"Aliwashinda akiwa hai na atawashinda akiwa kaburini",ujumbe mzito sana huu.
Mimi nikimuona kiongozi yeyote anakakamaza domo lake na kuanza kumshambulia Marehemu, awe wa upinzani ama Ccm huishia kumdhaau sana na kumuona hafai, bila kujali kabla yake nilimchukuliaje.
Wanashindwa kueleza sera na mikakati yao ya maendeleo wanabakia tu kukashifu marehemu, wakati bado wakitembelea nyota yake!
Watuambie sasa, iwe upinzani ama Ccm, ni sera zipi mpya za maendeleo ya kasi walizoziibua wao na kuanza kuzitekeleza zisiwe zile zile alizoziibua mwenzao wanayeshinda wakimkashifu ndiyo wanayotambia?
Tukihoji haya tunaambiwa wasukuma gang, alah, kwa hiyo nchi hii raia wote tumewekewa speed garvanor ya kufikiri nje ya box na kuvishwa miwani ya mbao tusione ukweli ni upi ili sote tubaki machawa wa kunyonya taka taka zao za kila aina siyo?
Tupeni Katiba mpya na bora muone kama hawa genge la mibaka uchumi wataendelea kuwepo na kupiga ngonjera za kinafiki na kuendelea kukojolea akili za raia wa nchi na kutuona sote ni wapumbaf.