#COVID19 Japo Chanjo ni hiyari, ila ni muhimu. Hupandi Ndege bila cheti cha Kupima COVID19. Kama unasafirisafiri, Chanjo ni Muhimu

Daaah yaani sijaelewa kbs,kwamba hao waliolia na kusaga meno hawajui kuwa wanatakiwa kwenda na cheti cha corona airport kinachoonyesha uko negative?
Asante kwa ushauri khs chanjo but khs corona test hiyo inajulikana,husafiri bila cheti cha corona cha negative results,hao wasafiri inamaana hata hiyo airline waliokata ticket hawakuwaambia?mbn mambo yako wazi na kila airline au nchi unayoenda inakua na masharti khs corona unayotakiwa kuyajua kabla ya kuanza safari.
Hao waliorudi PCR test zimechelewa kutolewa na maabara kuu ya taifa ni wengi wamekosa kusafiri leo maana mpaka muda huu vyeti vilivyotakiwa vitoke jana mpaka sasa havi havijatoka labda wanaosafiri usiku ndiyo wataondoka
 
UFAFANUZI

Hakuna sharti la chanjo ya Corona kwa wasafiri wanaokwenda nje ya nchi. Ni vema msafiri akauliza shirika la ndege analokwenda nalo pamoja na masharti ya nchi anayotembelea. Kwa zile nchi ambazo zinahitaji kipimo cha UVIKO-19 msafiri afanye kipimo hicho ndani ya masaa 24 hadi 48 kabla ya kuanza safari. Upimaji unafanyika kwa msafiri kufanya booking kupitia pimacovid.moh.go.tz ambapo atachagua kituo cha upimaji . Baada ya upimaji majibu yatatumwa kwake kwa njia ya barua pepe aliyotumia wakati wa booking. Akifika Airport cheti hicho kitahakikiwa katika dawati la afya. Unashauriwa kujiepusha na vyeti feki.

Kuhusu uzushi unaoenea kwamba Chanjo ya UVIKO-19 inatolewa mashuleni hiyo sio kweli,Chanjo zote zinatolewa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vilivyoainishwa na Chanjo hiyo inatolewa kwa makundi Yale matatu yalivyotangazwa.

Watoto sio walengwa wa Chanjo hii na vilevile hakuna kituo kwenye shule.

Imetolewa na ;
Catherine Sungura
Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini-Afya
8/8/2021
Kwani mkuu wale uliowaona pale terminal 3 wakilia, walikuwa wanalilia vyeti vya vipimo? Mwamba tusifanyane wajinga aisee, wewe umewaona kabisa wanalia kwa vile hawakuwa na vyeti vya chanjo sasa unageukaje tena mchana kweupe namna hii? Au umetishiwa kwamba utakosa uteyuzi? Mimi nimechua ile hoja yako ya mwanzo hii ya kutuomba radhi siikubali kwa sababu wakati wale raia wanajutia kukosa vyeti vya chanjo wewe ulikuwapo na uliwasikia kabisa!
 
Haya tuone sasa wale wenye vijikanisa feki vya kuibia watu watafanyaje wakitaka kuomba pesa kwa mabwana zao kule Ulaya na Marekani?
 
Kama umeshachanjwa, kwa nini tena uonyeshe cheti cha kupima?

Ina maana chanjo uliyochanjwa haina maana?
Chanjo ni kinga, hata ukichanja bado unaweza kupata Corona kwasababu virus huwa vina mutate na kutoa different variants from time to time, hivyo ili kujiridhisha msafiri huna Corona, lazima upime na kuonyesha cheti cha vipimo.
P
 
Haya tuone sasa wale wenye vijikanisa feki vya kuibia watu watafanyaje wakitaka kuomba pesa kwa mabwana zao kule Ulaya na Marekani?
Watahitaji kupima tuu na sio lazima kuchanja.
P
 
Wanabodi,

Déclaration of Interest.
Mimi Pascal Mayalla ni pro Vaccination ya Covid 19 na nimechanja chanjo ya Corona, na nawahimiza Watanzania, tuchanje.

Niko hapa Terminam 3 Airport ya DIA, nimeshuhudia baadhi ya watu wacheche wakijuta, wakilia kwa uchungu na kusaga meno kwa kakataliwa kusafiri kutokana na kutokuwa na cheti cha kipimo cha Corona hivyo kurudishwa nyumbani na mabegi ya, hivyo kosa la kukosa cheti cha kupima Covid 19, kunaweza kukusababisha safari yako ya ulaya kuishia Airport !.

Kumbe japo chanjo ya Corona ni hiyari, lakini kwa watu wanaotumia usafiri wa anga, ndege, au kukwea pipa kwa safari za kimataifa, chanjo hii ni muhimu. Ili upande ndege, ni lazima upime Corona na kupewa cheti kinachoonyesha hakuna Corona. Hivyo chanjo ya Corona ni muhimu ili kujiihakikishia usalama usipate Corona kirahisi , kwasababu siku hizi, ili usafiri nje, ni lazima upime Corona , na kuonyesha cheti kuwa umepima Corona na huna Corona ndio unapanda ndege. Ukichanja chanjo ya Corona, unazuia uwezekano wa kupata Corona kwa urahisi.

