January Makamba amefiti vizuri Wizara ya Mambo ya Nje. Heshima na ushawishi wa Tanzania duniani ni ya kiwango cha juu sana

January Makamba amefiti vizuri Wizara ya Mambo ya Nje. Heshima na ushawishi wa Tanzania duniani ni ya kiwango cha juu sana

Wizara imetulia, mambo yanafanyika vizuri kwa maneno na matendo. diaspora na wafanya biashara kimataifa kwa ujumla wao, wanakubali kazi na jitihada za wizara kupitia Waziri huyu kijana na mbunge wa Jimbo la bumbuli mh.January Makamba..

Mchango wa Tanzania kwenye forums mbalimbali duniani mathalani kwenye masula ya amani, Elimu , chakula, afya, hali ya hewa, uwekezaji, utalii, uchumi, nishati, viwanda n.k, na kijana huyu amemuwakilisha Rais Dr Samia Suluhu Hassan vizuri sana, pale ambao yeye binafsi anapokua ametingwa na majukumu mengine mazito ya urais ya kitaifa au kimataifa...

heshima na ushawishi wa Tanzania kimataifa ni wa kiwango cha juu sana hivi sasa. na matokeo yake fursa za masomo na ufadhili wa masomo nje ya nchi umeongezeka sana katika nyanja za sayansi, na teknolojia, ajira za walimu wa kiswahili na afya nje ya nchi, biashara, kumiminika kwa watalii na wawekezaji wa nje n.k

una shauri Mh.January Makamba waziri wa mambo ya nje ya nchi, aongeze juhudi zaidi eneo gani la kisiasa, kijamii au kiuchumi ili Tanzania iendelee kunufaika, kuaminika na kuheshimika zaidi duniani?🐒
Utulivu au hakuna miradi yenye maokoyo ya kukwapua?..... unajitoa ufahamu alichofanya Wizara ya nishati?
 
Asante mkuu kwa kuliuona hilo na wewe..hawa jamaa wanatuona sisi wajinga sana. Eti anakuja huku kusifia.
mwisho wa ujinga ndio mwanzo wa uerevu...

ni hatari wajinga kujikusanya pamoja maana wanaweza wakakubaliana hata kujitumbukiza ziwani huku wanaona wenzao wakizama na kutafunwa na mamba lakini wanaendelea kutumbikia hadi waishe wote dah!🐒
 
Utulivu au hakuna miradi yenye maokoyo ya kukwapua?..... unajitoa ufahamu alichofanya Wizara ya nishati?
mambo yanabadilika gentleman,
huoni kule Arusha kuna jamaa alikuaga mnyang'anyi wa malori ya watu na sasa ni nabii?🤣

kukariri ni mambo ya kizamani sana 🐒
 
Mwizi tu huyo kazi kumpiga mama fix, ule utapeli wake wa kujenga magorofa ya uwekezaji kwenye majiji nje ya nchi unaendeleaje?!.
Kuna watu hawana huruma kabisa na pesa za walipa kodi, imagine miradi ya hapa hapa bongo tu udanganyifu/wizi ni mwingi je huko nje ya nchi hali itakuwaje...si ndio yatajengwa majengo HEWA kabisa!!.
mbona mpango ni mzuri sana,
hapo Kenya tu tuna mgorofa moja mkubwa mno, halafu matata sana wa Tz, kumbi za aina mbalimbali, malls na miofisi mikubwa kubwa ya kitaifa na kimataifa imesheheni humo,

kuna ubaya gani tukipata maokoto kwa namna hiyo pia 🐒
 
Toka lini watanzania wanafatilia maswala ya mambo ya nje,hizo ni Wizara zisizokuwa na mchecheto.

Ili tujue yeye ameiva kwenye uongozi,apewe Wizara zainagusa Wananchi moja kwa moja kama Ardhi,Umeme,Maji au TAMISEMI uone kama hajachemka.
kwahiyo diaspora, wanafunzi, wafanyabiashara sio wananchi?

by the way,
kama hamfuatilii, huu ndio mrejesho sasa wa kinachoendelea 🐒
 
Back
Top Bottom