Japo anaonekana mtu wa kawaida tu ndani ya CCM, Humphrey Polepole sio mtu wa kawaida!, He is extra ordinary very powerful!

Japo anaonekana mtu wa kawaida tu ndani ya CCM, Humphrey Polepole sio mtu wa kawaida!, He is extra ordinary very powerful!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
CCM ndio chama tawala na kwa Tanzania, tukubali tukatae, CCM ni chama dola. Tunapoelekea uchaguzi Mkuu wa rais na wabunge October 25, mgombea akiishapitishwa kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM, then huyo ndio tayari ni mshindi, zoezi la uchaguzi ni kukamilisha tuu taratibu za uchaguzi ili tuu kuhalalisha.

Sasa tunapoelekea kwenye uchaguzi, mambo yote ni CCM na ngoma yote ni jinsi ya kupata uteuzi kupitia CCM, ili mtu uteuliwe kuwa mgombea wa CCM ni lazima moja ya mambo matano haya yakuhusu zaidi ya kuwa na sifa na vigezo...
  1. Uwe na good track record ya utendaji uliotukuka
  2. Uonyeshe uwezo wa kukikisaidia chama na kuisaidia nchi
  3. Uonyeshe uwezo wa kujenga hoja na kujieleza ili kundi CCM
  4. Uwe na powerful godfather atakaye ku back up kwenye vikao vya uteuzi
  5. Uwe na kisu kujali, hivyo kila penye uzia wewe unapenyeza rupia.
Sasa ndani ya CCM kuna viongozi wengi wenye nyadhifa, madaraka na mamlaka, kwenye power hierarchy ya ukubwa, mamlaka, madaraka na powers kutokea juu iko kama ifuatavyo
  1. Mweyekiti,
  2. M/Mwenyekiti Bara,
  3. M/Mwenyekiti Zanzibar
  4. Katibu Mkuu,
  5. Naibu Katibu Mkuu Bara
  6. Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
  7. Katibu Mwenezi
  8. Wajumbe wa Secretariat
  9. Wajumbe wa CC
  10. Wajumbe wa NEC
  11. Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa.
Hiyo ndio power axis ya CCM

Sasa kati ya No.1-7, powers ziko vested kwa individuals, ila nimetokea tuu kati ya hao watu 7 ambao ndio power axis ya CCM, miongoni mwao kuna watu wana real powers na vested powers, real powers ni wale wenye nguvu from within, hizi powers za mtu zilizo ndani yake, na vested powers ni powers za mtu kutokana na nafasi yake, cheo chake au wadhifa wake, hivyo unakuwa mtu ana cheo kikubwa chenye madaraka na mamlaka lakini hana real powers from within.

Ndani ya wale top 7 wa CCM interns of vyeo, wadhifa na madaraka, Humphrey Polepole ndio wa mwisho!, but in terms of powers from within, kwa my opinion, Humphrey Polepole ni miongoni mwa the top 3 most powerful people ndani ya CCM kwa powers from within!.

Japo Humphrey Polepole ni very simple, mnyenyekevu, very humble and down to earth na akiongea, anaonekana very weak kutokana na kuwa na soft spoken voice, huwa anaongea kwa sauti ya chini bila ku shout kama sauti ya unyonge vile, but amini usiamini, this is where real powers of persuasion lies!.

Namna pekee ya kujua where real powers lies, lazima uwe na jicho la tatu la kumsikiliza mtu, na kuweza kusimsikia in between the lines, yaani mtu anapoongea Luna mambo anayaongea na katika kuongea huko, kuna mambo anakuwa anayajua lakini hajayaongea, hivyo kupitia jicho la tatu na sikio la tatu, utaisikia sauti ndani yako, " the voices from within" ambayo itakuambia yale ambayo mzungumzaji huyo anayajua lakini hajayasema.

Mimi nilimsikiliza Humphrey Polepole hapa katika tukio hili
View: https://youtu.be/SYJjy4zg7ss

Nilipomsikiliza ndipo nikabaini this is very Powerful person.

Kuhusu Polepole kuwa Powerful haina mashaka, bali nilibaki na maswali kuhusu what is the source of his powers.

Leo kupitia kipindi cha Sunday Worship kinachorushwa live na Wasafi TV, kila siku za Jumapili asubuhi, Jumapili ya leo, Mgeni mwalikwa ni Humphrey Polepole, kiukweli baada ya kumsikiliza leo Humphrey Polepole, ndipo sasa nimeelewa source of his powers!.

Kama kuna mtu anataka ku lobby chochote kutoka CCM na serikalini, then the man to look for is Humphrey Polepole.

Hivyo siku ile nilipopandisha bandiko hili

Nikawaambia kuwa namtafuta Humphrey Polepole, nadhani baada ya bandiko hili, sasa ndio mtaelewa ni kwanini namtafuta Polepole!.
Bado namtafuta, nasubiria Corona itangazwe rasmi kuwa imekwisha Tanzania, hivyo kazi ya kumtafuta Polepole iendelee.

Nawatakia Jumapili Njema.

Paskali.
 
Polepole huyu aliebadilishwa msimamo wake na njaa.

Nikimkumbuka wakati wa ile Rasimu ya Katiba ya Warioba alivyokuwa anaipigia debe, halafu alivyokuja kubadilika ghafla, sina hamu nae.

Endelea kumtafuta tu; sikushangai, kwasababu hata wewe mwenyewe unaonekana ulishapotea...!!
 
Ulichosema ni kweli Polepole ni mtu mzito kuliko tunavyofikiria, nimewahi kwenda ofisini kwake Kwa ishu za hapa na pale, jamaa ana wasaidizi wasiopungua watano rasmi.

Kuanzia usalama, dereva, waandishi anafanya mawasiliano na watu wote wakubwa wa serikali kuanzia Rais, Wabunge, Wakuu wa Mikoa na vyombo vya usalama.

Anaweza akaamua Pascal leo ulale kituoni ukalala, usichukulie poa huyu komrade, tokea nimeenda ofisini kwake na kufanya naye mazungumzo nimetambua jamaa ana nguvu sana ndani ya serikali na chama, usichukulie poa. Mawasiliano ya Moja Kwa Moja na wakuu wengi anayo
 
Binafsi nimeanza kumfatilia Polepole kwa ukaribu wakati wa mchakato wa mabadiliko ya katiba mpya kuna vitu kadhaa nimeviona ndani yake ukiachilia hicho cheo alichonacho kwa sasa, katika hali ya kawaida huwezi kuelewa ukiweka ushabiki wa kivyama mbele.

Ana nguvu ya ushawishi na hoja, nafikiri ndiyo sababu iliyomfanya kupanda madaraja kiuongozi kwa haraka haraka.
 
Back
Top Bottom