Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?


Mkuu kwanza kwenye biblia au hata Quran sijawahi kusoma kuwa Ishmael alipewa nchi ya Harani. Sijawahi kwa kweli.

Umesema vizuri

Moja ya ishara kuwa aliyetimiza ahadi ni Isaka ni hilo la taifa lao kuwa mpaka hivi leo.

Mimi na wewe na hata jamii zingine nyingi hazijui Historia zao.

Huyo Muhammad mwenyewe hajui ni kwakivipi ametoka kwa Ibrahim.
Hao waarabu wanaojinasibisha na Ibrahim wenyewe hawaelewi na ushahidi uliowazi kuwa Baba yao ni Ibrahim.

Hata ikiulizwa uzao au taifa la waishmael ni lipi sasa hivi hakuna majibu.
 
Kwa hiyo aliyetaka kuchinjwa ni nani?
Hilo ndilo swali lipo mezani.
Tunaomba ulijibu.t
 
Kwa hoja za wengi humu zinaonyesha kuwa Quran haijaeleza habari za mtoto yupi wa Ibrahimu alitakiwa kutolewa kafara, lakini Bibilia imeweka wazi kuwa aliyetakiwa kutolewa kafara ni Isaka

Nikimnukuu FAIZFOX ameenda mbali na kusema Quran haijazungumza habari za mtoto yeyote wa Ibrahimu kuchinjwa, hilo si limeisha
 
Kwani urithi ulikuwa Ni nini ningependa Kujua..
Maana nikiangalia Biblia Nakuta kuwa Ishmael au Waishmael ndo wafanya Biashara wakubwa sana wa Agano la kale..
Urithi ni vitu vile unavyopewa na mzazi wako vilivyo halali yako kutoka kwake. Vinaweza kukubariki au kukulaani. Isaka alipewa urithi wa vitu vyote vya Ibrahim. Vikihusisha ardhi, Mungu( agano) la kuwa baba wa mataifa, Wafalme kutoka kwake, kubariki Kwa watakaombariki. Watoto wengine wa Ibrahim waliopewa zawadi hivyo hawakurithishwa chochote Cha baba yao.
Pia kulikua na zuio la kuoa aina za wanawake. Hakuruhusiwa kuoa mtu ambae sio wa uzao wa baba yake. Yeye alioa Mmisri. Na kama ahadi ingekua Kwa Ismael Kwa Nini hakuna nabii zaidi ya Mohamed aliyetoka kwenye viuno vyake?
 
Sijaona kwenye Qur'an kuwa Ibrahim alikuwa na mtoto anitwa Ismail, au hayo ni mafundisho nje ya Qur'an?
Suratul Maryam aya 54

وَٱذْكُرْ فِى ٱلْكِتَٰبِ إِسْمَٰعِيلَ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ صَادِقَ ٱلْوَعْدِ وَكَانَ رَسُولًۭا نَّبِيًّۭا

TAFSIRI:

Na mtaje katika Kitabu Ismail. Bila ya shaka yeye alikuwa ni mkweli wa ahadi, na alikuwa Mtume, Nabii.
Aya ya pili
surat Ibrahim Aya ya 39

ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ٱلَّذِى وَهَبَ لِى عَلَى ٱلْكِبَرِ إِسْمَٰعِيلَ وَإِسْحَٰقَ ۚ إِنَّ رَبِّى لَسَمِيعُ ٱلدُّعَآءِ

TAfsiri..

"Alhamdulillahi! Himdi zote ni za Mwenyezi Mungu aliye nipa juu ya uzee wangu Ismail na Is-haq. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusikia maombi."


Aya ya Tatu


Suratul Baqarah aya ya 127

وَإِذْ يَرْفَعُ إِبْرَٰهِۦمُ ٱلْقَوَاعِدَ مِنَ ٱلْبَيْتِ وَإِسْمَٰعِيلُ رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّآ ۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ

Tafsiri:

"Na kumbukeni Ibrahim na Ismail walipo inyanyua misingi ya ile Nyumba wakaomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi."


Aya Ya nne:

Suratul Baqarah aya ya 136

قُولُوٓا۟ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَآ أُنزِلَ إِلَىٰٓ إِبْرَٰهِۦمَ وَإِسْمَٰعِيلَ وَإِسْحَٰقَ وَيَعْقُوبَ وَٱلْأَسْبَاطِ وَمَآ أُوتِىَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَمَآ أُوتِىَ ٱلنَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍۢ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُۥ مُسْلِمُونَ


TAFSIRI:-

"Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake."


