Japan yaitangaza Tanzania kuwa Kitovu cha Uwekezaji, viwanda. Honda kujengwa nchini

Japan yaitangaza Tanzania kuwa Kitovu cha Uwekezaji, viwanda. Honda kujengwa nchini

Kwakwel inasikitisha kuona viongoz wetu ni watu wasio na vision juu ya taifa letu.serikal ya ccm imekubal nchi yetu kuwa soko kwa mataifa yaliyoendelea.sasa eb angalia wajapan wanakuja kuleta viwanda vyao hapahapa,ikiwa na tafsir kwamba cc tuwe ngaz ya kuwafikia wateja wao wote wa A/mash. Na zaid sana ni kuua vijiviwanda vidogo tulivyonavyo kwan vitamezwa na hii multinational corporations. Serikal imeshindwa kuweka mikakat kwamb ifike mahal tz iwe na industrial base ya kutosha tena iwe completely ya kizalendo.wameua kiwanda chetu cha nyumbu kibaha na kuongeza juhud kununua magar ya luxury from japan...whats the fu***k is this?????inasikitisha kwa kwel kuona taifa lina viongoz mbulula
 
Kiwanda cha HONDA!!!!! Watanganyika ni kweli kwamba tumesahau ndoto ya Mwl. Nyerere ya kuwa na uwezo wa kutengeneza magari yetu wenyewe (Nyumbu!!) Sualahili lingekuwa na maana kwetu kama tunge pigania maliasili yetu ya mchuchuma na liganga ambayo tumeamua kuwapa wajomba zetu wa maendeleo. Mbona tunalidhalilisha taifa letu kwenye mambo ambayo tulikuwa na vision nayo mpaka tukapeleka watoto wetu nje kusomea mambo hayo! Tatizotulilo nalo ni kushindwa kuwa na mwendelezo wa masuala ya msingi kwa uchumi wa taifa letu na tumeruhusu kila ajaye kuja na ngojela zake ili aonekane naye ametende kumbe kulikuwa na mipango mkakati tangu kitambo iliyo kosa mwendelezaji na uboreshaji ili kufikia lengo. Tuachane na fikra za huwezi endelea mpaka wawekezaji acha waje lakini watukute tumeisha piga hatua fulani ili tuwe na sauti katika uchumi wetu. Kutembelewa na viongozi wakubwa duniani isiwe ni sifa bali tujiulize wao wamepata nini kwenye ziara hizi, napenda kutabiri matatizo makubwa katika taifa letu yataanzia kwenye rasilimali tusipo wadhibiti viongozi wetu kwenye kasi hii ya uwekezaji. Tukumbuke Mkapa kwenye ng'we yake ya mwisho ya utawala na uwekezaji usio na tija (rejea mwacheni mzee akapumzike) na utitili wa mikataba isiyo wazi kwenye ng'we hii ya mwisho ya utawala huu. TUPONGEZANE ILA TUKUBALI KUKOSOANA NA KUELIMISHANA KWANI NCHI HII NI YETU SOTE
 
mi nadhani tukatae misaada and see how we can handle our selves maana so far tuna madeni ya nje dola milioni elfu 11 and sumthin.. why dont we trade our mineral with several investments.. we to start to think forward sasa.. serkali iruhusu wananchi kutoa mawazo yao of how we can move forward as a country kiuchumi maana hali si hali kwa kweli.. na inasikitisha kwamba wakati wa mkapa walijitahidi na nchi waliichukua ikiwa taaban leo hii ambapo tunakusanya kodi nyingi zaidi lakini maisha yamekua magumu kweli.. inflation at 20% now..WHERE ARE WE HEADING ! we have to start rethinkin of the future of our sons and daughters.. so far its not looking good at all.
 
vitaanza lini kazi tusije furahia ikaja kuwa kama ile ya General Tyre ya Arusha.
 
Wakati nikipongeza hatua hii,lakini tukumbuke kuwa pikipiki ni technolijia ya chini sana,na kwa kufahamu uundwaji wake kutajengwa kiwanda cha ku-assemble hizi pikipiki.kitu ambacho wachina wanafanya KKoo muda mrefu tu.

Kama tungefanikiwa kuwashawishi wajapani waweke Auto assembly plant hapo ningempa maksi JK,kwani hii ingetufanya tuachane na biashara ya Magari used.na wajapani hawawezi kukubali makapi YAO wakose pa kuyatupa.

Ushauri kwa serikali.waombe wachina waje kujenga assembly plants za Magari hapa Tanzania kwa ajili ya masoko ya Afrika.in 5 years Toyota watajenga kiwanda.hiki cha Honda tuwashukuru toyo na SanLG kwani ndio sababu hasa ya hawa jamaa kuja.

