Uchaguzi 2020 January Makamba asikitika kupitishwa bila kupingwa, atamani angechaguliwa na Wananchi wa Bumbuli

Uchaguzi 2020 January Makamba asikitika kupitishwa bila kupingwa, atamani angechaguliwa na Wananchi wa Bumbuli

January Makamba anasema mwaka 2015 kwenye kura za ubunge alifaulu kwa 84% na mwaka huu baada ya kufanya kazi kubwa jimboni alitegemea kufaulu kwa 90%.

Lakini kwa bahati mbaya kwa yale yaliyotokea amejikuta tayari amepitishwa kuwa mbunge jambo ambalo halimpi fahari yoyote kama mwanasiasa " hai".

January amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter.

My take; January kupitishwa bila kupingwa ni ufaulu wa % ngapi?

Maendeleo hayana vyama!
Kwa maana hiyo ni kuwa hakuwa tayari inamaanisha kuwa kasukumiwa huko
 
'Nahisi' Mchezo uliofanyika mwaka huu Nchi nzima hasa kwny majimbo yote ya watoto wa Mjini ilikuwa ni 'kukaa mezani' na wapinzani wako na kuwaomba wakosee kujaza fomu za uteuzi then wanawekeana Pingamizi wao kwa wao mwishowe wote wanakatwa unabaki peke yako
Umeona mbali sana.
 
Mamba huwa anamla mwanadamu huku analia, eti anamuonea huruma! Ndio Waswahili wakapata msemo wa "machozi ya mamba"
You are very right..jamaa anapiga tuu Siasa huyo, na kama alijua hiyo kitu haifai si na yeye angejitoa ili huo mchakato uanze upya aone ata kama Kura za maoni za CCM atapita..asilete mbwembwe.
 
Mnafiki mkubwa huyu. Madhulumati haya!
Kuna baadhi ya watanzania wenzetu hawana aibu! Wamejaa ushetani na nafsi zao haziwasuti kabisa! So sickening!
 
Zaidi ya asilimia elfmoja bwashee
Nakumbuka Rais Magufuli aliwapongeza Mrema na Cheyo kwa kumuunga mkono na kuwataka wapinzani wengine wafuate nyayo zao ili kuokoa fedha za walipa.

Kwani kupiga kura za Ndio na Hapana hakuna gharama bwashee?!
 
Back
Top Bottom