Japan kulipa $536 Million kwa makampuni yake 56 yahame kutoka China, yarudi nyumbani au nchi nyingine za Asia

Kati ya wewe na wajapan Nani anaakili
Wangekua na akili wasingeyaachia hayo mashirika kwenda kuwekeza UCHINA wakati wao wanahizopesa zakuwapa kwanini wasingewapa kabla

Kuwaruhusu wakawekeze huko kwamamiaka kibao nasasa wanawataka wawarejeshe nikigezo tosha kama hawakuwahi kujaaliwa akili
 
Mmarekani angekua anaona mbali asingeacha mchina afikie hapa alipofika angemgandamiza tokea uchumi wake upo chini.......kwa sasa kachelewa sana Marekani ....mchina nae lazima atakua anajipanga ndo maana kwa sasa katulia anaangalia Mmarekani atoe makucha yake yote hadi mwisho ndo ajue ataenda nae vipi.........na Mmarekani atazuia tu bidhaa ambazo ni za teknologia yake je bidhaa ambazo hazina teknolojia ya Mmarekani atafanyaje???Mmarekani kwa China kachelewa sana alitakiwa ashtuke mapema kwa sasa China mwenyewe nae anampango wa kutoa kampuni zake nje ya China maana ameshakua na middle class ya kutosha
 
Kusema all option hata kule IRAN KOREA kote walisema wakatishia mpaka regime change kwayale mataifa kikowapi leo ?!
 
Unazungumzia Mungu yupi Buddha

Hawana Mungu wanajiamni wenyewe hawamwamini hata ngozi nyeusi [emoji23][emoji23][emoji23] ni vigumu sana kukuta raia Mweusi Mchina ukimuta atakuwa chin ya uangalizi maalum[emoji119][emoji119]
 

Hii ni sawa na kucheza Draft mkuu. Mwenzio anakuachia unaenda King lakini mwisho wa siku anakutafuna[emoji23][emoji23]
 
Kwa hiyo wewe unaakili kuliko wajapan hongera
 
Wamarekani wa Jf sijui hua mnawaza nini.. Biashara ya dunia inaendeshwa na mikataba iliyofungwa na kusimamiwa na taasisi kama WTO na mara zote wanasisitiza serikali za mataifa ziliache soko liamue nani achukue na apeleke bidhaa na huduma wapi. Wanasisitiza nchi zifungue mipaka kwa ajili ya uwekezaji na masoko na kuachana na protectionisim.
Leo wamarekani mko hapa mnashadadia marekani kuharibu mifumo ya biashara ya kimataifa na Japan kutoa ruzuku kwa makampuni yake ili yaweze kuwa competitive kitu ambacho hata USA wamekuwa wakikataa na kwenda mbali zaidi hadi kuzipiga faini baadhi ya kampuni kama Airbus baada ya kuwatuhumu umoja wa Ulaya kuwapa ruzuku hivyo kuhatarisha kumtoa kwenye biashara Boeing.
Hivi ni kwamba sisi Tanzania tumejikatia tamaa kwamba hatutokaa tufikie export economy! Na vipi tumeshafika huko halafu taifa fulani linajitokeza kuanza kutuwekea vikwazo tusili access soko la kimataifa simply kwa kuwa wanahisi kwa kufanya hivo makampuni yao yataendelea kuwa makubwa kuliko ya kwetu, hamuoni mnashabikia upuuzi?
China kafika alipofika sio kwa bahati mbaya walikuwa na strategies na moja ya mbinu zinaweza kuwa wizi wa teknolojia ila je ni kila anaeweza kuiba anaweza kubadili alichokiiba kufanyia maendeleo?
Leo USA wanaweza ku explore universe kwa teknolojia aliyoiiba kwa wajerumani. Leo US Airforce wana ndege chapa MIG za Warusi, unajua wanazifanyia nini kama sio lengo lile lile la wizi wa teknolojia?
China inayoogopwa na kufanyiwa figisu leo na Trump ina mizizi yake toka kwa Deng Xiaoping rais alieleta mabadiliko makubwa ie the de-collectivization of agriculture, the opening up of the country to foreign investment, and permission for entrepreneurs to start businesses katika The Great Leap Forward miak ya 70 na 80. Hivi ndo hasa vimeifanya China kufika ilipo. Wizi wa teknolojia ilikuwa nyongeza tu.
Marekani atafanya fitna zote lakini hatafanikiwa kuwashusha wachina kwa kuwa ukiachana na mambo mengine ni ile imani yao kuamini tunaweza na asikwambie mtu wachina ni wachapa kazi
 
MADA ni Japan kuondoa makampuni yake uchina lakini imegeuka kuwa ya US vs china! [emoji3][emoji3][emoji3] Ama kweli wachina wameshikwa pabaya! Hata wakiunguza maharage watasema Marekani kasababisha.
 
Hakuna taifa ambalo litakuwa super power halafu lisianye kama hayo anayo yafanya China na USA Never

Tena acha kujipotosha
 
Hohoooo hoooo
 
Hohooo hoohooo
 
hayo ni matumainio yako; lakini ukweli kwa sasa hivi ndivyo ulivyo. Hujajua nani atakayekuja madarakani tena; usiongelee mambo ya kufikirika. Akija mwingine akabadili mwelekeo tutaliongea lakini hali ya sasa ni hiyo.
He he hee

Mlikuwa wapi siku zote !??..ha haha katika huu Uzi Sexer hawezi kujisogeza

Wakuu mnadondosha fact sio za sayari hii

Mbarikiwe sana
 
He hee hee ... Mimi Leo sina cha maana cha kucomment ..mmemaliza kila kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…