Mtu hupandi ndege bila ya kuwa na cheti kupima Corona!, hivyo ili usipate Corona ni muhimu sana kuchanja chanjo ya Corona ili kujiepusha na kupata Corona.

Zamani ukiingia tu Airport unawahi counter ya check in. Sasa ukiingia Airport unaanzia meza ya vérification ya cheti cha kupima Corona. Baada ya kuwa cleared kuwa umepima Corona na umekutwa hakuna ndio una proceed to check in counter.

Hivyo natoa wito, kama wewe ni mtu wa kusafiri safiri, au kazi yako inahusisha safari za nje ya nchi, hata kama umeamua kuitumia hiyari yako kutochanja nakushauri nenda kachanje, ili kuwa na uhakika umejikinga Corona ili ukipata safari, uweusije na uhakika wa Usalama wako dhidi ya Corona, kwa maana utapima na kukutwa hauna, usije kulia na kusaga meno, kama jana pale airport.

Japo chanjo ya Corona ni hiari, kwa watu wanao safiri safiri, chanjo ya Corona ni muhimu sana, hivyo hata kama ulipanga kuitumia hiyari yako usichanje, nakushauri kachanje!

Paskali
Update 1.
UFAFANUZI WA WIZARA YA AFYA

Hakuna sharti la chanjo ya Corona kwa wasafiri wanaokwenda nje ya nchi. Ni vema msafiri akauliza shirika la ndege analokwenda nalo pamoja na masharti ya nchi anayotembelea. Kwa zile nchi ambazo zinahitaji kipimo cha UVIKO-19 msafiri afanye kipimo hicho ndani ya masaa 24 hadi 48 kabla ya kuanza safari. Upimaji unafanyika kwa msafiri kufanya booking kupitia pimacovid.moh.go.tz ambapo atachagua kituo cha upimaji . Baada ya upimaji majibu yatatumwa kwake kwa njia ya barua pepe aliyotumia wakati wa booking. Akifika Airport cheti hicho kitahakikiwa katika dawati la afya. Unashauriwa kujiepusha na vyeti feki.

Kuhusu uzushi unaoenea kwamba Chanjo ya UVIKO-19 inatolewa mashuleni hiyo sio kweli,Chanjo zote zinatolewa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vilivyoainishwa na Chanjo hiyo inatolewa kwa makundi Yale matatu yalivyotangazwa.

Watoto sio walengwa wa Chanjo hii na vilevile hakuna kituo kwenye shule.

Imetolewa na ;
Catherine Sungura
Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini-Afya
8/8/2021

UPDATE 2.
Kufuatia upotoshaji uliotokana na thread hii, pale mwanzo kabla haijarekebishwa, mimi Pascal Mayalla naomba kuomba radhi kwa usumbufu wowote uliosababishwa na taarifa ya awali ambayo haikuwa sahihi, sio sahihi. Naahidi kutoa kila aina ya ushirikiano kwa serikali yetu kupitia Wizara ya Afya, na kushiriki kikamilifu katika utoaji wa elimu sahihi ya chanjo ya Corona.

Kunapotokea kosa lolote, katika jambo lolote, kitu muhimu sio tuu kuangalia kosa lililotendeka, (actus reus), bali nia ya mtenda kosa, kama alikuwa na nia ya kutenda kosa (mens rea)

Na mwisho naomba kusisitiza kuwa japo kwa sasa chanjo ya Corona ni hiari, kitu kinachohitajika kabla ya kusafiri nje ni cheti cha kupima Corona, huko tuendako tutafikia mahali cheti cha chanjo ya Corona kitahitajika kabla ya kupata Visa za kuingia nchi fulani fulani, hivyo nitafika muda chanjo ya Corona itakuwa ni hiari ya lazima.

Pasco Mayalla

Threads Nyingine za mwandishi huyu kuhusu Chanjo ya Corona

Mkuu kuna mtu amechanja mkono umevimba kakimbizwa hospitali lakini akafariki kwa upande wangu bado sina imani na hii chanjo. Na pia walisema ukichanja utapata korona ila haitakua na effect kubwa sasa nashindwa kuelewa nini maana yake. Mimi bado ninapata ukakasi na pia bado sijajua chanjo ipi ni salama kwa maana kila siku chanjo mpya inakuja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chanjo ni kinga, hata ukichanja bado unaweza kupata Corona kwasababu virus huwa vina mutate na kutoa different variants from time to time, hivyo ili kujiridhisha msafiri huna Corona, lazima upime na kuonyesha cheti cha vipimo.
P
Bullshit!

Naona unaongelea jambo ambalo hata hulielewi vizuri.

Hakuna maana yoyote ile kumuwekea restrictions mtu ambaye ameshachanjwa.

Huwezi kumwekea restrictions zile zile mtu ambaye ameshachanjwa na mtu ambaye bado hajachanjwa.

Otherwise, how do you convince someone to get the vaccine when at the end of the day that vaccine won’t make a difference between the vaccinated and the unvaccinated?
 
