Janga la COVID-19: Naipongeza Serikali kwa kukataa kuiga baadhi ya mbinu za ’Nchi za Magharibi’

Mkuu MsemajiUkweli , ONLY TIME WILL TELL.
Mkuu jmushi1;
Ni kweli time is the answer lakini pia mazingira ni sehemu muhimu sana katika kufikia maamuzi.

Nimesema, njia aliyotumia Rais Magufuli sio kwamba ndio sahihi katika kupambana na janga la COVID-19 bali njia aliyoitumia inaendana na mazingira ya Tanzania kiuchumi na kijamii.

Tunaona kwa sasa kinachoendelea katika nchi za Kenya, Uganda na Rwanda baada ya kutumia njia kama iliyotumiwa na nchi za Magharibi. Polisi wameanza kuwapiga risasi wananchi ambao wameamua kukaidi amri za kujifungia ndani ya nyumba zao. Baada ya wiki moja, hali itakuwa mbaya zaidi.

Ni mtu mjinga ambaye atajifungia ndani ya nyumba yake wakati anakufa polepole kwa kukosa chakula wakati akitoka nje anaweza kupata chakula.
 
Katika watu wasiomuunga Magufuli kwa mambo yake mengi, mimi ni mmojawapo, ila kwa hili na mengine machache sana namuunga mkono. Sina lolote la kumpinga au kumkosoa kwenye uamuzi wake huu.
Alert
Akaunti imedukuliwa
 
Ni kwa sababu Corona aijawa tatizo Tanzania na tuombe hali iendelee kubaki ivyo.

Wanaotaka watu kubaki majumbani sio kwamba wana hela za mchezo za kugawa isipokuwa hiyo ndio njia pekee ya kupunguza kasi ya ukuaji vinginevyo ingekuwa ni balaa.
Mkuu;
Mawazo yako yanaongelea nadharia!

Yaani unawaamuru watu wabaki majumbani wakati hawana chakula wakati chakula chao wanakipata wakitoka nje! Hizi sio akili matope?

Kwenye mada yangu nimesema mazingira ya kiuchumi na kijamii nchini hayaruhusu kutumia mbinu kama zilizotumiwa na nchi za magharibi.

Kumbuka waliosema, ''think globally but act locally'' hawakufanya makosa!
 


Kupanga ni kuchagua acha shughuli ziendelee kama kawaida maambukizi yapite kwa haraka katika kipindi icho uelewe kabisa huduma zako za afya aziteweza mudu wimbi la wagonjwa kwa ivyo a lot of people will die in the process.

Au ufanye control ugonjwa upite polepole uweze kuokoa maisha ya wengi.

Hizo ndio option zilizopo sasa kama kuna watu hili waweze pata mlo lazima watoke ukubali pia na option ya kwanza wacha wengi wafe ugonjwa upite haraka.
 
Mkuu njia zinazotumiwa na nchi za magharibi, ni maelekezo ya wataalam. Kwa mfano ingekuwa ni amri ya Trump, watu wangeingia kitaa mapema sana. Hata ile kusema kuwa anataka mambo yalegezwe kuanzia wakati wa Easter, imewashangaza wataalam na ikapelekea Dr Fauci kuweka mambo sawa na kusema Hiyo ni “aspiration date”, yani tarehe ambayo ni matamanio ya Trump, lakini uhalisia ndiyo utakaotoa uamuzi.

Kwahiyo siyo sahihi hata kidogo kuita maelekezo ya wataalam kuwa ni mbinu za nchi za magharibi.

Toa sababu nyingine, lakini hii ni upotoshaji.
 
MsemaUkweli umesema kweli tupu. Total lockdown pekee kwa Tanzania itauwa watu wengi sana kuliko hiyo corona, na kwa muda mrefu zaidi. Asilimia takribani 80% ya watanzania ni wakulima wadogo wadogo. Na asilimia 20 iliyobaki chakula chao kinatoka kwa hawa wakulima wadogowadogo. Sasa hivi ni kipindi cha masika, kipindi cha kulima. Ukiwa lock down maana yake mwaka huu watanzania wote million 60 hawatakuwa na chakula cho chote. Mifugo yote itakufa na kadhalika. Serikali itawezaje kuwalisha watanzania wote, kwa kipato kipi?

Total lockdown itafanya shughuli zote za kiuchumi ziwe sifuri kwa kipindi chote cha mlipuko huu wa corona ambao hatujui utachukua miezi au miaka mingapi. Maana yake mapato ya serikali (TRA) yatakuwa zero. Hivyo hakutakuwa na mishahara wala kitu cho chote kwa watumishi wa umma wote na hata wale ambao si watumishi wa umma. Yaani hata majeshi yetu ambayo nayo yatakuwa kwenye lock down except a few na wahudumu wa afya watakaokuwa wakitibu wagonjwa wa corona wanaweza nao wakakosa mishahara maana TRA watakuwa hawakusanyi cha kutosha na akiba yetu ndogo haitatosha. Wengi wetu ambao kipato chetu kwa siku ni hand to mouth tutakufa kwa njaa ndani ya siku mbili au tatu tu za total lock down, kitu ambacho hakuna atakayekubali, wote watatoka nje na polisi haitaweza kuwamudu.

