Japan yaitangaza Tanzania kuwa Kitovu cha Uwekezaji, viwanda. Honda kujengwa nchini

Japan yaitangaza Tanzania kuwa Kitovu cha Uwekezaji, viwanda. Honda kujengwa nchini

sasa nchi inauzwa kwa 10% mikataba mibovu, tunawatoa wanachi kwenye maeneo yao tunawapa wawekezaji, nchi yetu tunakuwa wakimbizi.
Acheni mawazo potofu!, we kama una shamba unahisi utanyang'anywa tumia akili vizuri. Shamba umekua nalo tangu babu wa babu yako hujawahi kulima chochote humo! Unafurahia tu kuwa pori na umeridhika na kijumba chako cha majani. Mpaka lini?

Kwa kukusaidia mawazo: Nenda andikisha kampuni ya kilimo (itakugharimu si zaidi ya laki 5 kuandika nyaraka na kulipa ada), mashamba yako yamilikishe kampuni hiyo, halafu kaa chonjo kuuliza na kusikilizia hao wajapani wanaotaka kuja kulima pamba uwaambie walete mashine na utaalamu mshirikiane!

"Usipokubali kuliwa, kidogo huli"...JK
 
10/08/20130
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  • Japan yatangaza sera mpya kwa Tanzania Sasa Tanzania kuwa nchi lengwa ya Japan
  • Japan itasaidia Tanzania kuwa kitovu cha uwekezaji katika Afrika
  • Kushiriki maboresho Reli ya Kati
  • Kusaidia kupanua na kuboresha Bandari ya Dar Es Salaam
  • Viwanda vya Japan kujengwa nchini kikiwemo cha kutengeneza pikipiki za Honda
  • Ni matokeo ya Ziara ya Rais Kikwete Japan
JAPAN imeamua kuanzisha ushirikiano mkubwa zaidi na Tanzania ambako nchi hiyo itaifanya Tanzania kuwa nchi lengwa ya Japan na kuiwezesha kuwa kitovu cha biashara na uwekezaji katika Afrika kwa nia ya kuiwezesha kuwa na uchumi ulioimarika na wenye kuzalisha ajira nyingi kwa wananchi.

Uamuzi huo wa Japan ni matunda ya mazungumzo kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu wa Japan, Mheshimiwa Shinzo Abe yaliyofanyika Tokyo, Japan wakati Rais Kikwete alipotembelea nchi hiyo Juni, mwaka huu, 2013.

Uamuzi na msimamo mpya wa Japan umetangazwa rasmi leo, Jumamosi, Agosti 10, 2013 na Waziri wa
Uchumi, Biashara na Viwanda wa nchi hiyo, Mheshimiwa Toshimistu Motegi alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete, Ikulu, Dar Es Salaam.

Kwa upande wa Tanzania, mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anashughulika na Uwekezaji na Uwezeshaji Mheshimiwa Mary Nagu, Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Dkt. Abdallah Kigoda na Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe.

Waziri Motegi amemwambia Rais Kikwete kuwa ametumwa na Waziri Mkuu Abe kufuatilia mazungumzo kati yao na kutangaza rasmi kuwa Japan imeiteua Tanzania kuwa nchi lengwa na kitovu cha uwekezaji wa Japan katika Afrika Mashariki na katika Afrika kwa jumla.

Waziri Motegi pia amemwambia Rais Kikwete kuwa pia amekuja Tanzania kutoa taarifa kuwa Japan iko tayari kushiriki katika kuboresha na kuifanya ya kisasa zaidi Reli ya Kati kwa kujenga njia ya kimataifa badala ya njia nyembamba ya sasa. Amesema kuwa Japan itatuma wataalam wake kuangalia jinsi gani ya kuanza kazi hiyo ya uboreshaji wa Reli hiyo.

Aidha, Mheshimiwa Motegi ametangaza kuwa Japan itashiriki katika upanuzi na uboreshaji wa Bandari ya Dar Es Salaam kwa kuifanya ya kisasa zaidi.

Waziri Motegi amesema kuwa katika azma ya Japan ya kuifanya Tanzania nchi ya mfano katika Afrika katika uwekezaji na uchumi ulioimarisha, amekuja na kundi la wafanya biashara wa Japan ambao wanaendelea kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wa Tanzania kuona jinsi gani wanavyoweza kusaidiana katika kuwekeza katika uchumi wa Tanzania.

Waziri pia amesema kuwa moja ya malengo ya uamuzi huo wa Japan ni kuhakikisha kuwa bidhaa ambazo kwa sasa zinanunuliwa moja kwa moja kutoka Japan zitazalishwa hapa nchini katika viwanda ambavyo vitajengwa na makampuni ya Japan.

