Sean Paul
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 1,330
- 3,289
Kuyatilia shaka ni muhimu, watu wengi wanahamia kwa njia za panya toka nchi jirani. Nilisoma na mtu anaitwa Niyonziza, mwingine nilikutana naye mitaani jina lake Amatus Ndayishimye. Kiasili, haya si majina ya Kitanzania, ni Warundi.Point yako imesimama kwa kunyooka. Kama hivyo ndivyo ingawa inahitaji uthibitisho wa asili ya mtu, kwa nini majina ya asili kama hayo ya kijaluo kwa watu wa mikoa ya magharibi hasa Kigoma yanatiliwa shaka na idara ya uhamiaji?
Kuna wakati nilidate na bint mdogo alikua hata haongei Kiswahili vizuri. Siku ya kwanza kukutana naye tulikua na gari sehemu, nikamwita akaja. Tulipokuwa tunapiga story nikagundua hakuwa Mtanzania......mimi na yule mwezangu aliyekuwa dereva tukaanza kumhoji. Kwa kuonekano wetu, akaanza kutuogopa. Tulipomuuliza amesoma wapi shule ya msingi, akajichanganya akataja mkoa, wilaya na kata ambayo yule dereva ndio kwao. Tukagundua anatuongopea, ikabidi atueleze ukweli kuwa anaishi na dada yake ambaye yupo huku Tz miaka mingi ila kwao ni Burundi. Hana kibali wala chochote yupo yupo tu, na hapo ni Mwanza. Akikaa miaka 5 huyu si anapata hadi passport yetu.
Bint kanyooka Mtutsi mzuri sana. Nikachukua namba.
So we acha tu uhamiaji wafanye kazi yao.