Kwanza kabisa sayari kama Venus, Jupiter na mars zinang'aa sana hivyo unaweza kuzijua kutokana na brightness yake.
Lakini kila sayari ina sifa flani mfano Venus orbit yake Iko karibu sana na jua hivo inaonekana mda mchache tu baada ya jua kuzama au muda mchache kabla jua kuchomoza na hii ndio sayari inayong'aa sana, mercury nayo huoneka baada ya jua kuzama lakini haing'ai sana.
Jupiter nayo inang'aa sana na utaijua Kwa rangi yake nyeupe, Kwa pindi hki pale jua linapozama inakuwa usawa wa kichwa (overhead)
Mars pia hung'aa sana na hii ni nyekundu Kwa rangi yake, (ipo karibu na taurus constellation Kwa kipindi hiki)
Saturn huokana lakini kwa beginner unaweza ukadhani ni nyota but ni rahisi kuiona.
Uranus huonekana kama nyota ndogo hivo si rahisi kuiona kama sayari bali utadhani ni nyota tu.
All in all pale jua linapozama tu zile nyota zinaanza kuonekana ni sayari.
Ukitumia app itakusaidia zaidi. Mfano Mimi natumia stellarium kujua location ya vitu vyote angani