Kwa kuanzia amesema kuwa makampuni mawili ya Honda na Panasonic yamekubali kujenga viwanda nchini kimoja kwa ajili ya kutengeneza pikipiki za Honda hapa hapa nchini na kingine kwa ajili ya kutengeneza vifaa vya umeme.

“Huu ni mwanzo tu Mheshimiwa Rais kwa sababu kama nilivyosema kuwa tunataka Tanzania kuwa nchi mfano ya uwekezaji wa Japan katika eneo hili la dunia na namna hiyo kwa pamoja tutakuwa tumeshirikiana katika kuongeza ajira kwa wananchi wa Tanzania,” Mheshimiwa Motegi amemwambia Rais Kikwete.

Waziri huyo pia amesema kuwa baadhi ya makampuni ya Japan yana mipango ya kuwekeza katika kilimo, na hasa kilimo cha pamba, na kuanzisha viwanda vya nguo hapa hapa nchini.

Wakati wa mazungumzo yao mjini Tokyo, Rais Kikwete alimtaka Waziri Mkuu Abe kuwekeza zaidi katika Afrika akisisitiza kuwa Japan ni moja ya mataifa makubwa duniani ambayo yamefanikiwa kupata soko kubwa katika Afrika na hasa soko la magari.

Uamuzi huo wa Japan na ziara ya Mheshimiwa Motegi inakuja wiki na miezi michache baada ya Tanzania kuwa imepokea viongozi wa mataifa mengi yakiwemo mataifa makubwa ya Marekani na China na inathibitisha ni kiasi gani siasa na sera za Tanzania zinavyokubalika duniani.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

10 Agosti, 2013

Mi nasubiri mageuzi hapo Bandarini tu
 
katika viwanda vitakavyojengwa na Japan tanzania tuwekee mchanganuo wajapani wanachukua pasenti ngapi na sisi tunabaki na pasenti ngapi? VINGINEVYO NI KUUZIWA MBUSI KWENYE GUNIA
 
Namuonea huruma huyo waziri wa Japan kwa kushindwa kuelewa kuwa Kikwete ndio chanzo cha haya matatizo anayotaka kutatua...

Anaongelea kuboresha reli wakati mtoto wa Kikwete aitwaye Riziwani ndio kinara wa biashara ya usafirishaji mizigo kwa malori. Ubovu wa reli Ni mpango mkakati wa Kikwete kumtakatisha mwanaye na biashara ya malori ambayo pia mawaziri wengi pamoja na wahindi na waarabu rafiki zake Kikwete wanahusika.

Ukija kwenye upanuzi wa bandari mjapani hajaambiwa kuwa mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na wachina umekataza upanuzi wowote wa bandari ya Dar. Ngoja mjapani aje kikazi zaidi ndio atamjua Kikwete.

Labda atusaidie kupambana na biashara ya madawa ya kulevya...

Yeap! YOU NAIL IT Kiongozi! Hata mawaziri kutoka Ujerumani walikuja na kutoa ahadi kutengeneza upya reli ya kati, hatujaona hata taruma moja lililo letwa kuimarisha hiyo reli.

Inachekesha kuona kwamba IKULU inaendeleza siasa za AHADI wakati uchaguzi ulishaisha miaka mitatu iliyo pita. BURE kabisa hii serikali.
 
Hii thread imebeba ujumbe muhimu na mzito kwetu lakini kwa sababu haina chadema wala sheikh ponda ndani inaonekana ya hovyo

nimefurah sana mtazamo wako kaka-vijana hawajitambui, wao ni kupinga kila kitu. Upinzan unawanyima akili ya kufikir na sasa wanadhan ili uwe mpinzani unatakiwa kupinga killa kitu-wataathirika
ki akili na wataanza kujipinga hata wao wenyewe kwa yale wanayokubaliana-
 
Karibu sana Wajapani, Tanzania ni nchi ya amani, tushirikiane kwa faida ya wote.
TANZANIA MBELE, AFRIKA MASHARIKI INAFUATA.
tatizo si wageni njoo! tatizo mtanzania ananufaikaje, tuache mizaa kwenye maisha
 
Cha kushangaza habari imekaa kishabiki utadhabi hao wajepu wanakuja kuggawa zawadi. Hawa maCCM kamwe hawawezi kuleta maendeleo, nillitegemea hao jamaa kuonekana kama partners WA kibiashara ambapo wote tutanufaika but hapa inaonekana na Ni msaada. Ikumbukwe pia serikali ya Japan haijengi viwanda bali Ni makampuni ya kijapani, kinachotakiwa Ni kiwekwa mazingira bora ya uwekezaji ili kampuni kutoka sio Tu Japan hata Korea, Kenya,Saudia, Finland ikija inayakuta na kuwekeza kwa manufaa ya wote

