Janga la COVID-19: Rais Cyrill Ramaphosa aitisha mkutano wa nchi jirani na SA

Janga la COVID-19: Rais Cyrill Ramaphosa aitisha mkutano wa nchi jirani na SA

Kama yangekuwa ni maamuzi yake asingekubali uenyekiti wa SADC
Kama lugha haipandi angekataa
Mlikuwa mnampongeza humu alipopewa uenyekiti
Akili zenu hazina akili
Kwani siku hizi lugha inaweza kuwa tatizo?
Bavicha mnajitoa ufahamu tu,,Rais kaongea chato dunia nzima imemsikia
 
May 8, 2020
Yaounde, Cameroon

Wafanyakazi 100 sekta ya afya waambukizwa corona

Equinoxe Tv: The 6PM News, Friday, May 8, 2020
Serikali ya Cameroon imetangaza kuwa zaidi ya wafanyakazi 100 wa hospitali nchini humo wameambukizwa virusi vya coronavirus baada ya kupimwa.

Source : Afrique Replay TV
 
leo mzee mzima kachemsha yaani kama Mwenyekiti wa SADC hana excuse ya kukosa mkutano na head of states! Ndo maana nilisema atoke Chato akae Dodoma capital city! Kwenye crisis management nampa 0/10! Sasa mbona Mkapa (Guardian wake) asimshauri, kama Kabudi kashindwa? Amemea pembe sio?
Kabudi alikuwa amefuata dawa Madagascar utadhani yeye ni Waziri wa Afya. Sasa Jiwe akakosa mkalimani. Gerson Msigwa naye labda awe ana dictionary karibu..
 
Ndiyo maana nikasema kutojua kiingereza sio tatizo
Kuna wakalimani

Ni tatizo,umejifunza/umetumia kiingereza Primary,Secondary(O/A 'level),University(Bachelor,Masters,Ph.d),Kazini then unashindwaje kuifahamu lugha hio?
 
Mwenyekiti wa AU na Rais wa Afrika Kusini ndugu Cyrill Ramaphosa amelazimika kuitisha mkutano wa mataifa jirani ambayo pia ni wanachama wa jumuiya ya SADC.

Mkutano huo umefanyika kwa njia ya video. Nchi zilizoshiriki ni Afrika Kusini, Angola, Lesotho, Eswatini Msumbiji, Namibia na Zimbabwe.

View attachment 1443627
View attachment 1443648

Huu mkutano ndio utapunguza Maandamano ya watu wake wanaokufa njaa kwa lockdown??
 
Ni tatizo,umejifunza/umetumia kiingereza Primary,Secondary(O/A 'level),University(Bachelor,Masters,Ph.d),Kazini then unashindwaje kuifahamu lugha hio?
Hujaelewa pointi yangu
Namaanisha kutojua kiingereza haiwezi kukufanya ushindwe kuhudhuria mkutano wa kimataifa
Hata hivyo Putin kutoongea kiingereza haimaanishi kuwa hajui, kafanya kazi KBG nchi mbalimbali huko Europe
 
" Hapa kuna tatizo. Kuna kitu kinaitwa kukubaliana kutokubaliana na ni kawaida. Hata hivyo, kukaa meza moja ni muhimu bila kujali mnakubaliana nini.
Ndivyo akina Nyerere, Kaunda, Khama, n.k. walivyoweza kutatua matatizo ya ukanda huu wakati huo.
Tulisema mapema katika siasa za kimataifa tumetoweka kabisa na kupoteza influence yote tuliyokuwa nayo. Na sidhani kama lugha inaweza kuwa kikwazo kwani si viongozi wote duniani wanaongea lugha moja. Ninachokiona ni vision, kwamba, nini mtazamo na hoja inajengwaje au kubomolewa vipi.

Hili lilifanyika mwanzoni mwa utawala na ilipofika wakati wa Tanzania kuwa mwenyeji wa SADCC ilikuwa kasheshe. Kila kiongozi alitaka kutuma mwakilishi ,tukaona zile ''ziara ''.

Kutuma mwakilishi katika Capacity ya Ukuu wa nchi ni ''dereliction of duties'

Nyerere alizungukwa na Manguli kama Salim Ahmed Salim, Hashim Mbita, J.Samwel Malecela, Ibrahimu Kaduma, Cleopa Msuya , Sokoine n.k. Pamoja na hayo ilipolazimu kiongozi wa nchi, alikwenda mwenyewe

Katika zama hizi kutuma uwakilishi si tu ni kutelekeza majukumu lakini pia tujiulize kuhusu wanaotumwa!
Vision ya Magufuli ni kujenga barabara tu, hamna rais pale

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani siku hizi lugha inaweza kuwa tatizo?
Bavicha mnajitoa ufahamu tu,,Rais kaongea chato dunia nzima imemsikia
Ile ilikuwa one way traffic
Katika tele conference angetakiwa kujibu maswali
Hapo ndo pangechimbika
 
Mwenyekiti wa AU na Rais wa Afrika Kusini ndugu Cyrill Ramaphosa amelazimika kuitisha mkutano wa mataifa jirani ambayo pia ni wanachama wa jumuiya ya SADC.

Mkutano huo umefanyika kwa njia ya video. Nchi zilizoshiriki ni Afrika Kusini, Angola, Lesotho, Eswatini Msumbiji, Namibia na Zimbabwe.

View attachment 1443627
View attachment 1443648
Malawi na Zambia walihudhuria?
 
Back
Top Bottom