Paskali uko sahihi sana na kweli huyo Polepole ana nguvu sana ndani ya CCM. Sababu hasa ya Polepole kuwa na nguvu ndani ya CCM
1. Polepole ni mtu aliyesoma mambo ya ccm na kuyakariri vyema hasa sheria na miongozo ya chama.
2. Polepole hakuwa sehemu ya wanachama wezi kwani hakuwa kuwa kwenye sehemu ya ulaji ndani ya chama au serikali kabla ya Magufuli, hivyo kuwa katika kundi la wanaccm wachache wasio na kashfa.
3. Magufuli hajui mambo mengi ya ccm, hivyo anamuamini na kumtumia zaidi Polepole kwenye taratibu zote za chama.
4. Magufuli ni mtu anayependa kunyenyekewa na kusujudiwa, na Polepole anamnyenyekea na kumsujudia Magufuli kuliko hata afanyavyo kwa Mungu. Hali hiyo inamfanya Magufuli kumkubali zaidi Polepole kuliko mwanaCCM yoyote, aliye chamani au serikalini.
Kwa sababu hizi hapo juu, Polepole ndio msiri na mshauri mkubwa wa CCM kuliko mwanaCCM yoyote. Hapo ndio nguvu zote za Polepole zilipo. Iwapo ukielewana na Polepole, basi wewe unaweza kupata cheo chochote ndani ya nchi hii.