Kingine si vibaya tukaomba viwanda kwa ajili ya primary resources,na sio secondary ones.kwa mfano,kiwanda na kutengeneza circuit za redio na television Kina maana kubwa kwetu kuliko kiwanda cha redio,kwa maana hii tuombe cluster ya viwanda na sio standalone units ambazo zinatumika Kama political gestures with little meaning.

Imagine dangote angeleta kiwanda cha matofali.
 
Good Move, Hawa super Giant wa Dunia wote wanaigombania Tanzania kama mpira wa kona, hofu yangu ni sera mbovu za CCM ikichagizwa na mifumo yao mibovu isiyokuwa ya uwazi utakavyoendelea kuididimiza nchi yetu... Wageni waje weenyeji waumie sasa iwe mwisho jamani...
Wao wanatuhitaji kuliko sisi tunavyowahitaji sijui kwanini haiwaingii akilini hawa mbulula wa CCM...Tukiweka kila kitu kwa uwazi Tanzania inaweza kuendelea ndani ya miaka mitano tu na si hizi takwimu za akina Ndulu za uchumi kukua kwa 1% wakati tuna kila kitu na vingine tumepewa sisi tu kama zawadi kutoka kwa mwenyeezi mungu...


Nilikuwa nafuatilia michango mingi kuhusiana na habari hii. Angalau wewe ndio umefanya uchambuzi wenye tija. Wengine ni lawama, matusi, kebehi, mizaha. Watanzania inatupasa tubadilike sana katika kutazama mambo la sivyo tutasukumemwa pembeni ya mkondo wa maendeleo ya katika zama hizi.
 
They say ''This is time for Africa'' But I think they mean Tanzania.....It started with China....America -US now Japan! wake up Tanzania ni wakati wa kupiga deal sasa...strike deal fellows, it is our time!
 
10/08/20130
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  • Japan yatangaza sera mpya kwa Tanzania Sasa Tanzania kuwa nchi lengwa ya Japan
  • Japan itasaidia Tanzania kuwa kitovu cha uwekezaji katika Afrika
  • Kushiriki maboresho Reli ya Kati
  • Kusaidia kupanua na kuboresha Bandari ya Dar Es Salaam
  • Viwanda vya Japan kujengwa nchini kikiwemo cha kutengeneza pikipiki za Honda
  • Ni matokeo ya Ziara ya Rais Kikwete Japan
JAPAN imeamua kuanzisha ushirikiano mkubwa zaidi na Tanzania ambako nchi hiyo itaifanya Tanzania kuwa nchi lengwa ya Japan na kuiwezesha kuwa kitovu cha biashara na uwekezaji katika Afrika kwa nia ya kuiwezesha kuwa na uchumi ulioimarika na wenye kuzalisha ajira nyingi kwa wananchi.

Uamuzi huo wa Japan ni matunda ya mazungumzo kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu wa Japan, Mheshimiwa Shinzo Abe yaliyofanyika Tokyo, Japan wakati Rais Kikwete alipotembelea nchi hiyo Juni, mwaka huu, 2013.

Uamuzi na msimamo mpya wa Japan umetangazwa rasmi leo, Jumamosi, Agosti 10, 2013 na Waziri wa
Uchumi, Biashara na Viwanda wa nchi hiyo, Mheshimiwa Toshimistu Motegi alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete, Ikulu, Dar Es Salaam.

Kwa upande wa Tanzania, mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anashughulika na Uwekezaji na Uwezeshaji Mheshimiwa Mary Nagu, Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Dkt. Abdallah Kigoda na Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe.

Waziri Motegi amemwambia Rais Kikwete kuwa ametumwa na Waziri Mkuu Abe kufuatilia mazungumzo kati yao na kutangaza rasmi kuwa Japan imeiteua Tanzania kuwa nchi lengwa na kitovu cha uwekezaji wa Japan katika Afrika Mashariki na katika Afrika kwa jumla.

Waziri Motegi pia amemwambia Rais Kikwete kuwa pia amekuja Tanzania kutoa taarifa kuwa Japan iko tayari kushiriki katika kuboresha na kuifanya ya kisasa zaidi Reli ya Kati kwa kujenga njia ya kimataifa badala ya njia nyembamba ya sasa. Amesema kuwa Japan itatuma wataalam wake kuangalia jinsi gani ya kuanza kazi hiyo ya uboreshaji wa Reli hiyo.

Aidha, Mheshimiwa Motegi ametangaza kuwa Japan itashiriki katika upanuzi na uboreshaji wa Bandari ya Dar Es Salaam kwa kuifanya ya kisasa zaidi.

