Japan yaitangaza Tanzania kuwa Kitovu cha Uwekezaji, viwanda. Honda kujengwa nchini

Tumeshawahi kupita "BARABARA" hii wakati wa "ALMASI,DHAHABU,GAS" na vingine vingi,kwa nini tuamini sasa hivi Tanzania itakuwa DUBAI.
Dubai liyosheheni masnipers na wamwaga tindikali!!!?.
Ngoja tusubiri na kuona nchi inayoendeleza na nchi nyingine baada ya yenyewe kushindwa kujiendeleza, nadhani tutakuwa wa kwanza na wa aina yake!
 
Uwekezaji Nchini Tz unahitaji Sayansi kubwa sana kwani Ubinafusishaji uliofanyika awamu ya tatu umepelekea baadhi ya Viwanda kufa na baadhi vipo taabani hivyo Kama tumeshindwa kuviendeleza viwanda vilivyokuwepo Tokea awamu ya kwanza iweje kwa hivyo viwanda vipya? Tatizo kubwa wanalopata Wawekezaji ni Ufisadi hususani ikitokea mwekezaji akatoa ajila kubwa kwa Wazawa ambapo hutengeneza umoja na kubuni mbinu ya kujinufaisha Binafsi huku Viwanda vikiyumba na kufirisika. Swali je?hao Wajapani wa Honda watakuja na uongozi full na Watafunga CCTV kila kona kwenye Viwanda vyao? Hii ni tahadhali kwani inafahamika moja ya changamoto kubwa kwenye uwekezaji ni udokozi na hata mwekezaji akiweka CCTV kisha akamweka mzawa pale lazima afanye manuva Vinginevyo CCTV akae Mzungu na asiwe anajulikana Tunawakaribisha Wajapani na wengineo wote Duniani waje wawekeze kokote lakini uwekezaji wa uhakika isije ikawa kama TAMKO na Scania pale kibaha.japani jipangeni vizuri leteni hata viwanda vya magari lakini mzingatie changamoto za uwekezaji Tz kwani kuna Vilema pendwa vingi sana
 
tumeambiwa tutakachopata watanzania ila bado hamjatuambia hao wajapan watachukua nini in return!

Tazama documentary hii hutadanganywa tena na vibaraka wa wakoloni
https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/503251-documentary-ya-aljazeera-inayofichua-utumwa-wa-viongozi-wa-nchi-za-kiafrica.html
 
https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/503251-documentary-ya-aljazeera-inayofichua-utumwa-wa-viongozi-wa-nchi-za-kiafrica.html
 
Kwani hukusikia Mkulu anayoyaongea kila mara kuwa hii nchi ilikuwa inachezewa sana!
 
Wajapan walie tu maana Sehemu zote za kujengea viwanda BAKHRESA kesha pewa bure.. Inabidi wajapani waingie mkataba na Bakhresa wakitaka ardhi
 
Huu mwaka wa tatu sasa tangu mtuhabarishe kuhusu hii kitu. Naomba kujua kiwanda hiko kwa sasa hapa bongo kipo maeneo gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…