Hakika janga la corona limewazamisha sana wapinzani na hoja yao ya kulazimisha lockdown, kulazimisha habari za uongo kwamba hali ni mbaya saana wakati watanzania wao wanadunda na maisha kama kawa.
Lockdown waliyoishabibia sana;
1. Imekosa kabisa uhalisia wa utekelezaji kwa nchi kama zetu. Madhara ya kukataa lockdown yameeleweka na yanaimbwa na wananchi wa kawaida kabisa.
2. Hata nchi za Ulaya/US zimekuja kuacha a na lockdown.
3. Faida zilizokuwa zinapigiwa upatu zimekuja kuonekana si halisia. Badala yake kuna consensus ya kwamba lockdown ina madhara na haifai kufuatwa
4. Mifano ya wananchi kuigomea lockdown iko wazi nchi nyingi wananchi wa kawaida wanaoandamana ikiwemo majirani zetu Kenya, Zambia, Afrika ya kusini.
Hata hivyo nawasifu viongozi wa upinzani kwa mshipa wa ung'ang'anizi! Wamejua lockdown haikubaliki na watanzania, haina faida za kiafya kama wanavyosema, kuna madhara makubwa zaidi ya lockdown, siyo mbinu inayopendwa tena! Lakini bado wameshindwa kukiri!