#COVID19 Japo Chanjo ni hiyari, ila ni muhimu. Hupandi Ndege bila cheti cha Kupima COVID19. Kama unasafirisafiri, Chanjo ni Muhimu

#COVID19 Japo Chanjo ni hiyari, ila ni muhimu. Hupandi Ndege bila cheti cha Kupima COVID19. Kama unasafirisafiri, Chanjo ni Muhimu

Majibu yanasababisha abiria wengi wanakosa ndege shida ni system zetu za zinachelewa kutoa majibu.
 
Mtu hupandi ndege bila ya kuwa na cheti kupima Corona!, hivyo ili usipate Corona ni muhimu sana kuchanja chanjo ya Corona ili kujiepusha na kupata Corona.

Zamani ukiingia tu Airport unawahi counter ya check in. Sasa ukiingia Airport unaanzia meza ya vérification ya cheti cha kupima Corona. Baada ya kuwa cleared kuwa umepima Corona na umekutwa hakuna ndio una proceed to check in counter.

Embu rudia hizi paragraph zako mbili alafu angalia na kichwa cha habari.

Wanangalia cheti ya kupima korona au chanjo ya korona?
 
Mkuu Manjagata , kiukweli mtu ukiwa mbobezi mno unafikia point unaharibu, ndio mimi, huwezi amini, very honestly nilipoona watu wanarudishwa kwa kukosa vyeti, nika assume ni vyeti vya chanjo, kumbe hitaji sio cheti cha chanjo, bali ni kipimo cha Corona.
Nakuomba uukubali msamaha wangu.
P
Paskali wewe ni mwandishi mashuhuri ila kadri siku zinavyoenda umahiri wako unapororomoka.

Hii yote inatokana na wewe kuandika kwa kutaka kuifurahisha serikali.
Itakugharimu sana.
 
Bora umepata wasaa wa kutafuta ukweli...

Maana kilichonileta kwenye uzi wako ni baada ya kukutana na screenshot ikieleza ni lazima kwa msafiri wa kimataifa kuwa na chanjo ilihali binafsi najua sio sahihi hilo
 
lakini kwa watu wanaotumia usafiri wa anga, ndege, au kukwea pipa kwa safari za kimataifa
Kuna tofauti gani kati ya usafiri wa anga, ndege na kukwea pipa?

Na una shahada ya uandishi wa habari na sheria, ulizipata-pataje wakati basic literal reasoning huna ???? Vyuo vyetu ni vya hovyo sana.
 
Hapa Tanzania haifiki hata asilimia 10 ya wananchi wote wanaopanda ndege.hvyo MTU kama we we unaemendea uongozi kwa kutuma viujumbe vyako jf vyepesi vyepesi unaonekana bado sana hata kuupata wenyekiti wa mtaa bado sana.na watu wa HV ndio wanaomuangusha samia baada ya kuanza kuwachukua Mara kwenye vituo vya radio,bongo fleva,Mara ma miss.unategemea tutapata nn zaidi ya matatizo tuu?
 
Muda utatupa majibu, you will see a more/less lethal or a more/less infectious strain again, courtesy of a mass vaccination scheme....
 
Wengine tumeamua kutokuchanja chanjo na tutafia Tanzania kizalendo bibi yangu yuko mapinga ulaya naenda kufanya nini mimi!!!!!
Mkuu kamituga , kwa vile chanjo ni hiyari, uko huru kutochanja, la huyo bibi yako Mapinga pia yuko salama as long as wewe hotompelekea Corona. Kwa vile wewe ni mchakarikaji, unaweza kukumbwa na Corona, na kwa vile wewe uko fit, wala usiugue au kuonyesha dalili yoyote, hivyo siku unamtembelea bibi Mapinga, ukampelekea, kama hana chanjo anything can happen. Ukichanja, unakuwa na uhakika wa kujilinda wewe na kumlinda bibi yako Mapinga. Ukikumbana na Corona huku umechanja, uwezekano wa kupata ni mdogo na huambukizi wengine !.

Kachanje!.
P
 
Sitasafiri tena. Maana sio lazima nisafiri. Nitazunguka mikoani tu
Kuna wasafiri wa aina tatu, safari binafsi, safari za kikazi, na safari za dharura, uwezo wa kuamua hautasafiri tena ni kwa safari binafsi tuu lakini hapo ulipo unaweza kupata deal nzuri nchi jirani ukahitaji kusafiri au ukapata dharura, inayokuhitaji kusafiri nje. Nakushauri bora tuu uchanje uwe tayari na uhakika na usalama wako na kuwalinda wengine.

P
 
Waziri wa Afya, Dorothy Gwajima karudi na rungu.

Ametoa rai kuwa viongozi ambao mpaka sasa hawajachanjwa, watatakiwa waachie ngazi kwani hawawezi kusimamia kampeni ya kusimamia uchanjwaji dhidi ya corona.

Waziri wa Afya amesema kama Rais kachanja ili iwe mfano, sasa hao viongozi hawatetei msimamo wa Serikali

Tulisha liona hili huko nyuma: #COVID19 - Kuchanja sasa kuwe lazima, hasa wafanyakazi serikalini. Chanja au achia ngazi

View attachment 2028866
Naunga mkono hoja, hiki alichokisema Waziri Gwajima, ni kitu cha kweli, kama serikali yako imekubali chanjo na rais wako kachanja, wewe kiongozi wa umma, lazima uonyeshe uongozi kwa vitendo na kwa mfano, kwa viongozi wote wakuu wa umma lazima wachanje hadharani, ule uhiari, hauwahusu viongozi wa umma, kwa viongozi wa umma kuchanja ni lazima, asiyechanja aachie ngazi!.

Niliwahi kusema mahali, chanjo ya Korona japo inasemwa kuwa ni hiyari, hii ni hiyari ya lazima, kuna nchi mtu huruhusiwi kuingia bila cheti cha chanjo ya Corona. Hivyo sasa tunaanza mdogo mdogo kwa viongozi wa umma, chanjo sio hiyari ni lazima,
kama wewe ni kiongozi wa umma na huamini chanjo, achia ngazi!.
P.
 
Back
Top Bottom