Janga la COVID-19: Naipongeza Serikali kwa kukataa kuiga baadhi ya mbinu za ’Nchi za Magharibi’

Kumbe wewe haujui hata maana ya" lockdown ".
sasa ukiacha maduka ya chakula WAZI atanunua nani wakati umekata watu wasitoke NJE?
Ndo maana nawaambia hyo ishu ni ngumu.
Angalia wahindi wanavyotiana bakora
Hakuna nchi iliyozuia uuzwaji wa chakula.View attachment 1401453

Mwisho wa hatua za huyo bwana zipo wazi. Ndio sawa na ubishi wenu kama mnadhani kutakuwa na outcome nyingine serikari isipoumiza kichwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waangalie kwanza India wanavyotiana bakora watu wanalia kama watoto..
Leo hii tukisema tusifanye kazi hata uchumi wa nchi unashuka na mapato hamna.
Hata wale wanategemea mwisho wa mwezi wa naweza wasilipwe..
Alafu unaweza ukawa na hela lakini maduka yamefungwa,magenge yamefungwa utanunua nini?.
Pata picha pale kariakoo pafungwe?.
BORA CORONA KULIKO NJAA.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana uganda watu wawili wamepigwa risasi eti kisa kukataa kukaa ndani , ongezea na viboko vya india + kenya mambo sio mambo watu wanapigwa balaa.

Kwakweli bora mtu apate corona kuliko mateso ya ajabu hivyo.. sijawahi kuona watu wasiokuwa civillized na wasio tumia common sense kama polisi na wanajeshi.. hawa jamaa hamnazo kabisa.
 
Ndio maana na mimi nikasema tatizo letu ni fatalism thinking.

Kwa wenzetu wanapopata majanga ndio akili zao zinapofanya kazi zaidi kutafuta solution; kwenye muda mfupi wameweza kuja na cheap hand held technology inayoweza pima Corona ndani ya nusu saa na kutoa majibu, kuongeza hospital treatment capacity wameweza modify mashine moja ya ventilator kuwa na uwezo wa kuhudumia watu wawili kwa wakati, etc wakati researches zingine luluki za kupambana na changamoto zinaendelea.

Sisi tatizo letu waafrica atupendi kuumiza vichwa tunapenda simple solutions tena ambazo extreme; kusema watu waendelee na maisha kama kawaida ni sawa kukubali kushindwa vita kabla aijaanza.

Let me assure you ata kwa mabeberu compliance is not voluntary ukikamatwa unadhurura bila ya sababu maalum kuna fines, mkikutwa mpo kikundi fine na ukikutwa umetoka una dalili za mafua wanafikiria kukupeleka jela that is how serious they are kwenye kuakikisha wanaidhibiti Corona. Na hawa watu atuwafikii kwa ubora wa hospitali, vifaa tiba wala financial resources.

Chukulia waziri mkuu wa UK, waziri wa afya na Chief medical officer; watu ambao unategemea ofisi zao zitakuwa disinfected regularly, wao wenyewe wana elimu ya kutosha kuweza kuchukua hatua za kujikinga na ndio leaders kwenye kupambana na Corona lakini wamepata maambukizi; sembuse mama ntilie na wateja wake kwenye barabara zetu.

Ni hivi hii Corona tuisikie tu kwa wenzetu muulize mtu anaeishi U.K akueleze usione PM na hao vigogo waliobainika wamepimwa ukadhani kila mtu ana hiyo nafasi ya kupata kipimo; malaki ya watu wanaugulia mafua ndani na kujitibu wenyewe bila ya kuelewa kama wana Corona au mafua ya kawaida.

Uruhusiwi kwenda kwa GP, Pharmacy wala hospitali kama una mafua; umtafute mtu wa kwenda kukununilia dawa unazozijua ujitibie. Kupiga simu hospitali mpaka uwe na homa kali na kikoozi kianze.

Kwa ivyo hao unaoona wamepimwa kama Prince Charles, PM na wengine ni kwa sababu ya kuwa na nafasi. Wenzetu wapo serious na hii control kwa sababu wanajua nini kitafuata wakisema life has to go on as normal. Sasa sisi ambao atufanyi research zozote tunadhani lockdown ni swala la option well it can be but a very costly one.
 
