January Makamba: Sisi hatuzalishi mafuta

January Makamba: Sisi hatuzalishi mafuta

Roy Logan

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2021
Posts
790
Reaction score
3,190
Waziri wa Nishati January Makamba, amesema kwamba bei za mafuta nchini inatokana na gharama mbalimbali ikiwemo zile zilizotumika kununulia mafuta, gharama ya usafirishaji na gharama za biashara yenyewe hapa nchini.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 5, 2022, bungeni Dodoma, wakati kujadili hoja iliyotolewa na Mbunge wa Kilindi, Omari Mohamed Kigua, ya kusimamisha shughuli za Bunge zilizokuwa zikiendelea ili kujadili hali ya mfumuko wa bei ya mafuta nchini.

"Wote tunajua bei za mafuta zimepanda duniani na sisi kama nchi sio wazalishaji wa mafuta tunanunua mafuta kutoka nje na sehemu kubwa ya bei ya mafuta inayopangwa nchini inatokana na gharama ya mafuta yenyewe, gharama ya kuleta, kodi na tozo mbalimbali na gharama za kufanya biashara yenyewe hapa nchini," amesema Waziri Makamba

Screenshot_20220505-183331_Twitter.jpg
 
Huyu jamaa anajifanyaga smart sana, ila kiukweli tangu achukue hii Wizara, ni kama inauweka wazi upeo wake.
Huyo jamaa alifeli shule... kaunga unga sa hizi yupo hapo alipo. Alafu eti ana ndoto za kuwa namba moja!

NB: Nakumbuka aliwahi kusema tusipate wasiwasi mafuta yapo ya kutosha kwa miezi kadhaa mbele. Kumbe walikuwa wanachakata bei, kuiongeza zaidi.
 
Ila kwahii kauli waziri kakosea. Hili sio jibu lakutupa sisi. Inamaana Zanzibar ambako mafuta ni 2600 wao wanazalisha mafuta?
Ametukosea sana waziri.
Tatizo la watz tunalalamika na hatuchukui hatua wacha watufanye watakavyo.
Kiongozi anaweza kujibu na kufanya atakavyo hakuna wa kumsumbua.
Kuwa kiongozi Tz ni raha sana no stressed 😫
 
Huyo jamaa alifeli shule... kaunga unga sa hizi yupo hapo alipo. Alafu eti ana ndoto za kuwa namba moja!
Ila kwa CCM hii tuliyonayo, wala sitashangaa yeye kuwa mgombea wao siku moja, hii chain, sisi wengine hatuwasogelei, wala hawataki tuwe karibu nao, wanaamini wao ndio wenye hatimiliki na Nchi hii.
 
Back
Top Bottom