Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!

Yani huwa unaandika mambo ya misingi,mipia kwa macho ya ziada naona tapeli sio mwarabu bari anaeridhia na kama watanzania walowengi wanaona kwanini wanaoushabikia wasione? Hapa Pascal tunalia na aliempa Mimba mwanafunzi wakati aliyebeba mimba hakuwahi lalamika kama amebakwa,,
 
Naona mnatafuta pa kujikosha. Agreement yeyote ikisainiwa inakuwa enforcable unless imesema wazi kuwa saini hizo sio ishara ya commitment. Kwa vile mmesaini kuwa Agreement hiyo haiwezi kuvunjwa kwa sababu yeyote ( ikiwa pamoja na kutotimiza masharti yake), mkijaribu kuuvunja itabidi penalties kibao. Bandari ya Djibouti hivi karibuni imeamriwa kuwalipa DPW mamilioni ya dola baada ya kuamua kumpa kazi mchina tofauti na makubaliano yao na DPW. Mliamua kuweka pamba masikioni kwa kuamini kuwa muarabu ni muungwana sasa tuone mtakavyojinasua akionyesha makucha yake. Hamuwezi kusema makubaliano aliyosaini Rais na Waziri yalikuwa ya masihara tu. DPW tunae hata afanye nini. Tutafukuzana kwenye HGA lakini kwenye IGA hatuchomoki.

Amandla...
 
P tafadhali be a real nigga with truth to flown to yo' mouth, wew ni muandishi nguli sasa unapokuja na mamb ya kusadikika ambayo una uhakika kbs hayawezekan unaitia aibu tasnia yako!! Unasema tukigundua ni matapeli tutawafurusha 🤣🤣🤣 mmeshindwa fanya vetting kabla kuanza early process, nakuhakikishia hakuna mwenye ubavu wa kuwafurusha na hii ngoma ndo ishaisha!! Eti kuwafurusha 🤣🤣🤣mtalipa madeni ya kimikataba mpaka mwisho wa dahari!!!
 
Watanzania na utahira,hamjambo!

Huo Mkataba kwenda Bungeni umetokana na kutaka kuzima kelele za watu,but Mkataba ulisha sainiwa siku nyingi na watu wapo saiti wanaendelea na kazi.

Mkataba lukuki tena ya project kubwa haipelekwi Bungeni na inaendelea.Tatizo mmoja kubwa ni kuwa Watanzania huwa hawafatilii mambo yanayofanywa na Serikali yao.

Tuulize tuliopo huki tutakuambia
 
Jiadhari na wasiojulikana maana sasa wamepewa kinga tukufu!
 
Wewe kama umesoma sheria basi ulienda kusomea ujinga.

Jwanza Emirate of Dubai ni "state" iliyopo kwenye Muungano wa United Arab Emirates.

Dubai ina sovereign wealth fund ambayo haihusiani na UAE fund.


Kama hiyo haikutoshi, Ruler wa Dubai ana haki ya kum appoint yeyote asaini mkataba kwa ajili ya Dubai, hata wewe.

Dubai ni Monarchy siyo republic kama Tanzania.


Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Watanzania ni watu wa kulalamika mitandaoni Lakini hata siku moja hawawezi kuchukua hatua. Mtu aliyeguswa sana aende mahakamani akazuie mkataba usisainiwe. Nyingine zote kelele za mwenye nyumba tu ambazo hazimzuii mpangaji kulala usingizi.
 
Paschal, umeandika kwa tahadhari ya kutotaka uonekani ni mkosoaji wa serikali. Waambie Watanzania ukweli kwamba imeisha hiyo. na si huyu aliyesemwa labda tungoje mwingine
 
Watanzania ni watu wa kulalamika mitandaoni Lakini hata siku moja hawawezi kuchukua hatua. Mtu aliyeguswa sana aende mahakamani akazuie mkataba usisainiwe. Nyingine zote kelele za mwenye nyumba tu ambazo hazimzuii mpangaji kulala usingizi.

Mahakama zipi unaweza kwenda kuzuia matakwa ya serikali? Mifano ipo kibao kuwa serikali haiheshimu mahakama. Labda useme mahakama za kimataifa ila sio hizi za majaji wa michongo.
 
Watu wamesoma kichwa Cha habari hawajasoma content wanaanza kushusha kejeli kwa Mleta mada.

Huu uvivu wa kusoma na ugumu wa kuelewa utatu cost siku zote!
100% Ndiyo maana si ajabu tunaingizwa mkenge kwenye mikataba ya kitapeli.

Pascal Mayalla ameandika ujumbe wa maana sana. Watu waache porojo, wajifunze kusoma na kuchambua mambo. Pia, waache hasira, hazitowasaidia kwa sasa. Mbaya wao yuko palee katulia, analindwa na kulishwa 24/7.
 
Wakili msomi nakuita mara3 kwanza asante umeandika kizalendo kiasi umeeleweka trust me the so called makubaliano kama ulivyotueleza , kisomi haya makubaliano yamevalishwa mwanvuli yaonekane kama kweli ni makubaliano lakini kiualisia huu ni mkataba kabisa tena usio na kikomo

ukirudi hapa najua utaliongelea hili maana binafsi nakusubiri uoneshe ukomo wa makubaliano haya ni upi? Umeoneshwa wapi? Na kama gaukuonesha Maana yake ni nini?. 🤣🤣

kwa akili za watanzania watakao leweshwa na pesa za mwarabu sidhani kama kuna kiumbe atadhubutu kusema haya yalikuwa makubaliano na si mkataba.

Dah kuna kitu nilitamani ukiongelee ila umekuja kisomi zaidi unang'ata kidogo unapuliza😉
msomi bana wacha tuendelee kula mtori nyama tutazikuta chini naweka kambi hapa. Pascal Mayalla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…