Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Hakuna tatizo la Zanzibar kuwa Dubai, Singapore au Paris.Deni wanalipa serikali ya muungano na sio zanzibar yaani sisi watanganyika ni malofa wa kiwango cha juu sana watu milioni 1 wanapata pesa nyingi kiasi hicho. Watanganyima tuamkeni jamani kwa mwendo huu samia mpaka atoke madarakani zanzibar itakuwa kama singapore.
Zanzibar wana SMZ na hilo wakiweza kulifanya si tatizo kwa Mtanganyika hata kidogo
AG wakati huo wa GNU alikuwa Othman Masoud. Yeye na wenzake wa CUF wakasema wanataka SMZ ikope bila kupitia JMT kwasababu hilo linazuia maendeleo, JK akawapa haki yao.
Leo wale wale waliokataa mikopo kupitia JMT wanajibanza migongoni kukomba pesa na kuwaachia Watangayika mzigo wa deni.
Tunachosema hapa ni kuwa SMZ ikope hata Trillioni 1000 , walipe wenyewe
Ikiwa watapitia JMT basi tuonyeshwe wapi na kiasi gani wanarudisha madeni waliochukua
Lakini pia tuangalie ukweli! huwezi kutoa Bilioni 280 kwa watu milioni 1.2 ambao ni sawa na wakazi wa jimbo la uchaguzi la Ubungo wala si Dar ,Arusha, Tunduru au Simiyu
Ni hesabu gani zinatumika ?