Wanabodi,
Hii ni Makala yangu ya gazeti la Mwananchi.
View attachment 3334620
Leo, naendelea na zile makala za Ijue Katiba ya JMT, nikijikita kwenye kitu kinachoitwa Sovereignty, huu ni uhuru wan chi, kutoingiliwa kwenye mambo yake ya ndani. Nimeileta mada hii baadab ya kusikia malalamiko ya baadhi ya Watanzania kuwa Bunge la Ulaya, limepitisha maazimio yanaingilia uhuru wetu na soveignity ya nchi yetu.
Sovereignty ni kitendo cha nchi kuwa huru kuamua mambo yake na kufanya mambo yake kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu yoyote, taasisi yoyote, au mataifa yoyote, hivyo kitendo kilichofanywa na Bunge la Ulaya, kuonekana kama ni kuingilia sovereignty yetu na kulipangia Bunge la JMT nini cha kufanya.
Kimataifa, Tanzania ni nchi moja ya JMT, yenye rais mmoja, rais wa JMT, yenye katiba moja, katiba moja ya JMT na soveiginity moja ya sovereignty ya JMT.
Tanzania ni nchi huru inayotawaliwa na katiba ya JMT, sheria zilizotungwa na Bunge la JMT, kanuni na taratibu za JMT. Kitaifa, Tanzania itaendeshwa kwa katiba ya JMT na sheria zilizotungwa na Bunge la JMT. Lakini katika uendeshaji wa nchi, nchi zote zinaendeshwa kwa sheria mbili,
1. Sheria za nchi husika, zinaitwa domestic laws, ni sheria zinazotungwa na Bunge letu, ni sheria zetu za ndani.
2. Sheria za kimataifa, International Laws ambazo hazikutungwa na Bunge letu, lakini Tanzania, tumezisaini kuzikubali, na sheria hizo za kimataifa, kuletwa nchini, kuingizwa kwenye Bunge letu kupitia process inayoitwa ratification, kwa Bunge kuridhia mikataba ya kimataifa, sheria hizo zikiisha ridhiwa na Bunge husika, yaani baada ya kuwa ratified, zinageuka ni sheria za Tanzania!, kwa lugha nyingine, ratification ni process ya ku domesticate international laws into local laws, yaani mikataba yote ya kimataifa Tanzania iliyo saini na Bunge letu kuridhia, sheria za mikataba hiyo zinakuwa ni sheria za Tanzania.
Hivyo Tanzania ikikiuka kipengele chochochote cha sheria hizo za kimataifa, Tanzania inaweza kujadiliwa na mabunge yoyote au taasisi za kimataifa na kupewa amri halali za kutekeleza sheria zote na kimataifa zilzo kiukwa, hivyo Bunge la Ulaya liko huru kuijadili nchi yoyote inayokiuka sheria zozote za kimataifa.
Kitu Watanzania wengi wasichojua ni kuwa kuna sheria nyingi za kimataifa kuhusu haki za binaadamu kwa mujibu wa Tamko la Kimataifa la Haki za Binaadamu, UDHR, ambalo Tanzania tumesaini, lakini hatuzitekelezi haki hizo, ikiwemo haki muhimu ya kuishi, wakati sheria zetu bado zina hukumu ya kifo.
Ili tuweze kutoka kwenye mtanziko huu, hatua ya kwanza ni kwa Bunge letu, linapata mamlaka yake kwa wananchi, kupitia katiba ya JMT ya Mwaka 1977, Wananchi ndio wenye nchi, wenye katiba, wenye Bunge, Bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi, linafanya shughuli zake kwa niaba ya wananchini, linatakiwa kutimiza kikamilifu wajibu wake wa kuisimamia serikali na vyombo vyake vyote kwa mujibu wa Ibara 63(2) ya Katiba ya JMT, kuhakikisha serikali haikiuki sheria zozote za kitaifa na kimataifa nchini Tanzania.
Kwa maneno mengine ni kwamba Bunge linapaswa kuisimamia Serikali kikamilifu na kuhakikisha serikali na chombo chake chochote, lazima kufanya mambo yake yote kwa mujibu wa katiba ya JMT, na wasiruhusu serikali yetu au chombo chochote cha serikali kufanya jambo lolote ambalo ni kinyume cha Katiba ya JMT.
Sio mara moja wala mara mbili nimeandika kwenye safu hii, umuhimu wa kufanya kwanza mabadiliko madogo ya katiba, ndipo tuje tufanye mabadiliko ya sheria, kwasababu katiba ndio sheria mama, na sheria nyingine zote, kabla hazijatungwa ni lazima ziendane na katiba.
