Kuna makabila/jamii yameingiliana EA.
Mfano wajaluo wapo , Kenya [Kisumu,Nyanza,Bondo ] , Tanzania wapo Shirati ] Uganda wapo Bunyoro.
Wamasai wapo Tanzania [Arusha, Longido, Ngorongoro ] Kenya wapo [Narok , Nairobi, Naivasha ] hata Nairobi ni jina la kimasai maana yake mji/sehemu yenye baridi.
Wasomali wapo Somali na Kenya , Kenya wapo kwa wingi Garissa, Wajir na Nairobi na Somalia wapo katika migawanyiko ya kikoo/ukoo.
Wakurya wapo [Tarime,Serengeti na Shirati ]kwa Tanzania na Kenya wanaitwa "wakuria" wapo kwa wingi Kisii na Migori hivyo unakuta majina kama Chacha, Maraga, Mwita utayakuta Tanzania na Kenya pia.