Uchaguzi 2020 January Makamba asikitika kupitishwa bila kupingwa, atamani angechaguliwa na Wananchi wa Bumbuli

Uchaguzi 2020 January Makamba asikitika kupitishwa bila kupingwa, atamani angechaguliwa na Wananchi wa Bumbuli

Siku hizi Viti maalumu hadi wanaume
January Makamba anasema mwaka 2015 kwenye kura za ubunge alifaulu kwa 84% na mwaka huu baada ya kufanya kazi kubwa jimboni alitegemea kufaulu kwa 90%.

Lakini kwa bahati mbaya kwa yale yaliyotokea amejikuta tayari amepitishwa kuwa mbunge jambo ambalo halimpi fahari yoyote kama mwanasiasa " hai".

January amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter.

My take: January kupitishwa bila kupingwa ni ufaulu wa % ngapi?

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwa sasa January ni mbunge wa viti maalumu na hilo ndio linalomsikitisha.

Yaani Ummy Mwalimu akishinda atakuwa na hadhi kubwa zaidi yake!
Hata kwa wabunge wa viti maalum hayupo.

Maana wale wamegawanyika. Wako wa kuteuliwa kupitia jumuiya za vyama, wako wa kuteuliwa na rais, na kadhalika.

Yeye kote hayupo.

Kisheria ubunge wake unaweza kuwekewa pingamizi. Maana hautambuliki kikatiba.

Ndiyo maana hata yeye mwenyewe anajistukia.
 
Labda ndio maana awali Bob Chacha Wangwe alishinda kesi yake pale mahakama kuu kuhusu wasimamizi wa uchaguzi!
 
Ubunge wa aina hiyo hauna raha,thamani wala heshima mbele ya Jamii.
Seriously ?, Wabunge wetu hawa (overpaid, underperforming) raha yao ni kuitwa waheshimiwa na kuwa watawala...,

Thamani ? (hio thamani unaipima vipi) kama ni financially ulizia posho zao na pension zao (kipindi hiki ambapo mtaani ni pachungu umejiuliza kwanini watu wanapigana kufa na kupona kwenda mjengoni)? Kupita direct inamaanisha ni kupunguza gharama za Kampeni....
 
Hii ndiyo inayotufanya tuamini kuwa Magufuli aliwateua watu wasio na akili kuwa wakurugenzi!

Tunamlaumu zaidi Magufuli. Hivi kati ya Watanzania zaidi ya milioni 60 hakuwapata watu wenye akili wa kuweza kuwa wakurugenzi, hata kufikia hatua akawajaza watu wenye uwendawazimu kuwa wakurugenzi?

Kupitishwa bila kupingwa ni uwendawazimu, ni ujinga na ujuha wa hali ya juu. Hakuna mwenye akili, awe CCM, CHADEMA, ACT au mwingine yeyote anayeweza kulifurahia au kulishabikia hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama imemuuma sana....
Basi nafikiri anpaswa kujitoa (kuwajibika) ili asiendelee kisikitika...[emoji41][emoji41]
 
January Makamba anasema mwaka 2015 kwenye kura za ubunge alifaulu kwa 84% na mwaka huu baada ya kufanya kazi kubwa jimboni alitegemea kufaulu kwa 90%.

Lakini kwa bahati mbaya kwa yale yaliyotokea amejikuta tayari amepitishwa kuwa mbunge jambo ambalo halimpi fahari yoyote kama mwanasiasa " hai".

January amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter.

My take: January kupitishwa bila kupingwa ni ufaulu wa % ngapi?

Maendeleo hayana vyama!
Mpuuzi huyu na wakati alisuka mkakati yeye na DED
 
Labda ndio maana awali Bob Chacha Wangwe alishinda kesi yake pale mahakama kuu kuhusu wasimamizi wa uchaguzi!
Ile hukumu imenirudishia imani kidooogo kwenye mahakama zetu.

Na inaonesha kwamba.

1. Ujasiri unazaa matunda. Watu waache uoga.

Katika mchezo wa kuigiza wa maisha ya Kaizari, kwa mujibu wa William Shakespeare, ambaye alimsoma Plutarch, na kutafsiriwa kwenda Kiswahili na Julius Nyerere.

Julius Kaizari anasema.

"A coward dies a thousand times before his death, but the valiant taste of death but once. It seems to me most strange that men should fear, seeing that death, a necessary end, will come when it will come."

William Shakespeare, Julius Caesar

2. Kulalamika lalamika pembeni tu bila kufungua jesi mahakamani hakusaidii sana.

3. Kila jitihada, hata ikiwa ndogo vipi, hata hizi za kulalamika lalamika pembeni tu, inasaidia. Hata kama ni kwa kujenga uelewa tu.

4.Kujipanga kuwa na mtandao wa ndani na nje ya nchi ni kitu muhimu. Bob amejipanga vizuri sana ndani na nje ya nchi. Namfuatilia kwa makini.

5. Wanasheria wenye mapenzi mema kufanya kazi pamoja pro bono ni kitu muhimubsana. Nilikuwa naongea na Shangazi kuhusu hii kesi akawa ananielezea kazi waliyofanya ni kubwa sana kuliko inavyoonekana kijuu juu. Ila wameifanya, tena pro bono.
 
Aache unafiki,
Kama ameumia ajitoe ili mchakato uanze upya.
Maana akijitoa hapatakuwepo na mgombea kwa hiyo uchaguzi utaitishwa upya.

Back
Top Bottom