Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
inashangaza sana kuona kila jambo linalotokea watu wanalichukulia negetively, hivi swala hapa ni kikwete au maslahi kwa nchi, ni ulitaka rahisi asitafute wawekezaji, au bado mna mawazo ya nyerere kwamba tuache raslimali kwa kua haziozi, soo what? jaribuni kuwa positive angalau kidogo achani kuwaza giza kila wakati jaribuni kuiona nuru! kwa mtindo huu hamtakaa mzione fursa hata kama zitakua sebuleni kwenu! jipange acha kupiga mayowe..period!
Hili jambo ni jema sana kwa nchi ila nasikitika tuna viongozi wa ajabu nchini. Mwezi uliopita alikuja makamu Rais wa Samsung akitokea South Africa alikuja kwa lengo la kuangalia eneo zuri la kujenga kiwanda cha uzalishaji wa bidhaa za samsung nchini. Alipokelewa na afisa wa wizara wakaenda kumtupa bagamoyo bila ya maelezo yeyote yenye umuhimu kuhusu uwekezaji. Kisa ni tu hakuelewana na wakubwa wetu basi wakubwa wetu wakampotezea. Matokeo yake akapanda ndege na kwenda zake Kenya na kuishia zake South Korea. Hawa wawekezaji wanaweza kuwa na nia nzuri ya kuwekeza nchi ila na sisi tunalazimika kubadilika kifikra na kiakili na tuwe na uzalendo zaidi kwenye mambo yenye maslahi ya nchi.
Nashauri wahusika wafanye maandalizi kabambe kuwezesha wawekeze nchini ili tupate kutoa ajira kwa vijana wetu na taifa liende mbele. Tuache ubinafsi na tuwe wazalendo.
Hivi wajapani wameona kwamba pikipiki ndio suluhisho la utatuzi wa usafiri kwa watanzania au vipi, si tayari kuna pikipiki toka Uchina na vibajaji kutoka India?
Sasa nchi yetu inajazwa mapikipiki tu kila kona?
Ingeeleweka kama wangeamua kujenga kiwanda cha magari yenye kutumia malighafi za hapa hapa Tanzania na yenye gharama nafuu, kwani yatazuia magari yote chakavu na yaliyotumia yanayotokea hukohuko Japan.
Pia kiwanda cha magari kingetoa ajira lukuki kwa vijana wengi wahitimu wa masuala ya ufundi na teknolojia na sio teknolojia ya kutengeneza pikipiki hata watoto wa shule wakipewa vifaa vyote si wanaweza kutengeneza vibajaji?
Sasa tathmini ingefanywa kwamba kipi kinalipa kiwanda cha pikipiki au cha magari lakini 10% inasema pikipiki!!!
Imarisheni miundombinu ya gas na jengeni kiwanda cha kuyeyusha chuma kwanza kabla ya kuanza kufikiria viwanda vya auto-industry. Hakuna auto-industry, au building materials vitakavyoweza jengwa kama hakuna viwanda vikubwa vya uyeyushaji chuma. Hizi assembling plants kama zinazofanywa na wachina kwa pikipiki ni upuuzi mtupu.Wakati nikipongeza hatua hii,lakini tukumbuke kuwa pikipiki ni technolijia ya chini sana,na kwa kufahamu uundwaji wake kutajengwa kiwanda cha ku-assemble hizi pikipiki.kitu ambacho wachina wanafanya KKoo muda mrefu tu.
Kama tungefanikiwa kuwashawishi wajapani waweke Auto assembly plant hapo ningempa maksi JK,kwani hii ingetufanya tuachane na biashara ya Magari used.na wajapani hawawezi kukubali makapi YAO wakose pa kuyatupa.
Ushauri kwa serikali.waombe wachina waje kujenga assembly plants za Magari hapa Tanzania kwa ajili ya masoko ya Afrika.in 5 years Toyota watajenga kiwanda.hiki cha Honda tuwashukuru toyo na SanLG kwani ndio sababu hasa ya hawa jamaa kuja.
Kingine si vibaya tukaomba viwanda kwa ajili ya primary resources,na sio secondary ones.kwa mfano,kiwanda na kutengeneza circuit za redio na television Kina maana kubwa kwetu kuliko kiwanda cha redio,kwa maana hii tuombe cluster ya viwanda na sio standalone units ambazo zinatumika Kama political gestures with little meaning.
Imagine dangote angeleta kiwanda cha matofali.
Mkuu, rudia chanzo chako. Sipingani na wewe juu ya bureaucracy na kukosa uweledi wa kushawishi fursa za uwekezaji kwa viongozi wetu, lakini hili la Samsung kujenga kiwanda cha electronics goods kwa Tanzania kwa sasa ni jambo lisilokuwepo kwa sasa. Hii ni kutokana na mazingira husika na sababu nyinginezo kidogo. Rejea tena chanzo chako otherwise hii kitu ni hearsay.
