Januari 3, 2023 kutakuwa na kupatwa kwa sayari ya Mars

Januari 3, 2023 kutakuwa na kupatwa kwa sayari ya Mars

Huu uzi bila picha in porojo tu, tupieni ata picha za googo kama mshindwa kupiga wajinga nyinyi (kwa sauti ya king kaka)
 
HAYA JAMANI KUMEKUCHA, MARS TAYARI IMEJITOKEZA UPANDE WA PIL, ANGALIA PEMBENI YA MWEZI UTAIONA MARS
 
Wako watakaojifanya hawaionii inazungukwa na Jua tu iko pembeni yake
 
Imechukua kama saa moja na dakika 45 hivi mpaka mars kutoka upande wapili tangia ilipofunikwa na mwezi
 
Nipe tofauti kwa Muda huo zinavoonekana ili nijue hizi ni sayari na sio nyota
Kwanza kabisa sayari kama Venus, Jupiter na mars zinang'aa sana hivyo unaweza kuzijua kutokana na brightness yake.

Lakini kila sayari ina sifa flani mfano Venus orbit yake Iko karibu sana na jua hivo inaonekana mda mchache tu baada ya jua kuzama au muda mchache kabla jua kuchomoza na hii ndio sayari inayong'aa sana, mercury nayo huoneka baada ya jua kuzama lakini haing'ai sana.

Jupiter nayo inang'aa sana na utaijua Kwa rangi yake nyeupe, Kwa pindi hki pale jua linapozama inakuwa usawa wa kichwa (overhead)

Mars pia hung'aa sana na hii ni nyekundu Kwa rangi yake, (ipo karibu na taurus constellation Kwa kipindi hiki)

Saturn huokana lakini kwa beginner unaweza ukadhani ni nyota but ni rahisi kuiona.

Uranus huonekana kama nyota ndogo hivo si rahisi kuiona kama sayari bali utadhani ni nyota tu.

All in all pale jua linapozama tu zile nyota zinaanza kuonekana ni sayari.

Ukitumia app itakusaidia zaidi. Mfano Mimi natumia stellarium kujua location ya vitu vyote angani
 
watu hamuelewi, mwezi siyo kwamba utazima au kubadilika rang, ila ni sayari ya mars itamezwa na mwezi kwa lugha nyepesi. Mida ya saa 4 mars ilionekana pembeni ya mwezi. Mpaka sasa tunaisubiri itokee upande wa pili muda mchache ujao.
sawa mkuu basi mimi sijui kitu, ngoja nikalale.
 
Imeshaachiwa
Screenshot_20230104-003820.jpg
 
Back
Top Bottom