Japo anaonekana mtu wa kawaida tu ndani ya CCM, Humphrey Polepole sio mtu wa kawaida!, He is extra ordinary very powerful!

Japo anaonekana mtu wa kawaida tu ndani ya CCM, Humphrey Polepole sio mtu wa kawaida!, He is extra ordinary very powerful!

basi itabidi kangilugola aione hii post ili abadili wa kumsifu...badala ya kumsifu jiwe aanze kumsifu hamph

Sio hata kumsifu maana tayari Kange Lugola anafahamika na Magufuli. Anachotakiwa ni kuongea kiutuuzima na Polepole. Huu ndio muda wa Polepole naye kutoka kimaisha kama kina Makonda, Riz one, Mwigulu nk.
 
Sina muda wa kumfuatilia mtu ambaye ninamfahamu na nimefanya naye kazi kwa ukaribu tena ofisi moja, namfahamu sana hana lolote zaidi ya kujikomba kisa njaa
Mkuu sipo kwaajili ya mnyukano wala ubishani, jaribu kumtazama kwa jicho la tatu huyu jamaa Kuna vitu utaviona ukishindwa kufanya hivyo uachie muda utatoa majibu mazuri siku za mbele, hata usijihangaishe kwendelea kuni-quote sitajujibu chochote.
 
Kuna siku nilimsikia clouds kama wiki na nusu iliyopita,nikajiridhisha huyu mtu ana kitu kizito kichwani.

Namna alivyokuwa anaulizwa maswali na kujibu,namna anavyopangilia majibu na kuweka akiba ya maneno,nikajisemea hata labda alijua anakwenda kuulizwa kitu gani kabla hajatoka kwake asubuhi.

Tumezoea kumuita chakubanga,kwa maana ya mpiga domo kwa kazi hiyo,ila kosa kubwa tunalofanya kama watu wa upande B,ni kumchukulia kwa urahisi rahisi tu,mtu kama pole pole.
 
Kama CDM ingekuwa na democrasia ndani yake,chama kisingepoteza dira kama ilivyo leo.

Kosa kubwa tunalofanya ni kuwa wa kwanza kuona ya nje na kufukia moshi ndani ya chama,wakati ccm haifanyi jambo lolote kwa uzito wake bali kwa madhara yake.
 
Kama CDM ingekuwa na democrasia ndani yake,chama kisingepoteza dira kama ilivyo leo.

Kosa kubwa tunalofanya ni kuwa wa kwanza kuona ya nje na kufukia moshi ndani ya chama,wakati ccm haifanyi jambo lolote kwa uzito wake bali kwa madhara yake.

Kuna tofauti ya chama kupoteza dira, na kufanyiwa hujuma na rais aliye madarakani ili ionekane imepoteza dira. Tuna uwezo mzuri wa kujua ipi ni kupoteza dira, na hujuma za kisiasa boss.
 
Ulichoandika kina ukweli. Kama mwana NEC tu anaweza kumkoromea na kumwamisha RPC je, huyu Polepole?.
Nimejibu kulingana na cheo chake cha wazi tunachokijua wote

Mnapoambiwa ccm ni chama tawala,kauli hii huwa haijaacha chenji mfukoni.

Polisi wanakuwa wa kwanza kuonekana waathirika sababu ni watumishi live,ila hali iko hivyo kila unapopajua.wako chini huko na ule mhimili uliojichimbia zaidi.

Ndio maana huwezi kuona mtu anawaletea jeuri maana kukicha atapoteza haki zake,ikiwezekana atapotea na njia.
 
Na Ana nguvu zaidi kwenye teuzi mbalimbali so umeanza vyema wkt huu hatakuacha kabisa mkuu
 
Sio hata kumsifu maana tayari Kange Lugola anafahamika na Magufuli. Anachotakiwa ni kuongea kiutuuzima na Polepole. Huu ndio muda wa Polepole naye kutoka kimaisha kama kina Makonda, Riz one, Mwigulu nk.
Hata pia upande wa pili ni wakati sahihi sasa wale wanaotaka kupata Vm ndani ya CDM wakaiongea vizuri na Joyce John Mukya maana yuko Karibu sana MZEE wa KONYAGI KUBWA.
 
Kuna tofauti ya chama kupoteza dira, na kufanyiwa hujuma na rais aliye madarakani ili ionekane imepoteza dira. Tuna uwezo mzuri wa kujua ipi ni kupoteza dira, na hujuma za kisiasa boss.

Sijui kama ni mahali sahihi hapa,lakini wacha nikuulize swali dogo.
Yupo mtu alitegemea safari hiyo itakiwa ni rahisi milele!!!,kama yupo huyo ndiye ameiponza chedema.

Thats why,tulipiga kelele siku za mwanzo kabisa,kwamba tuna mengi ya kusifu rais kuliko kumsimanga,maana inawezekana hilo likachukuliwa kama uchochezi.
Saddly watu kumbe wanafanya biashara,sio mikakati ya kuisaidia nchi.
 
Yes, Polepole ni very powerful. Anaweza kuongea na yeyote dakika yoyote. Lakini pia yuko vizuri upstairs
Mkuu Ukiwa mnyenyekevu, utaonywa na utasahihishwa makosa yako, na hivyo utasaidiwa kuwa mtu mwema zaidi. Ukiwa mnyenyekevu utafikika na wengi na utakuwa msaada kwa watu/kimbilio la watu. Zaidi sana, ukiwa mnyenyekevu utapendwa na watu wote kama alivyo Ndugu Polepole.
 
"CCM ndio chama tawala na kwa Tanzania, tukubali tukatae, CCM ni chama dola.

Tunapoelekea uchaguzi Mkuu wa rais na wabunge October 25, mgombea akiishapitishwa kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM, then huyo ndio tayari ni mshindi, zoezi la uchaguzi ni kukamilisha tuu taratibu za uchaguzi ili tuu kuhalalisha." pascall mayalla


Pascal Mayalla, maneno ulioandika ni kitendo cha kuvunja katiba na sheria za NEC. Nyinyi ma CCM huwa hamujitambui munapo vunja sheria au katiba ya nchi.

Kampeni hazijaanza lakini mme-declare ushindi. Kwa ufupi ni kuwa mikakati ya kuiba kura za walalahoi imetimia.

Na kama huyu Pascali atakuwa mbunge na utumbo alioandika hapa JF basi nasikitika kuwa Tanzania itafilisika na itakuwa hatarini. Pascali ndio aliyekuja na wazo la kujenga bridge kilomita 40 toka Dar es Salaam hadi unguja na kujidai kuwa uwezo wanao.

Wazanzibari walimpinga vilivo sababu ya msimamo wake. Watu wa aina hii wataharakisha kuuvunja muungano. Anamuabudu Polepole kama mungu wake.

Masikitiko makubwa kwani Polepole ni katika watu wasio aminika kabisa na ndio maana baada ya kurudi kutoka Pemba kuutizama uhai wa chama Polepole ameingia mitini.

Amefeli kukisaidia chama kuvuna wanachama wapya licha jitihada ya kuiuwa CUF.
 
Back
Top Bottom