Mkuu kuna mtu amechanja mkono umevimba kakimbizwa hospitali lakini akafariki kwa upande wangu bado sina imani na hii chanjo. Na pia walisema ukichanja utapata korona ila haitakua na effect kubwa sasa nashindwa kuelewa nini maana yake. Mimi bado ninapata ukakasi na pia bado sijajua chanjo ipi ni salama kwa maana kila siku chanjo mpya inakuja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu dr shayo , kwanza pole sana kwa hiyo incident. Kwa vile kila mtu ana saa yake aliyopangiwa, saa ikifika ni imefika, unakwenda. Hivyo kuna uwezekano saa yake ndio ilikuwa imefika. Unless utupatie post mortem report kuonyesha the cause of death ni hiyo chanjo.
Kuhusu chanjo ipi ni salama, chanjo zote ni salama ila zinatofautiana eficacy na side effects, kutegemeana na eneo, mfano Israël wanatumia chanjo Marekani na kuziponda chanjo za India, China na Urusi ila zimekuja kuwa best kwa huku kwetu Afrika kuliko chanjo za wazungu!.
P
 
Bullshit!

Naona unaongelea jambo ambalo hata hulielewi vizuri.

Hakuna maana yoyote ile kumuwekea restrictions mtu ambaye ameshachanjwa.

Huwezi kumwekea restrictions zile zile mtu ambaye ameshachanjwa na mtu ambaye bado hajachanjwa.

Otherwise, how do you convince someone to get the vaccine when at the end of the day that vaccine won’t make a difference between the vaccinated and the unvaccinated?

Akili nyingi izi[emoji123]
 
Mkuu dr shayo , kwanza pole sana kwa hiyo incident. Kwa vile kila mtu ana saa yake aliyopangiwa, saa ikifika ni imefika, unakwenda. Hivyo kuna uwezekano saa yake ndio ilikuwa imefika. Unless utupatie post mortem report kuonyesha the cause of death ni hiyo chanjo.
Kuhusu chanjo ipi ni salama, chanjo zote ni salama ila zinatofautiana eficacy na side effects, kutegemeana na eneo, mfano Israël wanatumia chanjo Marekani na kuziponda chanjo za India, China na Urusi ila zimekuja kuwa best kwa huku kwetu Afrika kuliko chanjo za wazungu!.
P
Mkuu mtu alikua ni mzima haumwi lakini baada ya kupata hiyo chanjo, mkono uliochomwa ndo ukaanza kuvimba hadi ukapelekea mauti. Sasa kwa kifupi hapo inaonyesha hiyo kinga ndo iliyomdhuru. Lakini pia kuna waliochanja siku za karibuni naona wako poa. Lakini ninachofikiri ni kwamba labda kuna baadhi ya watu hii chanjo haitawakubali. Kikubwa wataalam wetu waangalie scenario kama hiyo may be wakipima mtu blood group au allergie inaweza kusaidia.

Kwa vile mpaka sasa bado hatujapata uthibitisho wa kidakitari kuwa chanzo cha kifo ni hiyo chanjo, naomba endelea kuzihifadhi taarifa hizo ili kuzuia kuleta hofu. Kuna mtu anaonekana kusumbuliwa na kitu fulani, kumbe the cause of death is somethings else !.

Kitu ambacho sina uhakika kwa huku kwetu, ni kama tunauwezo huo wa kubaini kifo cha chanjo, usikute ni malaria !.
p
 
Hao waliorudi PCR test zimechelewa kutolewa na maabara kuu ya taifa ni wengi wamekosa kusafiri leo maana mpaka muda huu vyeti vilivyotakiwa vitoke jana mpaka sasa havi havijatoka labda wanaosafiri usiku ndiyo wataondoka
Kweli ni vyeti vya PCR, vimechelewa, na sio kwa kukosa chanjo.
P
 
Mayalla umechemka,ungetulia uulize vizuri.
Umechanganya cheti cha kipimo cha corona na chanjo ya corona ni vitu viwili tofauti.
Chanjo ya corona ni hiari cheti cha kipimo cha corona covid test ni lazima ukisafiri na ndege.
 
Kwani mkuu wale uliowaona pale terminal 3 wakilia, walikuwa wanalilia vyeti vya vipimo? Mwamba tusifanyane wajinga aisee, wewe umewaona kabisa wanalia kwa vile hawakuwa na vyeti vya chanjo sasa unageukaje tena mchana kweupe namna hii? Au umetishiwa kwamba utakosa uteyuzi? Mimi nimechua ile hoja yako ya mwanzo hii ya kutuomba radhi siikubali kwa sababu wakati wale raia wanajutia kukosa vyeti vya chanjo wewe ulikuwapo na uliwasikia kabisa!
Mkuu Manjagata , kiukweli mtu ukiwa mbobezi mno unafikia point unaharibu, ndio mimi, huwezi amini, very honestly nilipoona watu wanarudishwa kwa kukosa vyeti, nika assume ni vyeti vya chanjo, kumbe hitaji sio cheti cha chanjo, bali ni kipimo cha Corona.
Nakuomba uukubali msamaha wangu.
P
 
Back
Top Bottom