Wanabodi,
Bunge letu tukufu, limeridhia makubaliano ya IGA kati ya Serikali ya UAE na Tanzania, kampuni ya DP World ya Mwarabu wa Dubai, kutuendeshea Bandari zetu.
Kuna watu wana support hatua hiyo kwa hoja za msingi, kuwa DP World ni kampuni kubwa na ina uwezo mkubwa hivyo itatusaidia sana. Na kuna wanaopinga wakiwaita DP World ni matapeli, hivyo kitendo cha Bunge letu kuridhia hiyo IGA, kumewafanya wachoke na kudhani, it's the end of the road. Naomba kuwapa faraja kuwa it's not the end!.
Hiyo HGA ni makubaliano tuu na sio mkataba, yaani ni an agreement na sio contract. Kila mkataba ni agreement, lakini sio kila agreement ni mkataba, mfano mzuri ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuunda Tanzania, ni makubaliano tuu na sio mkataba, mkifika mahali mkashindwa kuelewana, mnagawana tuu fito, kila mtu anasepa kivyake
Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?!.
Hivyo kile Bunge letu lilichoridhia, ni agreement tuu, tukiithibitishia serikali yetu, hawa DP World, pamoja na uzuri wao wote, pamoja na uwezo wao mkubwa wa kuendesha Bandari kibao, lakini ni matapeli na wana matatizo lukuki, hivyo serikali yetu iwe makini sana kabla ya kusaini HGA, na utepeli wao, ukiwekwa wazi peupe, tutaisaidia sana serikali yetu na kulisaidia taifa letu tusiingizwe mkenge na Mwarabu wa Dubai kwasababu tuu ni mtu mkarimu, amemkirimu Mama yetu kuipaisha bure Tanzania kwenye expo Dubai, akawakirimu waserikali wetu, kwa trips za Dubai, akawakirimu waheshimiwa wabunge wetu kwa trips za Dubai, na kuwakirimu media na waandishi wa habari wetu kwa trips za Dubai.
Japo Rais wetu, Mama Samia, ana nia ya kweli na ya dhati kulisaidia taifa letu, lakini anapokutana na matapeli wa kimataifa wakamuingiza mkenge, sisi watu wa Mhimili wa Nne, the media, tuna wajibu wa kulisaidia taifa letu kwa kuonyesha utepeli uko wapi, kisha serikali yetu ikiamua kuendelea na HGA ya Mwarabu wa Dubai, sisi watu wa media, tutakuwa na a clear conscious kuwa tumetimiza wajibu wetu, tumeieleza serikali yetu inavyotaka kuingizwa mkenge.
Kwa vile mimi licha ya kuwa ni mwandishi tuu wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, mimi pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, kwa kujitolea kutetea haki bure, hivyo nitawaletea makubaliano hayo na kuwachambulia kuwaonyesha jinsi tunavyotaka kutapeliwa mchana kweupe.
Utapeli wa kwanza mkubwa, ni hakuna mtu yoyote kati yetu aliyefanya a due diligence report ya DP World, tunaelezwa ni Governmental Organisation, wakati sii kweli, it's a private company!.
Mkataba wa IGA na HGA inaingiwa kati ya serikali na serikali, hivyo ukisoma documents za makubaliano utaona ni kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya UAE, lakini signatories kwa serikali ya Tanzania ni serikali kweli, lakini kwa serikali ya UAE, signatories ni Mwarabu wa Dubai wa DP World na sio serikali ya UAE hivyo hapa tunatapeliwa!, serikali yetu inaingizwa mkenge kuingia mkataba na a private company disguised as a government of UAE kumbe ni kampuni binafsi!.
Jambo la pili, kuna kipengele cha kuizuia nchi isiendeleze Bandari nyingine, hivyo kuiweka mashakani Bandari ya Bagamoyo, hili halikubaliki hata kidogo!.
Kwavile saa hizi ni usiku mkubwa, Joni Mtembezi ananisisitiza nitembee tembee nae hivyo nitamalizia kesho.
Paskali.