Kuna mengi sana ya kuchambua hapa.
Kwanza mashoga si wanaume tu, kuna wanawake ambao ni mashoga.
Kwa maana ya ushoga being gay, lesbians are gay, nao ni mashoga.
Pia, mashoga, kwa maana ya gay, si wanaofanywa tu, hata wanaofanya wenzao nao ni mashoga. Wote ni gay. Sisi tunawaita mabasha.
Naona kuna bias sana ya kuwasema wanaofanywa lakini mabasha wao wanaowafanya hawasemwi.
Na hili linaonesha kuwa chuki dhidi ya mashoga kiukweli ni chuki dhidi ya wanawake. Ni chuki dhidi ya femininity.
Jamii yetu inaona hivi, Wanawake ndio wanaofanywa. Na wanawake ni dhaifu kwa kuwa wanafanywa.
Mashoga ni wanaume wanaofanywa, hawa wamezaliwa wanaume lakini wamechagua kuwa kama wanawake. Wanafanywa. Wameacha position ya juu ya glory ya wanaume, wamechukua position ya chini ya wanawake ya kufanywa. Ndiyo maana wanachukiwa sana. Kwa sababu wao wamechagua makusudi kuukataa uanaume katika jamii inayotukuza uanaume.
Na ukichunguza sana utaona watu wenye tatizo kubwa kabisa na mashoga ni wanaune, si wanawake. Wanawake pengine wanataka kuelewa zaidi na wako more ooen kuwa wcceot mashoga. Tatizo kubwa lipo kwa wanaune kwa sababu ndani kabisa wanaune wanaona mashoga ninkama wamewasakiti wanaune kwa kuuacha uanaume na kujiweka kama wanawake. Bila hata kufanya uchambuzi wa kina sana, jamii inatambua kuwa chuki dhidi ya ushoga kiukweli ni chuki dhidi ya femininity.
Ndiyo maana katika jamii yetu utasikia sana mashoga wanaume, hususan *******, wanaandamwa sana. Mabasha, wanaowafanya, hawaandamwi sana, kwa sababu wao mabasha kwa namna fulani bado wana exhibit masculinity, wanafanya, hawafanywi.
Na hukuti sana lesbians wakaandamwa. Hao wanaonekana ni wanawake wanachezeana tu hakuna mtu aliyekataa uanaume hapo.
Tena wanaume wengi wanapata hata fantasies za kuwa na lesbians. Tatizo pekee ambalo wanaume wengine wanalo na lesbians ni kwamba wale studs/dykes (dyke is no longer appropiate term) wale ma lesbian wanaokuwa kama wanaume katika mahusiano yao, kuna wanaume hawawapendi wale kwa sababu wanaona kuwa wale hawajakubali kuwa wanawake wa kufanywa na wanaume.
The issue is vita hii inataka kuiweka masculinity juu na femininity iwe chini. Mtu mwanamme anayekataa mascukinity anashambuliwa. Mtu mwanamke anayekataa femininity anashambuliwa.
Kati ya changamoto kubwa katika kuongelea mambo haya na Watanzania ni ukweli kwamba Watanzania wengi hawana elimu kwenye haya mambo, hawajui haya mambo, Tanzania watu hawaongei sana kuhusu mambo haya.
Watanzania hawafuatilii haya mambo kwa kuwa wengi wana bias against the issue already, na wengi hawajui Kiingereza.
Na kiukweli mengine haya si Tanzania tu hata huku nje bado hayaeleweki.