Waziri Motegi amesema kuwa katika azma ya Japan ya kuifanya Tanzania nchi ya mfano katika Afrika katika uwekezaji na uchumi ulioimarisha, amekuja na kundi la wafanya biashara wa Japan ambao wanaendelea kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wa Tanzania kuona jinsi gani wanavyoweza kusaidiana katika kuwekeza katika uchumi wa Tanzania.

Waziri pia amesema kuwa moja ya malengo ya uamuzi huo wa Japan ni kuhakikisha kuwa bidhaa ambazo kwa sasa zinanunuliwa moja kwa moja kutoka Japan zitazalishwa hapa nchini katika viwanda ambavyo vitajengwa na makampuni ya Japan.

Kwa kuanzia amesema kuwa makampuni mawili ya Honda na Panasonic yamekubali kujenga viwanda nchini kimoja kwa ajili ya kutengeneza pikipiki za Honda hapa hapa nchini na kingine kwa ajili ya kutengeneza vifaa vya umeme.

“Huu ni mwanzo tu Mheshimiwa Rais kwa sababu kama nilivyosema kuwa tunataka Tanzania kuwa nchi mfano ya uwekezaji wa Japan katika eneo hili la dunia na namna hiyo kwa pamoja tutakuwa tumeshirikiana katika kuongeza ajira kwa wananchi wa Tanzania,” Mheshimiwa Motegi amemwambia Rais Kikwete.

Waziri huyo pia amesema kuwa baadhi ya makampuni ya Japan yana mipango ya kuwekeza katika kilimo, na hasa kilimo cha pamba, na kuanzisha viwanda vya nguo hapa hapa nchini.

Wakati wa mazungumzo yao mjini Tokyo, Rais Kikwete alimtaka Waziri Mkuu Abe kuwekeza zaidi katika Afrika akisisitiza kuwa Japan ni moja ya mataifa makubwa duniani ambayo yamefanikiwa kupata soko kubwa katika Afrika na hasa soko la magari.

Uamuzi huo wa Japan na ziara ya Mheshimiwa Motegi inakuja wiki na miezi michache baada ya Tanzania kuwa imepokea viongozi wa mataifa mengi yakiwemo mataifa makubwa ya Marekani na China na inathibitisha ni kiasi gani siasa na sera za Tanzania zinavyokubalika duniani.


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.


10 Agosti, 2013

Nyie watu wa Ikulu wacheni kuiaibisha nchi. Huwezi ukasema hayo ni matokeo ya ziara ya JK, hivyo ndivyo WJP wamewaambia au mmeangalia kwa kina kwa nini JPN wameamua kufanya hivyo. Cheap spin.
 
kwa hili naunga mkono hoja 100%,tunaoimba Japan ifanye haraka kuja kuwekeza nchi iwe vijana wetu wapate ajira na uchumi wetu uzidi kukua
 
Nilikuwa nafuatilia michango mingi kuhusiana na habari hii. Angalau wewe ndio umefanya uchambuzi wenye tija. Wengine ni lawama, matusi, kebehi, mizaha. Watanzania inatupasa tubadilike sana katika kutazama mambo la sivyo tutasukumemwa pembeni ya mkondo wa maendeleo ya katika zama hizi.
Pamoja sana Mkuu, ila usishangae sana aina ya michango inayotolewa humu, hii ni reflection ya jamii yetu! watu wamekata tamaa, hawana uelewa mpana wa masuala ya uchumi wa kidunia, hawajui game linalochezwa duniani...elimu inayotolewa kwa watanzania inahitaji maboresho makubwa sana ... all in all JF ni zaidi ya darasa kwa wengi wetu, naamini hata Mkuu wa kaya huwa anapita hapa kupata data za uhakika.... Ni wakati muafaka sasa bila ya kujali itikadi zetu imani zetu tuanzishe the so called National Brain; hawa watakuwa watu mahsusi watakao kuwa wanafikiri na kuchambua kwa niaba ya Taifa, watu hawa wanatakiwa walelewe vizuri sana...kwa wenzetu huwa wanawatumia watu wao kama malobbiest! Hakuna waziri wa kibongo anaeweza kucheza game la hawa majamaa, ndo maana mikataba mingi imefungwa na warembo blondes ...
 
inashangaza sana kuona kila jambo linalotokea watu wanalichukulia negetively, hivi swala hapa ni kikwete au maslahi kwa nchi, ni ulitaka rahisi asitafute wawekezaji, au bado mna mawazo ya nyerere kwamba tuache raslimali kwa kua haziozi, soo what? jaribuni kuwa positive angalau kidogo achani kuwaza giza kila wakati jaribuni kuiona nuru! kwa mtindo huu hamtakaa mzione fursa hata kama zitakua sebuleni kwenu! jipange acha kupiga mayowe..period!



