Janga jingine lamkuta Emmanuel Mbasha, inadaiwa kaficha habari kuhusu mfanyakazi wake aliyejinyonga

ruanganyi

Senior Member
Joined
Aug 19, 2014
Posts
115
Reaction score
34


Majanga yanazidi kumuandama aliyekua mme wa muimbaji maarufu Frola Mbasha, akiwa bado ana kesi mahakamani akidaiwa kumbaka ndugu yake hili ndio janga jingine lilimkuta Emmanuel Mbasha. Janga hilo ni la kufariki kwa mfanyakazi wake wa ndani ambae alijinyonga ijumaa iliyopita.


Inadaiwa kua Emmanuel na mfanyakazi huyo walikua wakiishi wawili tu ndani ya nyumba ya Emmanuel, lakini kitu cha kushangaza zaidi ni pale mfanyakazi huyo alipojinyonga.

Inavyosemekana Emmanuel hakutoa taarifa kwa majirani kuhusu tukio hilo badala yake alitoa taarifa polisi na kisha kuusafirisha mwili wa marehemu kwa siri sana kwenda kumzika Singida.


 
maombii ya gwajima nanafanyaa kazi,kwanini alikuwa anamsingizia mpakwa mafuta wa bwana mtu wa ufufuo na uzima
 
Hii habari imekaa kimajungu na ushambenga.Sioni tatizo ushasema alitoa taarifa polisi.

Majungu si mtaji utakaofanya utajirike
 
Waswahili bwana. Yaani walitaka waambiwe wakae walio wapike uji wapige soga za kwenye misiba. Mchango sifuri. Watanzania bwana.Mumwache apumue jamaa. Mi nilizani hakutoa taarifa kumbe hakutoa taarifa kwa majirani. Hao majirani wangekuwa wema jamaa asingeingia kwenye crisis ya ndoa na mkewe
 
Sema tu amepatwa na janga la kufiwa na mfanyakazi wake wa ndani aliyejinyonga na nampa pole sana kwa hilo,mengine sijaelewa ulitaka kufikisha ujumbe gani kwa umma....!
 

udaku?
 
sasa majirani waambiwe kwani wao ni nani?wa muhimu ni polisi na huko alishapeleka taarifa....wabongo wapumbavu sana
 
wabongo wanapenda kufatilia maisha ya watu,wameokosa umbeya walotaka kuufanya msibani sasa roho zinawauma.
 
Kwani ile mechi ya CHELSIE NA MAN matokeo yalikuwa ngapi ngapi vile???

Pia na ile ya YANGA NA SIMBA.......?
 
majirani wao ndo polisi?au ndo waliomleta kutoka singida?au ndo wazazi?
uswahili tu unawasumbua hapo mtaani maana kimewauma wameshindwa pa kuanza kuleta umbea na picha za kwnye mitandao
 
ulitaka akodi watu muende kulia hapooo! jamani tupunguze uswahili hapa hata janga bado sijaliona. kuna gazeti siku za nyuma kidogo kichwa cha khabari kinasema WAZIRI ANASWA KIBAO watu wakalinunua wasome waziri gani huyo! kumbe ni jamaa anaitwa waziri ali mkazi wa vingunguti aliparakashwa makofi katika ugomvi.
sasa heading hizi jamani zinatia shaka.
 
Gwajima anatafuta kujisafisha hapa kwa uzinzi aliomfanyia mke wa Mbasha. Jeshi la Daudi liko kazini,,, by the way nendeni mkazindue ile chopa ya kubebea Sembe
 
Si alitoa Taarifa polisi na kupeleka mwili kwao? Ulitaka akutangazie na wewe? Watu wote wanao jinyonga una taarifa zao?

Hahahaaa si yakucheka lakini kwa comment yako nimejikuta nacheka, mleta mada atakuwa msajili wa vizazi na vifo!
 
Majanga yanazidi kumuandama aliyekua
mme wa muimbaji maarufu Frola Mbasha,
akiwa bado ana kesi mahakamani akidaiwa
kumbaka ndugu yake hili ndio janga jingine
lilimkuta Emmanuel Mbasha. Janga hilo ni la
kufariki kwa mfanyakazi wake wa ndani
ambae alijinyonga ijumaa iliyopita.
Inadaiwa kua Emmanuel na mfanyakazi huyo
walikua wakiishi wawili tu ndani ya nyumba
ya Emmanuel, lakini kitu cha kushangaza
zaidi ni pale mfanyakazi huyo alipojinyonga.
Inavyosemekana Emmanuel hakutoa taarifa
kwa majirani kuhusu tukio hilo badala yake
alitoa taarifa polisi na kisha kuusafirisha
mwili wa marehemu kwa siri sana kwenda
kumzika Singida.
Tumepata ujumbe kutoka kwa mmoja wa
majirani wa Emmanuel Mbasha ambae
hakutaka jina lake litajwe, ujumbe huo
ulisema ” Kuna kijana wa kazi toka Singida
alikuwa anaishi na Emmanuel Mbasha,
amejinyonga na kuacha ujumbe kuwa kwa
yaliyomkuta ameamua bora ajinyonge.
Walikuwa wanaishi na Mbasha tu huko ndani
na baada ya kujinyonga Mbasha amefanya
siri kubwa mno hawakuweka hata msiba.
Kijana alijinyonga Ijumaa na ndugu
wakatafutwa wakaenda kureport polisi kwa
ajili ya mazishi na wamemsafirisha kwenda
kuzika Singinda. Mbasha hakuta majirani
tujue. Mnaweza mtafuta kwa maelezo zaidi
maana nikiandika hapa yeye ndo mwenye
ukweli alimfanyia nini kijana wa watu. ”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…