Kuna mikataba mingi ya kimataifa Tanzania tumeiridhia, lakini hatuitekelezi!.
Mfano mzuri ni hii sheria iliyoanzisha Tume Huru ya Uchaguzi, sheria hii ni batili kwasababu ndani ya katiba bado haina tume huru. Mpaka hapa ninapoandika Katiba, ya JMT, haitambui INEC, bado inaitambua NEC.
Mfano mkubwa mzuri wa kawaida kabisa ni shurti la mgombea uongozi kudhaminiwa na chama cha siasa ni kinyume cha Ibara ya 21 ya katiba ya JMT, lakini kipengele hicgo kimechomekewa kwenye katiba yetu kibatiliti kwa mabadiliko ya katiba ya JMT yaliyofanywa hati ya dharura na Bunge, ambali lilibadili katiba kama vile linabadili sheria, wakati utaratibu wa Bunge kufanya mabadiliko halali ya katiba, haukufuatwa, hivyo hayo mabadiliko yamefanywa kiubatili!.
Shurti hili ni kinyume cha tamko la kimataifa la haki za binaadamu, ambalo Tanzania tumeridhia na kuingiza haki za binaadamu ndani ya katiba yetu. Tukizikiuka, tunashughulikiwa kimataifa.
Kipengele hicho ni kinyume cha tamko la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za kisiasa, Tanzania tumeridhia lakini hatutekelezi!.
Kipengele hicho pia ni kiyume cha African Charter of People and Political Rights ambazo Tanzania tumeridhia lakini hatutekelezi!.
Kati ya 1979 na 2005, Bunge la JMT limefanya mabadiliko ya katiba mara 14 kwa kutunga sheria ya mabadiliko ya katiba wakati Bunge kama Bunge, ni zao la katiba, halina mamlaka ya kubadilisha Katiba ya JMT kwa kutumia sheria ya kawaida ambayo haitamki kwamba lengo lake ni kubadilisha Katiba bali linaweza kubadili katiba kwa kutunga sheria ya mabadiliko ya katiba ndipo libadili katiba.
Dunia kwa sasa ni kijiji, Tanzania sio kisiwa, hivyo kila tunachofanya kinaonekana dunia nzima, na mataifa yote, kwa sasa yanayoendesha mambo yao kwa ukweli, uwazi na umakini mkubwa, na mambo ya mataifa yote yanafuatiliwa kimataifa, sote tunakijua kilichomkuta Rais Uhuru Kenyatta au El Bashri wa Sudan, tena afadhali hao walifikishwa mahakamani, lakini Ghadafi wa Libya na Sadaam Hussein, hawakuwa na bahati!, hata sisi enzi za Mwalimu Nyerere, tuliwasaidia ndugu zetu na majirani zetu wa Uganda, kwa kumshikisha adabu Yule dikiteta wao.
Ombi kwa Bunge letu, isimamieni serikali yetu kikamilifu, na ombi kwa serikali yetu, tuendelee kufanya mambo yetu kwa mujibu wa katiba na sheria, hatutasikia kunyooshewa kidole na yeyote na kupigiwa kelele yoyote.
Japo kelele za mlango, huwa hazimkoseshi mwenye nyumba usingizi, lakini zikizidi sana, zinakuwa ni kero kwa mwenye nyumba!, vipi hizi kelele za kutaka minimum reforms?, ni hitaji hili la minimum reforms, zimepelekea Chadema kuja na NRNE, ambayo kiukweli inasumbua sana kwa kelele!.
Ni kelele hizi, zimefanya mropokaji mmoja, akaropoka tuu kukinukisha mpaka uchaguzi usifanyike, na matokeo yake amehifadhiwa mahala salama, na kutwishwa kale ka kesi ka uongo na ukweli, matokeo yake sasa Tanzania inapigiwa kelele dunia nzima, Bunge la EU, wameanza, Congress soon watafuatia, hivi mwenye nyumba wetu kweli anapata msingizi mnono kweli?.
Ombi kwa Rais Samia, muda uliobaki kabla ya uchaguzi mkuu, ni muda wa kutosha kabisa kufanya mabadiliko madogo ya katiba na kuzizima kabisa hizi kelele zote ambazo zinatukera baadhi yetu, unless Mama kama wewe hazikukeri, na unapata usingizi wako mzuri kabisa!.
Mungu Mbariki Rais Samia Aweze!
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.