January Makamba: Bwawa la Nyerere limebakiza Mita 2 za Ujazo ili kuwa na uwezo wa kuzalisha Umeme

Serikali imetangaza kuwa, wiki moja ijayo kina cha maji katika bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere (JNHPP) litakuwa na uwezo wa kuanza kuzalisha umeme.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Mei 31, 2023 na Waziri wa Nishati, Januari Makamba wakati akiwasilisha bajeti yake kwa mwaka 2023/24 ambayo ameliomba Bunge lipitishe jumla ya Sh3.048 trilioni.

Waziri Makamba amesema kuwa ujazo wa maji uliofikiwa katika Bwawa hilo ni mita za ujazo 163, lakini kiwango kinachotakiwa bado mita za ujazo mbili.

“Mheshimiwa Spika, ninafurahi kulitaarifu Bunge lako kuwa, wiki ijayo hata tukiamua kuanza uzalishaji wa umeme tunaweza kwani kiwango cha chini cha uzalishaji maji tumebakiza mita za ujazo mbili tu,” amesema Makamba.
Hata hivyo Waziri amesema kuwa uzalishaji wa umeme utakaoanza rasmi katika mwaka huu wa fedha, utaingizwa katika gridi ya Taifa mwakani sambamba na umeme wa jua
 
Hiyo ni gia ili apate mitririoni yake 3 hapo..
Ngoja tumpe mwezi kabisa then utaniambia..
 
Alikuwa mjinga,huwezi haribu uchumi sekta zingine Kwa visingizio vya kipuuzi
Swali Mbona Sasa hivi Kila sekta Kuna pesa tena zimeongezeka mara 2,zometoka wapi? Mfano Watoto wa vyuo Vikuu wote wamepata mkopo yule mtu wenu alishindwa [emoji1787][emoji1787]
Hizo hela zipo wapi au mnagawana pesa zetu za kodi kama nyugu ,kama mlivyofanya kule kwa SGR kupitia mbarawa
 
Kwani huoni miradi ikitekelezwa? Sasa hivi bwawa linaenda kuzalisha umeme unadhani wanalipa kamasi zako broo
 
Hatinaye mashine ya kwanza kuanza kuzalisha umeme,

Mambo tayari huko [emoji91][emoji91][emoji91]
Hongera Serikali, Hongera Rais na Hongera Waziri Makamba

---

View attachment 2641420
Picha: WAZIRI wa Nishati, January Makamba
WAZIRI wa Nishati, January Makamba ameliambia Bunge kuwa kwa muda wa wiki moja kuanzia leo (Mei 31, 2023), Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere litafikisha kiwango cha ujazo wa maji utakaowezesha kuanza uzalishaji wa umeme.

Waziri huyo wa Nishati amesema hayo wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2023/ 2024 bungeni mjini Dodoma leo.

“Ninayo furaha kulitaarifu Bunge lako Tukufu kwamba katika kipindi cha wiki moja kuanzia leo, bwawa letu litafikisha kiwango cha ujazo wa maji (yaani mita 163 kutoka usawa wa bahari) kinachowezesha kuanza uzalishaji wa umeme” amesema Makamba.

Chanzo: Habari Leo
samia unamuogopa makamba?

tumbua huyu mtu anaharibu sana hiyo wizara na bado anakuita dhaifu akiwa na kina nape lakini bado unamkumbatia!
 
Yaani anachofanya makamba ni kuwalainisha wabunge wapitishe bajeti tu lakini anajua anasema uongo eti mwezi wa 6/2023 ikifika muda huo mtaona stori zinaanza Mungu atupe uhai tu
 
Hatinaye mashine ya kwanza kuanza kuzalisha umeme,

Mambo tayari huko 🔥🔥🔥
Hongera Serikali, Hongera Rais na Hongera Waziri Makamba

---

View attachment 2641420
Picha: WAZIRI wa Nishati, January Makamba
WAZIRI wa Nishati, January Makamba ameliambia Bunge kuwa kwa muda wa wiki moja kuanzia leo (Mei 31, 2023), Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere litafikisha kiwango cha ujazo wa maji utakaowezesha kuanza uzalishaji wa umeme.

Waziri huyo wa Nishati amesema hayo wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2023/ 2024 bungeni mjini Dodoma leo.

“Ninayo furaha kulitaarifu Bunge lako Tukufu kwamba katika kipindi cha wiki moja kuanzia leo, bwawa letu litafikisha kiwango cha ujazo wa maji (yaani mita 163 kutoka usawa wa bahari) kinachowezesha kuanza uzalishaji wa umeme” amesema Makamba.

Chanzo: Habari Leo
Mkuu hujamwelewa au pengine hajaeleweka.
Kwa taarifa yako ufungaji mitambo yenyewe bado haijakamilika.
Kutandika waya za umeme kusafirisha hadi Chalinze bado.

Huyo waziri naye taahira na awaachie wataalam waelezee.
Maana yake ilikuwa maji kwenye bwawa sasa ni yale ya kutosha kuzalisha umeme by june 2023.
 
Back
Top Bottom