Januari Makamba awajibu wanaohoji mpango wake wa kugawa mitungi ya gesi

Januari Makamba awajibu wanaohoji mpango wake wa kugawa mitungi ya gesi

Waziri wa Nishati, Januari Makamba amewajibu watu wanaohoji mpango wake wa kugawa mitungi ya gesi kwa wanawake katika ziara anayoendelea nayo katika mikoa 14 ya Tanzania na kusema wacha wabishane lakini lazima twende mbele

“Wacha watu waseme wabishane lakini lazima twende mbele kwenye nishati safi ya kupitia” amesema Makamba 14 Julai 2022, Sengerema Mwanza

Chanzo: Instagram ya wizara_ ya nishati_ tanzania
Amechoka kuishi ameanza kuongea UCHURO juu yake mwenyewe.
 
MASWALI 40 & Majibu 40 -ya JANUARY.: Ati kijana mwenye maono na ambitions, Asee woe to tanganyika.
 
Hii tabia yake ya kujidai much know
Makamba ana muonekano wa uelewa na na busara lakini akiongea dakika tano off the script unagundua ni mtupu na hana exposure japo wanasema kasoma / kaishi Minnesota.

Kiongozi wa nchi za mbele hawezi kamwe kuwaambia wananchi au wakosoaji "nyinyi endeleeni kubishana mimi naendelea mbele kwa mbele."

Waziri mwenye upeo kwa ki third world kama Makamba mpiga kura wake ni mmoja tu: Rais.

Na akishagundua Rais mwenyewe mwepesi basi anaweza kusema na kufanya lolote.
 
Waziri wa Nishati, Januari Makamba ameendelea kushikilia msimamo wake wa kuendelea kugawa majiko ya gesi na kusisitiza kuwa hatasikiliza maneno akisema lengo kupata mrejesho kwa Watanzania kuhusu matumizi ya sahihi ya nishati hasa kwa vijijini.

“Kuna watu wanapigapiga maneno oooh unagawa gawa gesi , hatusikilizi hayo maneno” Makamba



Chanzo: Mwananchi _official Julai 17, 2022
 
Waziri wa Nishati, Januari Makamba amewajibu watu wanaohoji mpango wake wa kugawa mitungi ya gesi kwa wanawake katika ziara anayoendelea nayo katika mikoa 14 ya Tanzania na kusema wacha wabishane lakini lazima twende mbele

“Wacha watu waseme wabishane lakini lazima twende mbele kwenye nishati safi ya kupitia” amesema Makamba 14 Julai 2022, Sengerema Mwanza

Chanzo: Instagram ya wizara_ ya nishati_ tanzania
January mbona anakua na maneno mazito, ajue yeye ni mtanzania Kama tulivyo wengine, na wasemao wanawakilosha watanzania wengine,

LAZIMA na SIO ombi kujua kukaa pale alipo kwamba anawazidi watz wote akili, Iyo ni ofisi ya umma leo yupo kesho hayupo ,kwani wamepita wangapi?

Nimtake apunguze kibri, WENDA lengo lake ni zuri , ila kama ameamua kugawa mitungi basi agawe KWA KILA familia mtungi mmoja tz mzima, vinginevyo SIO haki na ni ubaguzi ndani ya nchi
 

Makamba (hope huwa unasoma hizi nyuzi) haya si ndiyo majiko ya kuayendeleza na kugawa kwa wananchi?
 
Apunguze bei ya hiyo Gesi anaweza kugawa ikiisha wakashindwa kupata mipya sababu ya bei kuwa juu sana, wiki Iliyopita mtungi wa kg6 nimenunua sh 25,000/= siyo pesa ndogo kwa mtu wa kijijini ujue weee manyuzi shauri yako.
Na kwann ipande au inatoka Russia? Hawa jamaa hawaeleweki
 
Hii tabia yake ya kujidai much know asiyesikia ndio itazidi kumpoteza.

Kulazimisha kupeleka majiko ya gesi vijijini wakati uwezo wa kujaza hiyo gesi itakapoisha hawana ni kujidanganya.

Baada ya hii publicity anayofanya, namshauri arudi huko vijijini anapogawa hiyo mitungi na majiko ya gesi after 4 months, more than 90% ataikuta imechafuka vumbi store.
Mingi itageuzwa vigoda! Watu myopic kama hawa wanapoendesha nchi inakuwa ni tatizo sana.
 
Back
Top Bottom