Janga la P.I.D linatesa sana wadada sasa hivi, poleni sana Warembo

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
11,191
Reaction score
35,870
Ni maambukizi ya viungo vya uzazi vya mwanamke, kwa kawaida huhusisha uterasi, mirija ya uzazi, au ovari. Mara nyingi husababishwa na bakteria ya zinaa, bakteria wengine, UTI iliokomaa na complications wakati wa kuzaa.

Wadada wengi wanalia sana na hii issue kwa maana wengi wao wanakuja kuigundua ikiwa imeshakomaa kupelekea kutibika kwake kuwa kwa gharama na muda mrefu sana na PID kujirudia rudia hata pale ukishatumia dawa.

Wanaume wanachangia sana katika kuwaletea wake zao complication hii, kwa kufanya zina kavu kavu na malaya wa telegram then kubeba vimelea vya bakteria za STI pale atakapokutana na mkewe.

Lakini hii sio tu sababu kuu, UTI za kujirudia rudia siku hizi kupelekea na kutoitibu kwa muda mrefu inapelekea kusababisha inflamation kwenye maungio huko.
 


"Wanaume wanachangia sana katika kuwaletea wake zao complication hii, kwa kufanya zina kavu kavu na malaya wa telegram then kubeba vimelea vya bakteria za STI pale atakapokutana na mkewe"

Unatukosea sana wanaume, kwani wao wakilala nje hawawezi kupata mpaka wapate kwetu sisi? Na unawakosea pia Malaya wa telegram, umewahi kuwapima ukakutana navyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…