Yimakatso
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 7,060
- 9,468
Eeh Mungu hiki ni nini kimeandikwa hapa?View attachment 3048305
Mhe January Makamba na rafiki yake mkubwa wa siku nyingi Mhe Nape Moses Nauye huenda wakatimkia CHADEMA endapo watahakikishiwa nafasi ya January kugombea Urais 2025.
Mhe January Makamba anaona hakuna matumaini tena ya kuwa Rais ndani ya CCM huku akiamini fika kwamba yeye ni kipenzi Cha Watanzania walio wengi.
Bado haijafahamika sababu hasa za January Makamba kutenguliwa ila tetesi zinaonesha ni kushindwa kutekeleza majukumu yake vema.
Hata hivyo bado haijafahamika kama Chadema wanaweza wakampatia nafasi hiyo ya kujaribu bahati yake kama walivyofanya mwaka 2015 kwa Hayati Edward Ngoyai Lowassa au laa.
Kama mpango wao huu wa Siri utafanikiwa huenda tukashuhudia Uchaguzi mgumu zaidi kuwahi kutokea mwaka 2025 kati ya January Yusuph Makamba wa CHADEMA na Dkt Samia Suluhu Hassan wa CCM.
Wakati ni mwalimu wa kweli
Yaani January awe kipenzi cha watanzania wengi kwa lipi hasa analojivunia kulifanya kwa maslahi ya taifa?
Yaani uchaguzi uwe mgumu kisa January kagombea kupitia CHADEMA?
January hana impact yoyote na akigombea against Mheshimiwa Rais Samia basi Samia atapita mchana kweupe bila usumbufu wowote.
Angalau kidogo angegombea Lissu dhidi ya Mheshimiwa Rais Samia hapo pangetokea ugumu kiasi ila bado mama anashinda.