Mkuu umenena ,CCM hawana mpango wowte wa kuhandle hizo issue, hawajui kuwa wajapanai wanapanua empire yao kushindana na wachina kwani mauzo ya toyo si unayaona?Hii ni nafasi ya Serikali kutumia hiyo fursa kuwashindanisha hawa mataifa, na kuweka mipango ili japani wakianza tengeneza reli basi wasituibie madini hadi wajilipe hapo hapo, na baada ya kujilipa waje igeuza kuwa miundo mbinu yao y akupanua soko, watanzania wajiandae kuwa na share, wajiandae kubana level ya uzalishaji, na kuiba hizo technologia, pia waje wengine tena wa nchi zingine zenye technologia nyingine.

Serikali isipojiandaa, hivi viwanda vitaajiri wageni wengi sana kwa kiasi cha kuleta matatizo mengine makubwa ya uhamiaji.
 
Mojawapo katika sera hii ya Wajapan ni upanuzi na uboreshaji wa bandari ya Dar es Salaam.

Katika mkataba wa Wachina wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo nasikia kuna kipengele ambacho kinazuia uendelezaji wa bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.

Hili limekaaje? Serikali itakuwa haijakiuka masharti ya mkataba wa Wachina?
 
Wakubwa wanainyemelea Tz kama SIMBA akiwa lindoni
 
Bila kujali itikadi ya chama katika hili mh kikwete anastahili pongezi Kama hawa jamaa watajenga viwanda itatusaidia sana hii mipango ya kuinua kilimo bila viwanda ni kudanganyana tu again I hope wajapan watatekeleza a hadi zao wakati mwingine ni vizuri tuweke tofauti za kisiasa pembeni tuangalie mambo mazuri ya nchi yetu
 
Hii thread imebeba ujumbe muhimu na mzito kwetu lakini kwa sababu haina chadema wala sheikh ponda ndani inaonekana ya hovyo
Naniyahovyo kwelikweli, nashangaa sana watanzani kufurahia jambo la hovyo kama hili. Sasa watanzania tusahau kabisa kuja kuwa na viwanda vyetu wenyewe! tutaendelea kuwatajirisha wenzetu huku sisi tukiimba wimbo wa umaskini milele na milele, amina.
 
Kwasasa pikipiki tuna import kutoka nje lakini matokeo ya SUNLG ya kuua kila siku kwa ajali na BOXER kwa kupora,kuua na kumwagia watu tindikali yanatumaliza sasa wakituletea hapa hapa basi tutegemee kiama.
 
Ndo michoro ya kushinda uchaguzi 2015, subiri mtaniambia!!! Magamba nouma, it will sound good kama hiki kiwanda kitajengwa pale Tabora au Simuyi na siyo kila kitu Dar.
 
Hili jambo ni jema sana kwa nchi ila nasikitika tuna viongozi wa ajabu nchini. Mwezi uliopita alikuja makamu Rais wa Samsung akitokea South Africa alikuja kwa lengo la kuangalia eneo zuri la kujenga kiwanda cha uzalishaji wa bidhaa za samsung nchini. Alipokelewa na afisa wa wizara wakaenda kumtupa bagamoyo bila ya maelezo yeyote yenye umuhimu kuhusu uwekezaji. Kisa ni tu hakuelewana na wakubwa wetu basi wakubwa wetu wakampotezea. Matokeo yake akapanda ndege na kwenda zake Kenya na kuishia zake South Korea. Hawa wawekezaji wanaweza kuwa na nia nzuri ya kuwekeza nchi ila na sisi tunalazimika kubadilika kifikra na kiakili na tuwe na uzalendo zaidi kwenye mambo yenye maslahi ya nchi.

Nashauri wahusika wafanye maandalizi kabambe kuwezesha wawekeze nchini ili tupate kutoa ajira kwa vijana wetu na taifa liende mbele. Tuache ubinafsi na tuwe wazalendo.
 
HAWA JAMAA TUKIWA NA SERA NZURI ZA UWEKEZAJI TUTAFAIDIKA SANA NAKUMBUKA MWAKA 2011 NILITEMBELEA TOYOTA PALE JAPANI NA PIA NIKAFANIKIWA KUTEMBELEA NEMC TOKYO JAMAA WANA TEKNLOJIA YA HALI YA JUU SANA !Big up President japo wengine wanasema eti unaenda kula bata!KEEP IT UP.
 
Hii thread imebeba ujumbe muhimu na mzito kwetu lakini kwa sababu haina chadema wala sheikh ponda ndani inaonekana ya hovyo

Haya ni mawazo yako. Nani kakuambia yaonekana hovyo? Watu wanasema kile wanachofikiri na kuona.
 
Back
Top Bottom