Januari Makamba awajibu wanaohoji mpango wake wa kugawa mitungi ya gesi

Januari Makamba awajibu wanaohoji mpango wake wa kugawa mitungi ya gesi

saidoo25

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
624
Reaction score
1,456
Waziri wa Nishati, Januari Makamba amewajibu watu wanaohoji mpango wake wa kugawa mitungi ya gesi kwa wanawake katika ziara anayoendelea nayo katika mikoa 14 ya Tanzania na kusema wacha wabishane lakini lazima twende mbele

“Wacha watu waseme wabishane lakini lazima twende mbele kwenye nishati safi ya kupitia” amesema Makamba 14 Julai 2022, Sengerema Mwanza


Chanzo: Instagram ya wizara_ ya nishati_ tanzania
 
Hii tabia yake ya kujidai much know asiyesikia ndio itazidi kumpoteza.

Kulazimisha kupeleka majiko ya gesi vijijini wakati uwezo wa kujaza hiyo gesi itakapoisha hawana ni kujidanganya.

Baada ya hii publicity anayofanya, namshauri arudi huko vijijini anapogawa hiyo mitungi na majiko ya gesi after 4 months, more than 90% ataikuta imechafuka vumbi store.
 
future ya nishati ya majumbani hasa kwa kupikia ipo kwenye gesi na si umeme. Ni jambo zuri kwa Makamba.
 
Namuelewa waziri, japo wanakijiji bado vipato haviruhusu. Ila ni heri tu
 
Back
Top Bottom