Tuendelee kumuomba Mungu atuvushe kwenye hili janga. Tulishavuka na tunaendelea kuvuka majanga mengi tu yaliyoua watu wengi zaidi kuliko hiyi corona hususani kipindupindu, surua, kifua kikuu, ukimwi, utapiamlo, mafuriko, ajali za barabarani nk bila kuwekwa total lockdown. Hata hili tutalivuka bila total lockdown. Hakuna haja ya kuwa na hofu (panic). Huko China ambako population ni watu zaidi ya billion moja ugonjwa huu umeua watu wasiozidi elfu nne tu sawa na asilimia 0.0000001 of the population! Tusiogope, hii changamoto nayo itapita. Hofu na uwoga hupunguza kinga (immunity) ya mwili. Usiiruhusu. Ibada za makanisani na misikitini ni maeneo madhubuti ya kuwaondolea binadamu hofu na uwoga wa dunia hii na kuukabidhi kwa Mola, hivyo ku boost immunity ya binadamu.
 
Mkuu umeasi ccm au umeamua kuidharirisha nchi yetu? A Dona county,nchi tajiri wananchi wake wanawezaje kukosa maji Safi ya kunywa? Je hili bandiko lako na yule aliyepiga picha ya mahandaki kwenye Barbara za ngorongoro tofauti ni Nini?

..lingine ambalo watu wamesahau ni kwamba bwana mkubwa anapenda sana cameras na mikusanyiko. Sasa mtu wa aina hiyo siyo rahisi ahimize isolation hata kama jambo hilo lingekuwa linawezekana.
 
Pamoja na hayo, tungejifungia ndani ndo tungekufa zaidi kuliko hiyo covd-19.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu;
Maoni yako yamebeba msingi wa mada yangu.

Kuna baadhi ya watu nashindwa kuelewa kama wanajua mantiki ya maoni yako au wanajifanya hawajui.

Nasikia huko India na Kenya, wananchi wameanza kupambana na polisi kutokana na amri ya kuwataka wabakie majumbani.

Kuwakamata na kuwaweza ndani inakuwa ni sehemu ya kuendeleza dhana ya watu wengi kukusanyika kwa sababu watawarundika ndani ya gereza lakini kikubwa zaidi, kama kuna baadhi ya waliokamatwa watakuwa na virusi vya corona basi watawaambukiza wafungwa wengine gerezani.
 
Hakuna aliyesema mchezo umeisha bali tunachosema ni mbinu za mchezo kulingana na mazingira!
Mbinu za mchezo zinatokana na tabia za Corona anavyosambaa na uwezo wa huduma za afya kuhimili wagonjwa kwa wakati mmoja (kama lengo ni kuokoa maisha) and not so much kuhusu tabia zako za mazoea ya kuishi.

Ndio maana watu wamejipanga kudhibiti Corona sio kulinda namna walivyozoea kuishi kila siku; it helps kwa sababu wana uwezo wa kukabiliana na changamoto za uchumi (walau watu wapate basic needs katika kipindi icho).

Bahati mbaya sisi mazingira yetu kwenye kukabiliana na hilo janga linazua tatizo lingine; ambapo kwa majibu mepesi ni kukubali option 1 ipite tu liwalo na liwe kwa sababu lockdown also brings other social costs.
 

Huu uzi pamoja na ulivyojitahidi kuupamba nasikitika kukutaarifu ni moja ya mifano hai TWAWEZA wanapaswa kuiambatanisha kuhusiana kale ka 'trait' ka watanzania kwenye maamuzi yao yanayowagharimu vilivyo bila kutambua.

Tunayo matatizo ya elimu na bahati mbaya watawala wetu ambao walipaswa kuwa viongozi wetu wanayatumia to our detriment.

Cases tatu za lockdown zinazotuzunguka:

1. Rwanda: Wananchi wame elimishwa sana kuhusu huu ugonjwa. "Inafahamika pasi na shaka kwa watu wote kuwa huu ugonjwa ni wetu". Yaani wao kama jamii.

Kwamba jamii yote iko salama kama hakuna mtu hata mmoja anao. Vinginevyo si tajiri wala masikini bali wote ni marehemu watarajiwa.

Serikali za mitaa zina orodha ya familia zinazohitaji msaada wa chakula. Kuna mfuko unaochangiwa na makampuni na watu binafsi kusaidia familia hizo. Serikali inakamilisha kilicho pungua.

Tozo mbalimbali zikiwamo kodi za serikali, marejesho ya mikopo bank, malipo ya kodi za mapango, gharama za miamala simu nk zimeahirishwa au kuondolewa kabisa kuwapa watu ahueni.