Kumbe wewe haujui hata maana ya" lockdown ".
sasa ukiacha maduka ya chakula WAZI atanunua nani wakati umekata watu wasitoke NJE?
Ndo maana nawaambia hyo ishu ni ngumu.
Angalia wahindi wanavyotiana bakora

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye lockdown essential services zinafanya kazi kama kawaida na kuna utaratibu wa kutoka, kupeana gap ya six feet, etc. Kila nchi inatoa maelezo yake ya social interaction zingine kutoka mpaka upate permits.
 
Hivi JPM alisema tumwachie Mungu au anahamasisha watu waendelee kujazana kwenye nyumba za ibada na kuaminisha watu janga linaweza kutoweka kwa maombi?! Ajabu anatolea mfano wa wana-Israel na ugonjwa wa tauni badala ya kutuambia katika dunia ya leo ni janga lipi liliwahi kutoweka kwa ibada!!!

Btw, yaani seriously unalinganisha akina Kinjeketile Ngwale waliokuwa hawajui lolote kuhusu sayansi zaidi ya matambiko, na JPM anayefahamu umuhimu wa sayansi kwenye kupambana na majanga?!
 
Huyo akishakuona umemsifia tu Magufuli, atataka kumcrush magufuli au nchi, kwa namba yoyote ile, ndio roho lake linasuhuzika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe una matatizo. Unafikira za kimihemko. Kutompenda JPM kusiwe ni kikwazo cha kuwa na fikra huru. Utapata ugonjwa wa moyo maana unaye hadi 2025.
 
Duh!....hayo maneno uliyomalizia hapo chini....🙄🙄🙄...
 
Mleta mada amepotosha kwa kiasi kikubwa. Ameandika uwongo mwingi na kuwaamunisha watu yasiyokuwepo.

Sidhani kama anazifahamu nchi za Magharibi labda ni wale wanaoenda leo, wanaondoka keshokutwa.

Kama ulivyonena, hakuna nchi ambazo ni vigumu sana kuishi bila kufanya kazi, kama nchi za Magharibi.
 
Hivi wewe kwa akili yako ya kimihemko unadhani JPM alimaanisha hiyo? It was a political statement tu.
 
Mkuu kwa nchi za Africa ni HAIWEZEKANI, ili upate mlo ni lazima utoke otherwise utakufa njaa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vijijini ndio kuna hatari zaidi kama lockdown itafanyika, hakuna miundo mbinu yoyote ya kumuwezesha mtu kukaa ndani hata siku moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..kwenye kuzuia watu wa nje kuingia nchini nakubaliana na wewe.

..lakini janga hili lime-expose uwezo wa Jpm na uwezo wa serikali yetu.
Lime expose Kwa aslimia ndogo saana, tunasubilia full detailed capacity na nadhani in few days tutaelewa zaidi!
 

Siamini kuwa mtu yeyote anaemuabudu Magufuli atakuwa na mental capacity ya kuelewa logic iliyomo kwenye post yako hii.
 
Wewe una matatizo. Unafikira za kimihemko. Kutompenda JPM kusiwe ni kikwazo cha kuwa na fikra huru. Utapata ugonjwa wa moyo maana unaye hadi 2025.
Ngoja nikupuuze if you don't mind.
 

Sasa ndio muone akili au mantiki ya mtu kutumia pesa zake nyingi kununua ndege, kujenga reli etc wakati watu wake hawawezi kupata maji salama.
Halafu kuna mtu anadai huyo ndie Rais alietakiwa!! Pathetic.
 
Umeongea kama MTU smart, watanzania hatutambui kuwa hakuna jipya chini ya jua, we think we can outsmart smartness itself!!
 

Subiri siku nchi zote jirani zetu zitakapofunga mipaka yao na sisi na kuzuia watu kutoka kwetu kuingia kwao ndipo utaelewa maana ya maamuzi ya kipumbavu yanayochukuliwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…