Ziko nyingi ila kwa leo Chukua Hizo.labda nyongeza ni 2:133
 
Rudi kwenye Post Yangu comment namba #337
 
Sawa,..kwanza naomba tuweke biasness pembeni ili tupate jibu sahihi la mtoto yupi hasa aliyetaka kuchinjwa au kutolewa dhabihu kama ulivyosema........

Kwa nilivyofuatilia huu mjadala kuna hoja moja ambayo nadhani ndiyo ya wazi kabisa ameigusia DR Mambo Jambo ..... hoja ya umri wa wahusika pindi amri ya kuchinjwa ilivyotoka.....DR ameweka verses za Biblia ambazo zinaonyesha wazi kwamba wakati amri inatoka Ismail ndiyo mtoto pekee wa Ibrahim ambaye alikua ana :-
1. Uwezo wa kuongea (kama ilivyoonyeshwa kwenye biblia akijadiliana na Baba yake)
2. Uwezo wa kutembea zaidi ya Km 300,..kuelekea eneo ambalo tukio la kuchinjwa ilikua lifanyike.

NB: kwa mujibu wa hoja nilizopitia humu Ismail alikua na umri wa miaka 14,.wakati amri ya kuchinjwa inatoka........vipi kuhusu Ndugu yake alikua na umri gani? huenda alikua hajazaliwa au alizaliwa miezi michache baada ya tukio hilo.


So,. kimsingi kwenye hoja ya umri wa watoto husika... dadisi zinaonyesha Ismail ndiyo muhusika kwenye ishu ya kuchinjwa..endapo tukiondoa ushabiki nadhani tunaweza kukubaliana juu ya hili.
 
Sasa Ndugu.

Unaamini kulingana na biblia Ismael alibarikiwia, alizidishiwa na ahadi nyingi tu alipewa na nikweli hizi baraka alizipata

Kwanini usiiamini hio hio biblia iliosema, isaka ndio aliyetaka kutolewa kafara? Kwanini usiiamini hio hio biblia iliyosema mtoto wa ahadi ni isaka na upo ushaidi kwenye biblia.

Kama unaamini Qur'an, kwanini utetezi wako usijitenge na biblia ukaelezea kupitia Qur'an. Kama unaamini bible kwanini usitumie bible yenyewe

Mimi nachukia sana mtu anaeonganisha hivi vitabu viwili kwenye kuelezea point zake. Maana havina uhusiano wowote. Zaidi ya mgawanyo wake unaonzia kwa ibrahimu

Biblia imeshaelezea . Sasa tunasubr ushahidi kutoka kwenye Qur'an.
 
Unahangaika na nini wewe,vitu muhimu vyote kwenye QUR'AN vipo,ibada,sheria,mahusiano ya kijani,tawhiid...haihangaiki na birthday za watu
 
Hakuna Mtu anayejua Historia Ya Ishmael au waishmael zaidi ya Kutajwa kwenye Biblia na kwemye Historia mara kadhaa kama Wafanyabiashara maarufu..

Kuhusu baraka watoto waliobarikiwa wa Ibrahimu ni wawili.tu Ishmail na Isaka ila wengine 6 waliobali hawakubalikiwa Unafikiri kwanini?
 
Ibrahim mwarabu wa Iraq toka mji wa ur,180km kaskazini mwa saudia
 
Mimi nimeshangaa sana kusikia Hivyo maana Kuna aya Zaidi ya 10 zikimtaja Ismili na kuna moja illnataka kuhusu dua yake nimesahau ilipo nilikunbuka nitaileta..
Faiza kiukweli Anateleza
yes,.sahihi kaka hapo ameteleza...........ila tatizo Madam sidhani kama atakubali kwamba ameteleza... maana akikubali nadhani binafsi itakua mara ya kwanza kumuona akikiri kuteleza hapa JF.... Madam ni mtata Hahh 🙌
 
Mkuu nahisi haunifahamu Vizuri!
I am the Factual comparison person..

Huwa siegemei upande kama Shabiki Eti kwa kuwa naamini Hiki basi nikitetee..

Wanaonifahamu Jf Siku nyingi wanafahamu hilo..
Na ndo maana Naweza nikatoa Facts hata Kwa kutumia Hinduism au Hata other mystery kama wako sawa..