Rwanda wako kwenye lockdown ya siku 14 tayari wanabakiwa na takribani siku 7 hakuna aliykufa na njaa wala kukosa chakula.

Malo ya mizigo yanaingia na kutoka Rwanda si kuwa total lockdown maana yake kila kitu kimesimama na watu wamefungiwa vyumbani. Acheni kupotosha.

2. Kenya Mombasa wanataka total lockdown. Hawafurahishwi na hii partial ambayo kimsingi ni curfew iliyopo in place sasa hivi. Tayari Mombasa wamesha mobilize pesa kuhakikisha hakuna familia itaathirika maamuzi ya total lockdown yatakapotoka.

Pana nafuu nyingi serikali imetoa. Mishahara ya wakuu wakiwamo wabunge imekatwa.

Wananchi wanaelewa na wako pamoja katika hili.

Nafuu nyingi kwenye tozo mbalimbali zimewekwa kama ilivyo Rwanda. Hawa ni muda mdogo tu bado wanaenda total lockdown kama Rwanda.

3. Uganda huku kuna jenerali mwenye mkono wa chuma (haambiliki labda naye wanamwita jiwe). Ushirikishaji umma kwake ni mdogo. Yeye badala ya kwenda total lockdown anafanya ubaguzi wa wazi na bila kujali.

Mifano ni mingi: Kwa nini bodaboda, mabasi nk wasimame hali masoko yako wazi? Hana mipango yoyote ya kuwafidia wananchi, wengine wana mikopo bank, kula yao ni kazi ya siku nk. Hapa ni chaos.

Kwetu sisi tumebakia kudanganyana muda unakwenda. Total lockdown ni inevitable. Kama alivyosema Ramaphosa ni suala la muda tu. Jinsi muda unavyokwenda itaja tugharimu zaidi.

Kina Msigwa, kina Mashinji na wenzao Ilikuwa wafungwe. Ndani ya siku 3 zilichangwa 350,000,000/= na wananchi. Kwa nini kwenye jambo serious hili mnaliwekea siasa uchwara namna hii. Kwa nini isiwezekane kuchangisha kwa watakakuwa na upungufu wa chakula kama serikali haitaona umuhimu huo.

Hata hivyo kwa kipindi hiki cha dharura hii ya kuishi au kufa serikali inapaswa kusimamisha miradi yote mikubwa. Haya mambo ya uchaguzi mkuu si priority tena. Kuna ruzuku za vyama vya siasa. Tuweke raslimali zote tutoke hapa tukiwa salama kwanza mengine baadaye.

Taabu iko wapi? Hiyo njaa mnayokaa mnaongea iko wapi?

Pathetic!

TWAWEZA ushahidi mwingine katika ule utafiti wenu pendwa ni huu uzi wa huyu bwana msemajiukweli.
 

Mkuu nikiongezea kwa mengi niliyoyaandika, hali iko hivi:

Athari za #COVID19: Italia yaendelea kurekodi mamia ya vifo - JamiiForums

Magufuli hajaenda vitani na jeshi alilo nalo huyu kaamua kumshitakia Mungu.

"Ndani ya Yesu hakuna Corona". Mwisho wa kumnukuu.
 
Ninakubaliana na angalizo lako!

Kwanza nchi zetu zina njia za panya nyingi tu ambapo haiwezekani asilimia 100 kufunga mipaka na kufanikiwa asilimia 100.

Tanzania tunapakana na nchi zaidi ya nane. Huo ulinzi wa mipaka sidhani kama utawezekana!
 
Ninakubaliana na angalizo lako!

Kwanza nchi zetu zina njia za panya nyingi tu ambapo haiwezekani asilimia 100 kufunga mipaka na kufanikiwa asilimia 100.

Tanzania tunapakana na nchi zaidi ya nane. Huo ulinzi wa mipaka sidhani kama utawezekana!

Rwanda au South Africa wanaweza je? Uganda, Kenya nao je?

China wamefanikiwa kupitia lockdown. Korea kusini nao hivyo hivyo. Kwani siku nyingi mafanikio ya Rwanda na South Africa katika mwezi 1 mbivu na mbichi zitakuwa nje.

Mtatafuta hata kwa tochi sababu za kuhalalisha mipaka kuendekeza kuwa wazi.

Ila fahamuni kitakapo nuka sawa sawa ndipo itajulikana kuwa kufunga mipaka na kwenda lockdown kumbe ilikuwa inawezekana.

Kwa hapo haitakuwa for free itabidi tukumbushane pia kwa nini kwa muda wote tulipuuzia.

Hizi kelele za sasa ngoma bado mbichi, kila mtu ana mdomo. Hata Italy, Spain na USA ilikuwa hivi hivi wakati ngoma ilikuwa bado mbichi. Leo wanajuta kwa kuchelewa mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…