Majanga yanazidi kumuandama aliyekua
mme wa muimbaji maarufu Frola Mbasha,
akiwa bado ana kesi mahakamani akidaiwa
kumbaka ndugu yake hili ndio janga jingine
lilimkuta Emmanuel Mbasha. Janga hilo ni la
kufariki kwa mfanyakazi wake wa ndani
ambae alijinyonga ijumaa iliyopita.
Inadaiwa kua Emmanuel na mfanyakazi huyo
walikua wakiishi wawili tu ndani ya nyumba
ya Emmanuel, lakini kitu cha kushangaza
zaidi ni pale mfanyakazi huyo alipojinyonga.
Inavyosemekana Emmanuel hakutoa taarifa
kwa majirani kuhusu tukio hilo badala yake
alitoa taarifa polisi na kisha kuusafirisha
mwili wa marehemu kwa siri sana kwenda
kumzika Singida.
Tumepata ujumbe kutoka kwa mmoja wa
majirani wa Emmanuel Mbasha ambae
hakutaka jina lake litajwe, ujumbe huo
ulisema Kuna kijana wa kazi toka Singida
alikuwa anaishi na Emmanuel Mbasha,
amejinyonga na kuacha ujumbe kuwa kwa
yaliyomkuta ameamua bora ajinyonge.
Walikuwa wanaishi na Mbasha tu huko ndani
na baada ya kujinyonga Mbasha amefanya
siri kubwa mno hawakuweka hata msiba.
Kijana alijinyonga Ijumaa na ndugu
wakatafutwa wakaenda kureport polisi kwa
ajili ya mazishi na wamemsafirisha kwenda
kuzika Singinda. Mbasha hakuta majirani
tujue. Mnaweza mtafuta kwa maelezo zaidi
maana nikiandika hapa yeye ndo mwenye
ukweli alimfanyia nini kijana wa watu.