Makamba hauaminiki kwa sababu una majibu yasiyojitosheleza na yanayochelewa kuja kwa wakati, na mara nyingine hauna consistence kwenye majibu yako.
Leo unasema hivi, ukipingwa unabadilika kesho unasema tofauti about same thing, ni kama unaangalia uchochoro wa kujifichia kwenye majibu yako, ndio maana huaminiki.
Mfano.
1. Kuhusu ile crane ya tani 26 uliyoagiza toka nje, ukaambiwa mbona hata hapa Tanzania zipo crane zenye uzito huo? ukasema inatakiwa isiyohamishika, ok fine, mpaka leo hiyo isiyohamishika iko wapi?
2. Au kuhusu tatizo la umeme lililowahi kuwepo, ukatutangazia mgao wako nchi nzima kwa kisingizio awamu iliyopita mitambo ilikuwa haifanyiwi service, then after ukadai mgao utasahaulika, lakini wapi, mgao bado upo mpaka juzi tumetangaziwa mwingine.
Baadae ulivyoona mambo sio ukabadilika, mkatangaza sababu ya mgao wa umeme ni ukame, ghafla akatokea mtendaji bwawa la Nyumba ya Mungu akasema maji yaliyopo kule yanatosha kuwasha umeme kwa muda mrefu ujao, Makamba kimya...
Halafu hii tabia yako ya kukimbilia kuwaona wanaokuhoji ni maadui, ndio itakumaliza kabisa, usijione special usiyehojika, you are not, hicho cheo chako ni cha umma, wewe sio CEO wa private company.
Mwanzo ukihojiwa ulisema tatizo ni uwaziri wako, kama vile wewe ndie waziri wa Nishati pekee uliyewahi kutokea nchi hii.
Leo unawaambia wanaokuhoji wakuue, hii maana yake unakimbia majukumu yako, unajiona unaonewa unapoulizwa kuhusu yale yanayoihusu wizara yako, sasa kama hutaki kuulizwa wewe unataka aulizwe nani?
Anyway, tatizo ni la yule aliyekuweka hapo, amekudekeza matokeo yake unajiona kama "mtoto wa mama usiegusika", sasa kwa huu utoto wako, mtachafuka wote.