Kaka, uwekezaji una sehemu kuu mbili. Production side and consumption side/(supply side and demand side). Kwamba haina budi kuangalia gharama za uzalishaji na forecast ya mahitaji. Kwa upande wa uzalishaji, no way Tanzania kama itaweza kufanya/ au kupata mwekezaji wa kiwanda cha magari au zana kubwakubwa pasipo kwanza kujengwa kiwanda cha chuma, petol products na gesi. Aidha kwa upande wa consumption power, bado uwezo wetu kama Tanzania+East Africa ni mdogo kununua magari Brand New ukilinganisha na maeneo mengine kunakojengwa viwanda vya magari. Ratio ya idadi ya magari na raia kwa Tanzania ni "almost negligible" wakati ziko nchi idadi ya magari inazidi idadi ya raia wa nchi husika! Kwa sasa, pikipiki ndizo ambazo zina demand kubwa ambayo idadi kubwa ya watanzania+East na Central Africa wanamudu, hivyo lazima waanze na hilo. Kama itatokea uwezo wetu wa kutumia(consumtion power) kuongezeka huko usoni, na viwanda chochezi nilivyovitaja vikijengwa, uwezekano wa kupanua kiwanda cha Honda(kama kitajengwa) kuzalisha pia na magari ni mkubwa. Kwa sasa, economically no!
Kwanini Samsung wasijenge kiwanda cha electronics nchini? Mie nadhani kiwanda cha electronic goods is essential ili watu wetu wajifunze teknolojia ya samsung, kupunguza gharama za simu, majiko ya kupikia, vifaa vya umeme kama pasi, TV etc kutoa nafuu kwa mwananchi wa kawaida naye aweze kuboresha maisha yake, kuongeza mapato ya kodi. Samsung wana umuhimu nchini kama walivyo akina Dangote. Ila nimeshangazwa vice president anapokelewa na afisa tu wa wizara na kisha jamaa anaenda kumtupa Bagamoyo kama vile hana umuhimu. Samsung ni largest electronic company wamewaexceed sony karibuni lakini sisi hatuoni umuhimu wao. Basi subiri huko Kenya watakavyomchangamkia tutasikia wameenda kenya badala ya Tanzania.
Hivi karibuni wamekuja ujumbe wa Sri Lanka kwenye ule mkutano wa Smart Partnership, Wamekuja Mauritius kwenye mkutano na Rais, Na Primeir wa Thailand. Viongozi wetu kikubwa walichokiona kutoka kwa watu ni utalii but wameacha mambo ya msingi kabisa ambayo tungeliweka msisitizo wa kushirikiana na wenzetu. Mfano Sri Lanka na Mauritius wanaviwanda vya nguo na wanauza Marekani na Ulaya. Tungelijifunza wamefanyaje na wamefanikiwaje? Na vp tunaweza kushirikiana nao kuweza kufikia huko. Sisi tumeona utalii (majanga kwa kweli). Thailand ni world number one producer of rice (chakula kinachopenda dunia nzima) na uchumi wao uko zaidi umejikita kwenye kilimo (ndio uti wa mgongo wa Thailand). Kilimo kiliweza kushusha umaskini Thailand by 30% na kuongeza kiwango cha watu wenye pato la kati. Sie hatukuona umuhimu wa kufahamu wamefanyaje tunaangalia umeme wa radi na uwekezaji nchini kwanini tusiwaulize tunashirikiana vp kwenye kilimo since we have large arable land nchini?
