka 2010 ikaipita Japan ikawa ya 2 duniani

Hoja iko hapa: Hu Jintao aliingia madarakani mwaka 2003 kwa hiyo alikuta tayari mtangulizi wake Jiang Zemin ameifanya China kuwa member wa WTO tangu mwaka 2001

Kwa hiyo Hu Jintao akaanza kuvuna matunda yaliyohasisiwa na mtangulizi wake Jiang Zemin.

Ndio maana mimi na TPP sikuzote tunasema taifa la China wana dira na sera ya taifa ambayo kiongozi yoyote wa CPC anaifuta lengo kuukuza uchumi wa China

Comrades wote kuanzia Mao mpaka kufikia Xi lengo lao ni moja kuikuza China
Umesema vyema
 
Nadhani wewe ni mchina wa CCP anyeishi bongo kwa kutetea mambo ambayo hayakubaliani na ukweli.

Uchumi wa China imeanza kukuwa kwa kasi wakati wa Hu Jintao miaka ya 2000. Kabla ya hapo kulikuwa na maandaliazi ya "kujivua gamba" yaliyofanywa na watangulizi wake ambayo ndugu yenu anaaza kuyarudia magamba tena.
Unachozungumzia wewe ni ukuaji wa kasi sio ujenzi wa mwanzo wa uchumi wa Jamhuri ya watu wa China hapo ndipo tatizo lilipo baina yetu.

Pia ukuaji wa kasi wa uchumi wa China unao zungumzia wakati wa Hu Jintao ni matokeo ya jitihada za watangulizi wa mwanzo kabla ya wakati wake
 
Mbona anahangaika kuwaomba ma-CEO na viongozi wengine wa makampuni ya Marekani wasiondoke? Huyu mama siyo mmarekani wala hajawahi kuishi Marekani, na hiyo TV siyo ya marekani, nadhani iko India au Nepal. Kwa hiyo usiseme ni propaganda za Marekani.

Mzee hii habari ya youtube ni ya Wahindi. Always kwenye social media Wahindi wamekuwa wakitangaza habari za China ina negative way.

Hakuna mahali paliposemwa kuwa Xi amemsihi Bill Gate asiondoe uwekezaji wake China

Hao wafanyabishara wakubwa wanajua manufaa ya kuwekeza China.

Hata Elon Musk ziara yake ya mwisho mwezi jana nchini China alisema wazi kuwa China ni muhimu katika uchumi wa dunia na ukuaji wa Tesla
 
Unachozungumzia wewe ni ukuaji wa kasi sio ujenzi wa mwanzo wa uchumi wa Jamhuri ya watu wa China hapo ndipo tatizo lilipo baina yetu.

Pia ukuaji wa kasi wa uchumi wa China unao zungumzia wakati wa Hu Jintao ni matokeo ya jitihada za watangulizi wa mwanzo kabla ya wakati wake
Hata uchumi wa Tanzania unakua tangu tumepata uhuru. Kila mwaka tuna positive GDP growth lakini hatujaweza kuwa kama China. Hata wakati wa Mao uchumi wa china ulikuwa unakua
 
Hata uchumi wa Tanzania unakua tangu tumepata uhuru. Kila mwaka tuna positive GDP growth lakini hatujaweza kuwa kama China. Hata wakati wa Mao uchumi wa china ulikuwa unakua
Misingi ya uchumi wa China ilijengwa katika nini ? Na kipindi gani ujenzi huo ulianza ? Ukifahamu hii historia fupi utakuwa na uelewa kwa kina kuhusu uchumi wa China
 
Mzee hii habari ya youtube ni ya Wahindi. Always kwenye social media Wahindi wmekuwa wakitangaza habari za China ina negative way.

Hakuna mahali paliposemwa kuwa Xi amemsihi Bill Gate asiondoe uwekezaji wake China

Hao wafanyabishara wakubwa wanajua manufaa ya kuwekeza China.

Hata Elon Musk ziara yake ya mwisho China alisema wazi kuwa China ni muhimu katika uchumi wa dunia.
Nimeweka video hizo kwa vila ninapatika kirahisi, lakini wiki iliyopita Rais wa China ameaishaitisha mikutano zaid ya mitatu na viongozi wa biashara kadhaa kutoka Marekani. Ni katika juhudi zake za kujisafisha: Amekutana na Musk, Dimon, Cook na wengineo.

1686951427809.png
 
Angalia Micron wanavyotapa baada ya kupigwa ban na China wametambua umuhimu wa China kwenye biashara ya chip

Leo wamtengaza hivi:
US memory chipmaker Micron Technology said on Friday that it will invest 4.3 billion yuan ($602.77 million) in its chip packaging and testing factory in Xi'an, Shaanxi Province

Cc; Kichuguu Kizzy Wizzy
 
View attachment 2660040
Umeona tofauti ya habari hii na ile ya Wahindi wa youtube

Ndio maana nilisema sikuzote China ametaka kuwe na win win cooperation kati ya China na Marekani

Xi hajawahi kuwa na anti-USA policy. Ni vile Marekani wakiichokoza China nao Wachina huwa wanafanya trade coercion kama walivyofanya kwa Micron na sasa hivi wenyewe wamenywea
 
Angalia Micron wanavyotapa baada ya kupigwa ban na China wametambua umuhimu wa China kwenye biashara ya chip

Leo wamtengaza hivi:
US memory chipmaker Micron Technology said on Friday that it will invest 4.3 billion yuan ($602.77 million) in its chip packaging and testing factory in Xi'an, Shaanxi Province

Cc; Kichuguu Kizzy Wizzy
Micron ni kampuni ndogo sana mzee wangu. Walikuwa wanatengezea hard disk lakini wamepand kidogo siku hizi wanatengezea USB thumb drives na flash memory chips tu.
 
Nimeweka video hizo kwa vila ninapatika kirahisi, lakini wiki iliyopita Rais wa China ameaishaitisha mikutano zaid ya mitatu na viongozi wa biashara kadhaa kutoka Marekani. Ni katika juhudi zake za kujisafisha: Amekutana na Musk, Dimon, Cook na wengineo.

View attachment 2660040
Ni wapi Musk alikutan na Xi Jinping. Musk alikutana na waziri

Kwa taarifa yako sasa: ElonMusk made a trip to China and Tesla's stock soared continuously, helping him regain his position as the world's richest man. BillGates arrived in Beijing, and Microsoft's stock price rose in response, with its market value hitting an all-time high
 
Back
Top Bottom