"
JokaKuu, post: 35..hata mkutano wa wakuu wa EAC umeshindikana kwasababu Magufuli, Nkurunziza, na Salva Kiir, wameshindwa ku-connect na wenzao.
Hapa kuna tatizo. Kuna kitu kinaitwa kukubaliana kutokubaliana na ni kawaida. Hata hivyo, kukaa meza moja ni muhimu bila kujali mnakubaliana nini.
Ndivyo akina Nyerere, Kaunda, Khama, n.k. walivyoweza kutatua matatizo ya ukanda huu wakati huo.
..tumefika mahali Tz iko fungu moja na Burundi, na South Sudan. Jambo hili haliko sawa.
Tulisema mapema katika siasa za kimataifa tumetoweka kabisa na kupoteza influence yote tuliyokuwa nayo.
..mimi nadhani tatizo ni msimamo na mtizamo wake kuhusu covid19 na hatua zinazopaswa kuchukuliwa. Siamini kama lugha ndio tatizo.
Na sidhani kama lugha inaweza kuwa kikwazo kwani si viongozi wote duniani wanaongea lugha moja. Ninachokiona ni vision, kwamba, nini mtazamo na hoja inajengwaje au kubomolewa vipi.
..Pia angeweza kuwakilishwa na VP, PM, au Waziri wa mambo ya nchi. Kwanini hilo halikufanyika?
Hili lilifanyika mwanzoni mwa utawala na ilipofika wakati wa Tanzania kuwa mwenyeji wa SADCC ilikuwa kasheshe. Kila kiongozi alitaka kutuma mwakilishi ,tukaona zile ''ziara ''.
Kutuma mwakilishi katika Capacity ya Ukuu wa nchi ni ''dereliction of duties'
Nyerere alizungukwa na Manguli kama Salim Ahmed Salim, Hashim Mbita, J.Samwel Malecela, Ibrahimu Kaduma, Cleopa Msuya , Sokoine n.k. Pamoja na hayo ilipolazimu kiongozi wa nchi, alikwenda mwenyewe
Katika zama hizi kutuma uwakilishi si tu ni kutelekeza majukumu lakini pia tujiulize kuhusu wanaotumwa!