Narudia tena Kuhusu Mtoto aliyetolewa Kafara kwa Quran Haikutaja Jina ila wachambuzi na watafsiri wengi husema ni Ishamael..

Na stori iliyopo kwenye Biblia imetaja na imeleeza But Ni unlogical na Ni factual wrong..

Inaeleza kuwa Kipindi Ibrahimu akiwa na miaka 100 ndo Kipindi Mungu anamjaribu..

Lakini Biblia Inasema Isaka amezaliwa Ibrahimu akiwa na Miaka 100 na Ishamaili amezaliwa ibrahim akiwa na miaka 86..

Kwahyo kipindi Ibrahim akiwa na miaka 100 Isaka alikuwa na miezi na Ishmaili alikwa na miaka 14..

Na ndo kipindi ameagizwa kumtoa mtoto kafara..

Its True kwamba story ipo na Inasomeka But its Logical fallacy na Ina alot of Contradiction..

How comes mtoto wa Miezi kadhaa atembee Km 250 kwenda Kufanya kafara na How comes Hajaifikisha hata miaka na aweze kuongea..?

Try To think dont Confuse Faith, Beleive and Facts...
And FYI try to Reason Kila kitu
 
Mtume Muhammad S .A.W alisema msibishane kuhusu dini pasipo kuwa na elimu ......

Bismillah arahmanni rakhim
 
Sinai Zamani ilikuwa saudia kabla ya Ugawaji wa Mipaka..
Ingawa kwa sasa Iko katika Sinai penisula ambayo ni Kati kati ya Saudia, Jordan na Misri

Kwahyi jibu ni yes iko Saudia
DK Mambo Jambo, binafsi nakushukuru kwa uchambuzi mzuri sana.
Uko vizuri na umedhihirisha usomi wako
Ila ukweli unasimama kama ukweli.
 
Kwanza wekeni hapa hiyo Quran inayosema Ismail ndiyo alitakiwa kutolewa dhabihu.

Kwa upande wa Biblia ipo wazi ni kitabu cha Mwanzo 22:1-19. Abrahamu anataka kumtoa mwana wake wa pekee.

Jua pia kupitia Isaka ndipo anakuja kupatikana Yesu, ambaye Mungu alimtoa Mwanae wake huyo wa pekee kuwa dhabihu.

Kitabu cha mwanzo 24:5-6, Abrahamu anamrithisha Isaka Mali zake zote, ila watoto wake walizaliwa na Masuria wake walipewa Zawadi na kutakiwa kwenda mbali na Isaka huko Mashariki ya Kati.

So uzao wa Masuria haukuwa na mipango endelevu ya Mungu.
 

Unajua Ndugu.

Kwenye umri wa Isaka na Ibrahimu, inaweza kuwa changamoto kama isaka alikua bdo mchanga wakati wa kutolewa kafara.

Ukisoma Mwanzo sura 21.
21:8 inaonesha mtoto alikua akaachishwa kunyonya. Hii inadhihirisha mtoto alikua sio mchanga.

21:14 Ismael na mama yake wanatoka ili isaka asiwe mrithi pamoja na isaka.

21:34 Ibrahimu akakaa kwenye nchi ya wafilisti miaka mingi.

Sura 22.
Mungu anakuja kumjaribu Ibrahimu kuhusu kafara.
mwanz 22:1 tena inasema ikiwa baada ya mambo hayo yaan mambo ya Mwanzo 21 kupita.


Swali langu, Nini au kipi kinakuthibitishia wakati isaka anatolewa kafara alikua bdo mchanga?

Kama ibrahimu alikaa kwenye nchi ya wafilisti miaka mingi kwenye mwanz 21:34, ilikua ni baada ya kumzaa isaka au isaka alikua bdo ajazaliwa?
 
Ni naona thread ifungwe maana imejibu kila kitu hapa..
 
Ndugu yangu mwandishi mahiri. Kama sehemu ya jibu lako nakuzawadia kitabu kitabu hiki, kisome utafaidika sana.
Kitabu kimeandikwa na waislamu lazima wajipe promo wao.. siwezi kusoma maandiko yeyote yaliyoandikwa na waislamu yanaimpure ukweli
Mtoto wa pekee ni mtoto halali wa kwenye ndoa (Sarah na Ibrahim)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…