Ni kwasababu Samsung wanajenga electronic plant yao Misri ambayo lengo ni ku-target soko la Afrika, Middle East na Europe, na hili limewavutia kwao kwa sababu Egypt inaonekana kuwa imekaa ki-strategic kwa Afrika, Ulaya na Middle East ambapo itaweza kuuza bidhaa zake kwa urahisi Ulaya kutokana na nafuu ya kodi baina ya Ulaya na Afrika, na vilevile middle east ambayo ina soko zuri la electronics goods. Makubaliano husika yalishatiwa saini tangu mwaka jana. Hivyo kwa kampuni hizi MNCs, si rahisi kabla ile haijaanza then waje wajenge kiwanda cha namna hiyohiyo Tanzania ambayo pia iko eastern Africa-ni ngumu, labda uzalishaji wa bidhaa nyingine za Samsung maana wana bidhaa nyingi mno. Ndipo nikakwambia rejea chanzo chako. Samsung to build LE1.7bn plant in Egypt - Economy - Business - Ahram Online
Hapo kwenye red uko sahihi, umeme wa uhakika na ggesi ni muhimu sana kwa sababu ya kupunguza gharama za uzalishaji. Hii Assembling Car Plant, kumbuka Toyota anakusudia kujenga assembling plant Kenya, na kwa sasa, honda si equal-competitor wa Toyota kwa upande wa magari hivyo akifanya kitu cha namna hiyo kwa East Afrika atapata hasara kwani hataweza kushindana katika soko na Toyota. Ila kwa pikipiki yes. Hili la kujenga kabisa kiwanda ndilo linaloweza kufanyika lakini mbali na masuala uliyobainisha (red) ukumbuke pia sasa hivi uzalishaji wa bidhaa kubwakubwa kama gari haufanywi kwa "wholly produced" bali kwa "regional Network production" kwa hiyo tunaweza kuwa na comparative advantage ya malighafi ya chuma, lakini tukakosa ya other finishing products kama wiring, lighting, seating, labor force na mfano wake. Vilevile bado soko ni tatizo kwa East na Central Afrika. Hatuna budi kuinua Per capita income yetu japo ifikie around $6000-12000 ili kuvutia viwanda vya luxury goods. Hata ukiangalia ukiacha mbali idadi ndogo ya magari yanayotumiwa, bado mengi ni used lakini unapojenga kiwanda maana yake dhana ya used inatoweka.Je unadhani tutamudu? Ni kweli tunaweza kuuza maeneo mengine lakini jiulize wapi? Kila maeneo yamekuwa covered vizuri na plats za magari zilizoko maeneo tofautitofauti kama India, China, Indonesia, Brazil, Ulaya na Amerika, hivyo kiwanda cha magari kwa Afrika kinatarajiwa kulisha zaidi wateja wa Afrika, je wapo wenye uwez wa kurudisha gharama za uwekezaji-think deeply and wisely.Uzalishaji unawezekana nchini iwapo kuna upatikanaji wa rasilimali ghafi nchini wa uhakika. Kwa sasa mie nadhani upatikani wa rasilimali ghafi nchini bado kwani umeme wenyewe wa kusuasua, etc. Kuhusu viwanda vya kuzalisha consumer goods it is not necessary tukazalisha vifaa kwa ajili ya watu nchini mwetu. We could also produce for export. Kumbuka East Africa assembly plant mfano hakuna vipo vichache. Honda kama kitajengwa kitakuwa kiwanda cha kwanza Africa masharika na kati na kusini (sijui kama kusini kipo au la). Sasa tunaweza tusinunue sisi wakanunua wakenya etc. Mbona sisi tunanunua BMW za kutoka South Africa au Samsung products kutoka Malaysia? Kwahiyo kiwanda kikijengwa nchini sio lazima sisi ndio tuwe wateja wanaweza kuwa wengine but sisi ni lazima tuwe wazalishaji na watu wetu wapate kazi na walipe kodi.
Wafungue na Kiwanda cha Tindikali pia
Naichukulia positive habari hii kwamba ina manufaa makubwa lakini bado nina mashaka ya kujua iwapo nchi yetu inaendeshwa na 'plans' au 'wishes'. Sina hakika kama Serikali huwa inatangaza mipango yake ya ushirikiano katika hatua gani? Maana inaweza ikawa inatangaza habari zake mwanzoni mwa nia ya kushirikiana halafu wakati wa majadiliano ya ushirikiano pande mbili zikashindana na hivyo 'wishes' kukomea hapo. Niko confused na program ya upanuaji na uendelezaji wa Bandari ya Dar, kila leo unaskia taarifa mpya za mbia wa kuindeleza kiasi kwamba unapigwa na butwaa which is which? Bagamoyo Mega Port tumeambiwa itakuwa tayari 2017, lakini hata ukiitafuta kwa sasa iko hatua gani za ujenzi wake bado kizunguzungu. Vilevile kwa reli ya kati, flying overs n,k. Kila mwaka unaskia feasibility studies. Ndio maana katika uzi huu kuna watu wameona kama ni "masuala ya popularity ya kisiasa" tu ili kuendelea kuwajenga kisaikolojia watanzania juu ya "Future we want". Popularity ni njia nzuri ya kufanikiwa kisiasa lakini huwa haina muda mrefu, jambo la msingi wasitutangazie "wishes" tunataka kusikia .....imeanza ujenzi wa Reli ya Kati, Bandari, nk" otherwise tunapotezeana muda kudebate vitu ambavyo imaginary au wishes.
Mungu Ibariki Tanzania
Imarisheni miundombinu ya gas na jengeni kiwanda cha kuyeyusha chuma kwanza kabla ya kuanza kufikiria viwanda vya auto-industry. Hakuna auto-industry, au building materials vitakavyoweza jengwa kama hakuna viwanda vikubwa vya uyeyushaji chuma. Hizi assembling plants kama zinazofanywa na wachina kwa pikipiki ni upuuzi mtupu.