#COVID19 Japo Chanjo ni hiyari, ila ni muhimu. Hupandi Ndege bila cheti cha Kupima COVID19. Kama unasafirisafiri, Chanjo ni Muhimu

Hao waliorudi PCR test zimechelewa kutolewa na maabara kuu ya taifa ni wengi wamekosa kusafiri leo maana mpaka muda huu vyeti vilivyotakiwa vitoke jana mpaka sasa havi havijatoka labda wanaosafiri usiku ndiyo wataondoka
 
Kwani mkuu wale uliowaona pale terminal 3 wakilia, walikuwa wanalilia vyeti vya vipimo? Mwamba tusifanyane wajinga aisee, wewe umewaona kabisa wanalia kwa vile hawakuwa na vyeti vya chanjo sasa unageukaje tena mchana kweupe namna hii? Au umetishiwa kwamba utakosa uteyuzi? Mimi nimechua ile hoja yako ya mwanzo hii ya kutuomba radhi siikubali kwa sababu wakati wale raia wanajutia kukosa vyeti vya chanjo wewe ulikuwapo na uliwasikia kabisa!
 
Haya tuone sasa wale wenye vijikanisa feki vya kuibia watu watafanyaje wakitaka kuomba pesa kwa mabwana zao kule Ulaya na Marekani?
 
Kama umeshachanjwa, kwa nini tena uonyeshe cheti cha kupima?

Ina maana chanjo uliyochanjwa haina maana?
Chanjo ni kinga, hata ukichanja bado unaweza kupata Corona kwasababu virus huwa vina mutate na kutoa different variants from time to time, hivyo ili kujiridhisha msafiri huna Corona, lazima upime na kuonyesha cheti cha vipimo.
P
 
Haya tuone sasa wale wenye vijikanisa feki vya kuibia watu watafanyaje wakitaka kuomba pesa kwa mabwana zao kule Ulaya na Marekani?
Watahitaji kupima tuu na sio lazima kuchanja.
P
 
Mkuu kuna mtu amechanja mkono umevimba kakimbizwa hospitali lakini akafariki kwa upande wangu bado sina imani na hii chanjo. Na pia walisema ukichanja utapata korona ila haitakua na effect kubwa sasa nashindwa kuelewa nini maana yake. Mimi bado ninapata ukakasi na pia bado sijajua chanjo ipi ni salama kwa maana kila siku chanjo mpya inakuja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chanjo ni kinga, hata ukichanja bado unaweza kupata Corona kwasababu virus huwa vina mutate na kutoa different variants from time to time, hivyo ili kujiridhisha msafiri huna Corona, lazima upime na kuonyesha cheti cha vipimo.
P
Bullshit!

Naona unaongelea jambo ambalo hata hulielewi vizuri.

Hakuna maana yoyote ile kumuwekea restrictions mtu ambaye ameshachanjwa.

Huwezi kumwekea restrictions zile zile mtu ambaye ameshachanjwa na mtu ambaye bado hajachanjwa.

Otherwise, how do you convince someone to get the vaccine when at the end of the day that vaccine won’t make a difference between the vaccinated and the unvaccinated?
 
Mkuu dr shayo , kwanza pole sana kwa hiyo incident. Kwa vile kila mtu ana saa yake aliyopangiwa, saa ikifika ni imefika, unakwenda. Hivyo kuna uwezekano saa yake ndio ilikuwa imefika. Unless utupatie post mortem report kuonyesha the cause of death ni hiyo chanjo.
Kuhusu chanjo ipi ni salama, chanjo zote ni salama ila zinatofautiana eficacy na side effects, kutegemeana na eneo, mfano Israël wanatumia chanjo Marekani na kuziponda chanjo za India, China na Urusi ila zimekuja kuwa best kwa huku kwetu Afrika kuliko chanjo za wazungu!.
P
 

Akili nyingi izi[emoji123]
 
Mkuu mtu alikua ni mzima haumwi lakini baada ya kupata hiyo chanjo, mkono uliochomwa ndo ukaanza kuvimba hadi ukapelekea mauti. Sasa kwa kifupi hapo inaonyesha hiyo kinga ndo iliyomdhuru. Lakini pia kuna waliochanja siku za karibuni naona wako poa. Lakini ninachofikiri ni kwamba labda kuna baadhi ya watu hii chanjo haitawakubali. Kikubwa wataalam wetu waangalie scenario kama hiyo may be wakipima mtu blood group au allergie inaweza kusaidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa vile mpaka sasa bado hatujapata uthibitisho wa kidakitari kuwa chanzo cha kifo ni hiyo chanjo, naomba endelea kuzihifadhi taarifa hizo ili kuzuia kuleta hofu. Kuna mtu anaonekana kusumbuliwa na kitu fulani, kumbe the cause of death is somethings else !.

Kitu ambacho sina uhakika kwa huku kwetu, ni kama tunauwezo huo wa kubaini kifo cha chanjo, usikute ni malaria !.
p
 
Hao waliorudi PCR test zimechelewa kutolewa na maabara kuu ya taifa ni wengi wamekosa kusafiri leo maana mpaka muda huu vyeti vilivyotakiwa vitoke jana mpaka sasa havi havijatoka labda wanaosafiri usiku ndiyo wataondoka
Kweli ni vyeti vya PCR, vimechelewa, na sio kwa kukosa chanjo.
P
 
Mayalla umechemka,ungetulia uulize vizuri.
Umechanganya cheti cha kipimo cha corona na chanjo ya corona ni vitu viwili tofauti.
Chanjo ya corona ni hiari cheti cha kipimo cha corona covid test ni lazima ukisafiri na ndege.
 
Mkuu Manjagata , kiukweli mtu ukiwa mbobezi mno unafikia point unaharibu, ndio mimi, huwezi amini, very honestly nilipoona watu wanarudishwa kwa kukosa vyeti, nika assume ni vyeti vya chanjo, kumbe hitaji sio cheti cha chanjo, bali ni kipimo cha Corona.
Nakuomba uukubali msamaha wangu.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…