Mtwa Mkulu hakuna mwenye hitimisho kamili ni nani hasa alihusika na kifo cha Kennedy, ripoti rasmi ya serikali nadhani ya Bwana Warren ni kuwa Lee H Oswald ni muhusika pekee, baadhi ya wengi Marekani hawakubaliani nayo, hapo ndipo milango ya conspiracies kibao zimezaliwa! Wengine wakisema CIA, MAFIA, Jeshi la Marekani nk, au Urusi baada ya Marekani kuiwekea ngumu na kuilazimisha Urusi kuondoa Makombora yake Cuba.Hivyo Mkulu kila anayesoma habari za Kennedy huwa anatoa hitimisho yake.Mimi mwenyewe nimebadili mtizamo wangu Mara nyingi, nimepita mahali alipouawa mwezi uliopita nikiwatembeza jamaa zangu toka Tanzania, naanza kuamini risasi iloyomuua Kennedy haikutoka pale juu dirishani, maybe upande wa kichaka kile cha Grass Knoll, Lee Oswald angle aliyokaa ilikuwa ngumu mno kumpata Kennedy akiwa ndani ya gari ikitembea, anyway mauaji ya Kennedy yanabaki kuwashangaza wamarekani wengi kwa kukosa hitimisho wanalolitaka na kuikataa report ya Warren.