Mkuu inshangaza kuona wana CCM leo hamtaki hata kumheshimu hayati Mwalimu Nyerere. Kumbuka Mwalimu alijua miongoni mwa wasomi wachache wa mwanzo katika ngazi ya dr, na alikuwa mtaalam wa uchumi vile vile. Kaongoza nchi wakati wa kipindi kigumu cha siasa duniani. Vita baridi ilifanya nchi nyingi za Africa kupinduliwa na baadhi ya viongozi kuuwawa. Mapambano ya ukombozi wa nchi zilizo kuwa zikitawaliwa, yalipambamoto. Hivyo maendeleo alio fanikisha hayati Mwalimu ni makubwa katika mazingira magumu. Priorities kubwa kwa wakati wake zilikuwa kumkomboa mwananchi toka kwenye ukandamizaji wa mkabaila na wanyonyaji wa ndani na nnje ya nchi, elimu ili kupata wtaalam, afya ujenzi wa hospitali, maji safi, barabara nk, kusaidia mapambano ya ukombozi wa nchi zilizokuwa zikitawaliwa. Alijua bila ya matayarisho yakutosha huwezi kukurupuka kwenye uchimbaji wa madini na maliasili nyingine, hiyo ingenufaisha mataifa ya nje tu ambayo yangewekeza. Mfano Congo waliishia kupinduana na Patrice Lumumba kuuwawa, maendeleo yao mpaka leo yana sua sua, pamoja kwamba uchimbaji wa mali asili zao ulianza zamani sana.
 
inashangaza sana kuona kila jambo linalotokea watu wanalichukulia negetively, hivi swala hapa ni kikwete au maslahi kwa nchi, ni ulitaka rahisi asitafute wawekezaji, au bado mna mawazo ya nyerere kwamba tuache raslimali kwa kua haziozi, soo what? jaribuni kuwa positive angalau kidogo achani kuwaza giza kila wakati jaribuni kuiona nuru! kwa mtindo huu hamtakaa mzione fursa hata kama zitakua sebuleni kwenu! jipange acha kupiga mayowe..period!



Mkuu inshangaza kuona wana CCM leo hamtaki hata kumheshimu hayati Mwalimu Nyerere. Kumbuka Mwalimu alijua miongoni mwa wasomi wachache wa mwanzo katika ngazi ya dr, na alikuwa mtaalam wa uchumi vile vile. Kaongoza nchi wakati wa kipindi kigumu cha siasa duniani. Vita baridi ilifanya nchi nyingi za Africa kupinduliwa na baadhi ya viongozi kuuwawa. Mapambano ya ukombozi wa nchi zilizo kuwa zikitawaliwa, yalipambamoto. Hivyo maendeleo alio fanikisha hayati Mwalimu ni makubwa katika mazingira magumu. Priorities kubwa kwa wakati wake zilikuwa kumkomboa mwananchi toka kwenye ukandamizaji wa mkabaila na wanyonyaji wa ndani na nnje ya nchi, elimu ili kupata wtaalam, afya ujenzi wa hospitali, maji safi, barabara nk, kusaidia mapambano ya ukombozi wa nchi zilizokuwa zikitawaliwa. Alijua bila ya matayarisho yakutosha huwezi kukurupuka kwenye uchimbaji wa madini na maliasili nyingine, hiyo ingenufaisha mataifa ya nje tu ambayo yangewekeza. Mfano Congo waliishia kupinduana na Patrice Lumumba kuuwawa, maendeleo yao mpaka leo yana sua sua, pamoja kwamba uchimbaji wa mali asili zao ulianza zamani sana.
 
Niseme tu wazi kua maendeleo ni jambo Zuri sn katika hii Dunia! Ila huo uwekezaji ufate haki na uangalie maslahi ya watu wote na atimae taifa na wannanchi wote wapate kunufaika na huo uwekezaji! Mungu ibariki Tanzania
 
Sipati picha hawa rwanda,uganda na kenya wanavyozidi kuchanganyikiwa
 
Tumeshawahi kupita "BARABARA" wakati wa "MIGODI","GAS" na vingine vingi,kwa nini tuamini sasa hivi Tanzania itakuwa DUBAI.
 
Tumeshawahi kupita "BARABARA" hii wakati wa "ALMASI,DHAHABU,GAS" na vingine vingi,kwa nini tuamini sasa hivi Tanzania itakuwa DUBAI.
 
Back
Top Bottom